Urusi inajaribu kumsaidia rais Trump kushinda uchaguzi wa urais, wabunge wa Marekani waambiwa

File photo: Donald Trump na Vladimir Putin in 2017

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Trump alidaiwa kukerwa kuhusu mkutano huo wa maswala ya uchaguzi

Kitengo cha ujasusi cha Marekani kimeonya kwamba Urusi inajiribu tena kumsaidia rais Donald Trump kuchaguliwa tena katika uchaguzi wa mwezi Novemba kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani.

Matamshi hayo yanajiri baada ya mkutano wa faragha uliofanywa na kamati ya kijasusi mnamo tarehe 13 mwezi Februari , maafisa waliambia vyombo vya habari.

Rais Trump alidaiwa kukasirika , akilalama kwamba wanachama wa Democrats watatumia habari hiyo dhidi yake.

Alimbadilisha afisa mkuu wa ujususi Joseph Maguire siku ya Alhamisi. Gazeti la The New York Times liliripoti kwamba bwana Trump alikerwa kwamba Adam Schiff , mwanachama wa Democrat aliyeongoza kesi dhidi yake alikuwa katika mkutano huo.

Bwana Trump alishtakiwa na bunge la uwakilishi nchini Marekani kwa utumiaji mbaya wa mamlaka na kuzuia bunge la Congress. Aliondolewa makosa baada ya kesi hiyo iliochukua takriban wiki mbili katika bunge la seneti linalodhibitiwa na wanachama wengi wa Republican.

Wakati wa mkutano huo , wafuasi wa bwana Trump walihoji kwamba rais huyo alikuwa amechukuwa msimamo mkali , na kwamba ushirikiano wake na mataifa ya Ulaya umeimarishwa kutokana na hilo, lilisema gazeti hilo.

Bwana Schiff baadaye alituma ujumbe wa twitter kwamba iwapo bwana Trump alikuwa akiingilia kati ugawaji wa habari kati ya kitengo cha ujasusi cha Marekni na bunge la Congress kuhusu uingiliaji wa kigeni katika uchaguzi mkuu , rais alikuwa anahatarisha jaribio la kuzuia.

Bwana Maguire alikuwa anapigiwa upatu kuteuliwa kuchukua wadhfa huo wa Mkurugenzi wa kudumu wa shirika la kijasusis , lilisema gazeti la The washington Post.

Hatahivyo, gazeti hilo lilisema kwamba rais alibadili msimamo wake wakati alipogundua kuhusu mkutano huo na kile alichokitaja kama ukosefu wa utiifu kutoka kwa wafanyakazi wake.

Rais alitangaza wiki hii kwamba bwana Maguire atabadilishwa na Richard Grenell , balozi wa Marekani nchini Ujerumani na mwandani wa rais Trump.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Richard Grenell, balozi wa Marekani nchini Ujerumani aliteuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi wiki hii

Maafisa wawili wa utawala wa rais Trump waliambia gazeti la New York Times kwamba ubadilishaji wa Maguire muda mfupi baada ya mkutano huo uliojaa utata ulikuwa bahati.

Maafisa wa kitengo cha ujasusisi nchini Marekani wanasema kwamba Urusi iliingilia uchaguzi mkuu wa urais 2016 ili kupiga jeki kampeni ya rais Trump na kuzua ghasia katika mchakato mzima wa uchgauzi nchini Marekani.

Wanachama wa Democrats walimkosoa rais kwa kumchagua bwana Grenell ambaye awali alipinga kiwango cha Urusi kuingilia uchaguzi uliopita wa Marekani na amepongeza kuongezeka kwa wanasiasa wa mrengo wa kulia barani Ulaya.

Ned Price mshauri wa zamani wa mtangulizi wa rais Trump, Barrack Obama alisema kwamba rais alipuuzilia mbali wazo lake kwamba hatumii ujasusi.

''Tayari amemteua mwanasiasa na balozi wa Marekani aliye mkakamavu zaidi kwa kile kilichotarajiwa kuwa jukumu dhaifu'' , alituma ujumbe wa Twitter.