Jinsi ndoa ya ''karaha 'ilivyomsaidia kuyaokoa maisha ya maelfu ya watu

Uma Preman

Ndoa za kupangwa mara nyingi zinaweza kuwa za kushangaza. Ndoa ya masaibu ya Uma Preman haikubadili maisha yake pekee, bali maisha ta maelfu wengine- kwasababu ilimuachia ujuzi na motisha ya kuwasaidia Wahindi wenzake wasiojiweza kupata matibabu.

Uma wakati wote alikua na ndoto ya kuwa na harusi nzuri isiyo na kasoro katika madhabahu ya kitamaduni Kusini mwa India. Alikua akifikiria harusi yake itakua na mapambo ya kila aina yenye maua ya rangi za kuvutia

Lakini hilo halikutokea.

Uma bado anakumbuka mwezi wa Februari uliokua kana kwamba umetanda wingu la majivu. Ilikua ni asubuhi mwezi huo miaka 30 iliyopita wakati mama yake alipomtambulisha kwa Preman Thaikad. Uma alikua na umri wa miaka 19 tu, na Preman alikua na umri wa miaka 26.

Hakuwa wamewahi kukuana kabla, lakini aliambiwa kuwa alikua mumewake. Hapakuwa na sherehe wala muziki na akaamnbiwa hakutakuwa na harusi yoyote.

" Mama yangu aliniambia sasa mimi ni mali ya Preman. Aliniambia kuwa mimi ni mke wake , lakini sina haki kwa mali yake," anasema Uma.

Preman alimchukua nyumbani kwake na kumuacha usiku. Bado anakumbuka kuwa hakuweza kupata usingizi na badala yake alikodolea macho tu ukuta uliokua na rangi ya manjano iliyofifia na feni iliyokuwepo katika nyumba hiyo.

Asubuhi iliyofuatia , Preman alirejea saa kumi nambili asubuhi na akamuomba amsindikize kwenye baa. Akaendelea kunywa pombe kwa saa kadhaahuku Uma akiwa ameketi kimya, akijaribu kufikiria jinsi maisha yake yake yalivyochukua mkono wa ajabu.

Alimwambia yeye ni mke wake wa pili, lakini akafahamu kuwa alikuwa ni mke wa nne. P{ia alifichua kuwa alikua anaugua ugonjwa wa kifua kikuu mbaya na kwamba lengo la kumuoa lilikua ni amtunze.

Kabla

Uma alikulia katika mji wenye shughuli nyingi wa Coimbatore, uliopo katika jimbo la kusini mwa India la Tamil Nadu. Akiwa mtoto alitakua kuwa daktari kama baba yake, TK Balakrishnan.

Balakrishnan alikuwa alisomea udaktari kwa mwaka kabla ya kaka yke kumuomba kuacha masomo na kufanya kazi katika shamba lake. Alijifunza matibabu ya msingi na alikua na ujuzi wa kufunga vidonda. Uma alisikia familia za wagonjwa ambao alikua akiwatibu mara kwa mara- kwa hiyo alianza kuambatana na baba yake kila mara alipozunguka kuwatibu watu.

"Ninapenda tu chakula na kula na ndio maana nilizungunga na yeye," alisema.

lakini siku moja liona kitu ambacho kilimfanya agundue ni jinsi gani kazi ya baba yake ilikua ni ngumu. Baba yake alikua anamtibu mgonjwa aliyekua anaoa sehemu za mwili wake. Uma anasema alikua na maumjivu ambayo si ya kuvumilika.

Alikua anatumjia glovu zinazovaliwa katika bustani kwasababu hakuwa na glovu za upasuaji, lakini alimua mtulivu.."

Lakini mama yakeUma alichukia jinsi bwana yake alivuokua alitumia muda wake mwingi kuwasaidia wengine, anasema Uma

Alipokua na miaka minane, mama yake alimpa pesa kununua mishumaa kwa ajili ya sherehe za kinindi za Diwali - na aliporeea , mama yake alikua ameondoka.

"Nilibaini kuwa alimpenda mwanaume mwingine na aliondoka nae ," anasema Uma.

Ghafla ilikuwa ni jukumu la Umakumtunza kaka yake aliyekua na umri wa miaka mitatu. Anasema hakujua kupiga, lakini aliamua kujifunza kwasababu hakustahimili chakula walichopikiwa na baba yao.

" Nilikwenda katika makazi yaliyo karibu na nyumbani na kuwaomba wasichana wanifundishe. Walisema nisingeweza kupika kwasababu nilikua mdogo, lakini katika muda wa siku chache walikua wamemfunza kupia vyakula vya aina mbali mbali.

Miaka baadae Uma alipokua na umri wa miaka 17, alienda na baadhi ya majirani kutembelea hekalu maarufu katika Guruvayur -maili 87 kutoka Coimbatore - na huko alikutana na mwanaume ambaye alimwambia alimuona mwanaume aliyefanana kama yeye kabisaa.

Uma alimuachia anwani yake na siku chache baadae baua ikawasili katika posta.

Ilikua ni kutoka kwa mama yake.

