Virusi vya Corona: Jinsi unavyoweza kufanikiwa binafsi kujitenga ili kuepusha maambukizi.

Generic picture of woman at home on a sick day

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Watu wanaweza kuombwa wabaki nyumbani kwa muda wa wiki mbili kama walikuwa karibu na watu wenye maambukizi ya virusi vya corona

Watu wengi wanaweza kuwa wataombwa wajitenge na wengine ili kuepuka kueneza virusi vya Corona kutokana na kuenea kwa ugonjwa huo.

Lakini unapaswa kufanya nini ikiwa uko hatarini?

Zaidi ya watu 80 kwa mfano wametengwa nchini Uingereza kwa uchunguzi wa Virusi vya Corona.

Hakuna idadi rasmi za watu walioshauriwa kujitenga na watu wengine, lakini hatua ya kujitenga binafsi inaonekana kama njia muhimu ya kupunguza usambaaji wa virusi.

Lakini kujitenga mwenyewe inamaana gani na ni vipi unaweza kuhakikisha kujitenga kwako kunakuwa na mafanikio?

Chanzo cha picha, EPA

Ni nani anayepaswa kujitenga?

Unahitaji tu kujitenga kama umeambiwa ujitenge na maafisa wa afya.

Kwa kawaida wanaoambiwa wajitenge ni wale ambao''wamekua karibuni ama wako karibu'' na watu binafsi ambao walithibitishwa kuwa na virusi- waliobainika kukaa dakika 15 katika umbali wa mita mbili kutoka alipo mtu alieambukizwa.

Inakua ni lazima kujitenga na watu hususan kama umesafiri katika maeneo ya ndani ya China, Thailand, Japan, Korea kusini, Hong Kong, Taiwan, Singapore, Malaysia au Macau katika kipindi cha siku 14 zilizopita na una dalili kama vile kikohozi, homa ya mwili na kushindwa kupumua vizuri.

Katika hali kama hii, usiende kwa daktari au kituo cha afya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ukiwa na dalili za virusi vya Corona unashauriwa kujitenga binafsi ili kuepuka maambukizi zaidi

Badala yake kaa nyumbani.

Unashauriwa kuwasiliana mara moja na maafisa wa afya au hopsitali ili kupata usaidizi wa haraka wa matibabu.

Unapaswa kufanya nini unapojitenga kwa ajili ya kutoambukiza watu wengine virusi vya Corona?

Ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya ni kwamba ''ni jambo la kutumia akili ya kawaida'' jizuwie kukaribiana na watu wengine kadri uwezavyo - kama vile tu ambavyo ungefanya kama ungekua na mafua.

Hii ina maana kuwa unapaswa kubakia nyumbani kwa siku 14, na kutoenda kufanya kazi, shule au katika maeneo ya umma.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Usiende madukani au sokoni - agiza bidhaa au muombe rafiki akusaidie

Unapaswa kukaa kwenye chumba chenye hewa safi ya kutosha chenye dirisha linaloweza kufunguliwa, tofauti na vyumba vya watu wengine nyumbani kwenu.

Pia usiwakaribishe wageni kwako.

Ni vipi kama unaishi na mtu ambaye amejitenga kutokana na virusi vya Corona?

Ingawa inaweza kuwa vigumu kujitenga na mtu kutoka familia yako ama jirani yako kabisa, ushauri ni kuwa na ukomo wa ukaribu na mtu anayeshukiwa kuwa na maambukizi kwa kadri uwezavyo.

Ushauri wanaopewa watu wenye uwezekano wa kuugua virusi vya Corona ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni kwa walau dakika 20- hususani baada ya kugusana na mgonjwa au kugusa kifaa au kitu alichokigusa au kukitumia.

Inashauriwa usitumie vifaa vya nyumbani na mtu ambaye ametengwa.

Pia kama wanachumba tofauti na kama inawezekana wanapaswa kuwa na choo na bafu lao.

Inashauriwa pia kuonsha sakafu ya nyumba kila siku, kwa kutumia gloves kama unazo.

Uchafu ambao umetoka ama umeguswa na mgonjwa aliyetengwa unapaswa kuwekwa kwenye karatasi ya plastiki ya uchafu na kufungwa na kuwekwa katika karatasi nyingine.

Maelezo ya video,

Virusi vya Corona: Hospitali iliyojengwa ndani ya siku 10