Thomas Thabane: Waziri mkuu wa Lesotho aondoka nchini huku mashtaka ya mauaji yakimkabili

Thomas Thabane

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Thomas Thabane has announced that he will step down in July

Waziri mkuu wa Lesotho Thomas Thabane amekosa kufika mbele ya mahakama ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe wa zamani 2017.

Mshauri na mwana wa Thabane na mtoto wake anasema kwamba mzee huyo mwenye umri wa miaka 80 anapokea matibabu katika taifa jirani la Afrika kusini.

Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa na mauaji. Bwana Thabane atakuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kushtakiwa na mauaji akiwa afisini katika kesi iliolishanagaza taifa hilo dogo la Ufalme wa milimani.

Hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo. Maafisa wa polisi siku ya Alhamisi walisema kwamba atashtakiwa na mauaji siku ya Ijumaa. Alitarajiwa mahakamani mapema leo, kulingana na ripoti za Reuters.

Hakwenda mahakamani , alienda Afrika kusini kwa matibabu , alisema katibu wake Thabo Thakalekoala akizungumza na chombo cha habari cha AFP, na kuongezea vilikuwa vipimo vya matibabu vya mara kwa mara.

Lakini naibu kamishna wa polisi Paseka Mokete aliambia waandishi habari kwamba alikuwa hajui kuhusu aliko bwana Thabane , lakini akasema kwamba iwapo angekuwa nje ya taifa akipokea matibabu basi wangelazimika kusubiri ili kuendelea na kesi atakapowasili.

'Hatuwezi kwa sasa kusema kwamba alikiuka agizo la mahakama''.

Mkewe wa kwanza bwana Thabane ,58. alipigwa risasi katika mji mkuu wa Maseru, siku mbili kabla ya bwana Thabane kuwa waziri mkuu 2017.

Chanzo cha picha, The Post

Maelezo ya picha,

Bwana Thabane alimuoa Maesaiah katika hafla iliofanyika 2017

Alisema katika chombo cha habari siku ya Alhamisi kwamba alihudumia taifa na kwamba atastaafu mwisho wa Julai. Nimefanya kazi ya kuhakikisha kwamba kuna usalama na uthabiti Lesotho.

Leo...katika umri wangu, nimepoteza nguvu zangu nyingi ,alinukuliwa akisema.

Hakutaja madai dhidi yake. Chama tawala cha All Basotho Convenstion kilikuwa kimempatia siku ya mwisho ya Alhamisi kujiuzulu.

Je mauaji hayo yalifanyika vipi?

Chanzo cha picha, Lesotho Times

Maelezo ya picha,

Lipolelo alikuwa amepinga talaka iliowasilishwa na waziri mkuu

Lipolelo alipigwa risasi akiwa karibu kandokando ya barabara chafu alipokuwa akirudi nyumbani katika kijiji kidogo kandokando ya mji mkuu wa Maseru.

Alikabiliwa na talaka mbaya iliojaa chuki na bwana Thabane wakati alipouawa. Wakati huo, waziri mkuu alikuwa akiishi na Maesaiah, mwenye umri wa miaka 42 kama ambaye alikuwa mkewe.

Bwana Lipolelo alikua tayari ameshinda kesi ya kutambuliwa kama mke wa kwanza wa waziri mkuu badala ya Maesaiah.

Maesaiah akiandamana na bwana Thabane wakati alipokuwa akila kiapo baada ya kifo cha mkewe wa kwanza.

Miezi miwili baadaye yeye na bwana Thabane walioana katika sherehe ya kikatoliki iliofanyika katika uwanja wa Maseru uliojaa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maesaiah akiwa jumba la waziri mkuu mapema wiki hii

Maesaiah alishtakiwa na mauaji ya mke mwenza tarehe 5 mwezi Februari na sasa yuko nje kwa dhamana ya dola 67.

Pia ameshtakiwa na jaribio la mauaji ya rafikiye Thato Sibolla ambaye alikuwa na Lipoleo wakati huo wa ufyatuuaji wa risasina anatarajiwa kuwa shahidi mkuu katika mauaji hayo.