Uma alikimbilia Guruvayur kuungana na mama yake , lakini akagundua mara moja kuwa kulikua na tatizo. Mume wake wa pil alikua amekopa pesa nyingi , na halafu akamtelekeza-na wakopeshaji wake walikua wanadai malipo.

"Niliona watu wakija kumuona nyimbani kwke kila siku kumsumbua na kumtisha kwa ajili ya pesa," Uma anasema . "ilikuwa inasikitisha sana kushuhudia hali hiyo ."

Suluhu ya mama yake ilikua ni kumuoza kwa Umma ambaye alikua ana pesa nyingi ili aweze kulipa madeni. Alijaribu kukataa na kutafuta kazi , lakini hatimae ilibidi akubali.

''Nilijihisi nisiye na thamani. Nilikubali tu hatma yangu na nikaenda kuolewa na Preman."

Baadae

" Kila siku alipoondoka kwenda kazini, Preman alinifungia ndani ya nyumba ," alikumbuka Uma.

"Sikuruhusiwa kukutana na mt u yeyote a kwenda nje- hata kwa dakika mija. Kwa miezi sita nilikua peke yangu. Nilipoteza hali ya kujiamini na ujiheshimu."

Kadri miaka ilivyokwenda , kifua kikuu cha Preman kiliendelea kuwa kibaya zaidi. Wawili hao wakaanza kutumia muda wao mwingi hospitalini, na mwaka 1997, miaka saba badae Preman akafariki . Ingawa wakati mmoja aliwahi kusema kuwa hana haki ya mali zake, alimuachia mali zote alipokufa

Uma anasema alijihisi huru kw amara ya kwanza maishani mwake.

" Sikutaka afe, lakini nilihisi nimepata fursa ya pili ya maisha."

Maelezo ya picha,

Uma na picha ya mume wake

Ilimchukua muda kutambua ni nini anachotaka kufanya katika uhuru wake mpya.

Katika miaka yake ya maisha na Preman, Uma alikua amegundua kwamba wtu maskini walikua mara kwa mara hawana uweo wa kupata matibabu yanayofaa , si tu kwa sababu hawakuwa na uwezo , bali pia kwasbabu hawakuwa na haki ya kupata taarifa-hawakujua matibabu na vifaa vya matibabu havikuwa vinapatikana.

Kwa hivyo Uma alikua ameanza kuwasaidia , kujaza fomu kwa ajili yao , akiwaongoza kuwapata madaktari wanaowafaa na wakati mwingine kuwasikiliza tu matatizo yao.

Muda mfupi watu walianza kumpigia siku wakiomba ushahidi na hivyo ndivyo kituo cha habari cha Santhi- Santhi Medical Information Centre kilivyozaliwa. Uma alikuwa amepata wito wa maisha yake-hakuwa anawatibu watu , kama baba yake, lakini alikuwa anawasaidia kupata matibabu.

Hata hivyo kuwasaidia watu ilibidi Uma kupate ujuzi mwanyewe na kwasababu miaka ya 1990 hapakua na intaneti ilibidi asafiri mbali katika hospitali mbali mbali kupata taarifa kuhusu matibabu na kuziweka mahala ambapo watu wangezipata bure.

"Ilibidi nisafiri kwasbabu hakuna hospitali ambayo ilijibu barua ," anasema.

Katika kipindi cha muongo uliopita, kituo cha Santhi kimetoa kipaumbele kwa kuwasaidia wagonjwa wa figo.

Hapakua na vituo vya kutosha vya matibabu ya figo - dialysis nchini na kiwango cha watu kujitolea kuwapatia wagonjwa ini kilikua ni duni. Uma amekua akifanya juhudi kubadili hili, akichangisha pesa kwa ajili ya kufungua vituo vipya kwa wote

" Kituo chetu cha kwanza cha dialysis kilianza katika wilaya ya Thrissur Kerala. Sasa tuna vituo 20 kote nchini India. Watu wengi matajiri walijitolea kuchangia vituo hivyo ," anasema.

Uma anasema kuwashawishi watu kutoa figo zao sio rahisi kwasababu huwa mara nyingi wanahofu juu ya mathadha yake kwa afya zao.

Kwa hivyo aliamua kutoa mfano, na kutoa figo zake mwenyewe. Alimpatia yatima ambaye figo zake ziliharibika.

Maelezo ya picha,

Moja ya figo za Uma ilimsaidia Salil (pichani)kuishi maisha ya kawaida

Salil anasema anaishi kwasababu alipewa figo na Uma.

"Nilikua na umri wa miaka 26 nilipofanyiwa matibabu ya dialysis. Alipokuna na mimi , aliniambiakwamba atatoa fiogo yake kama nitaendela kufanya kazi baada ya upandikizaji wa figo."

Aliendela kufanya kazi-na baada ya muda alienda kufanya kazi na Uma.

Salil anasema Uma ni mwanamke anayeamini kabisha ukweli wa maneno ya Mahatma Gandhi kwamba "unapaswa kuwa mabadiliko unayotaka kuyashuhudia ".

" Kilamyu anataka kubadilisha dunialakini hakuna hata mmoja ambaye yuko tayari kubadilika mwenye ," Uma anasema. "Nilibadili mtizamo wangu na nikatoa figo langu kama msaada, lakini pia nikampata kaka ."

Picha zote na Sivaram V