Riek Machar: Riek Machar aapishwa kuwa makamu rais wa kwanza huku Rebecca Garang akiwa makamu ya pili

Riek Machar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Riek Machar

Aliyekuwa kiongozi wa waasi Sudani Kusini Riek Machar ameapishwa kama makamu rais wa kwanza katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Juba.

Rais Salva Kiir alishuhudia sherehe hiyo pamoja na Fattah Al-Burhan, mwenyekiti wa Baraza la Sudan pamoja na wawakilishi kutoka washirika wake wa eneo.

Hii ni baada ya rais wa Sudan Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi huyo wa zamani wa waasi Riek Machar kukubaliana kuunda serikali ya mpito ya Umoja ya Taifa, kabla ya tarehe 22 Februari.

Inaaminiwa kuwa hatua hii itasaidia kurejesha amani ya kudumu nchini Sudan Kusini, lakini mikataba mingi ya amani imekua ikivunjwa mara kwa amara.

Bwana Machar alikubali kuchukua nafasi yake ya awali ya makamu rais, na serikali ya sasa itavunjwa ili kutoa fursa kwa wajumbe zaidi wa upinzani.

Baadhi ya masuala bado hayajatatuliwa, mkiwemo kugawana madaraka na suala la kuwajumuisha wapiganaji wa waasi lakini lakini wamekubailiana kuunda serikali na kutatua matatizo mengine baadae.

Mkataba ulitangazwa saa kadhaa baada ya Umoja wa Umoja wa Mataifa kutoa ripoti inayozishutumu pande zote kwa kusababisha njaa kwa raia kwa makusudi wakati wa vita vya awenyewe kwa ajili ya kupigania madaraka.

Maelezo ya picha,

Rebecca Garang pia ameapishwa kuwa makamu wa rais

Makamu wengine watatu wameapishwa katika hafla hiyo , akiwemo Rebecca Garang, mke wa John Garang - mwanzilishi wa taifa la Sudani Kusini:

Mmoja ya makamu hao atateuliwa na muungano wa upinzani - Muungano wa Upinzani wa Sudani Kusini lakini bado haujakubaliana nani atakayewawakilisha.

Makubaliano yana umuhimu gani?

Tumaini ni kwamba mkataba utamaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka sita, ambavyo vimewauwa watu wapatao 400,000 na kuwasambaratisha raia wake milioni 12.

Rais Kiir ameelezea matunaini kwamba kipindi cha mpito cha miaka kitatoa fursa kwa wakimbizi na raia waliosambaratishwa na mapigano ndani ya nchi kurejea katika nyumba zao.

Zaidi ya hayo idadi kubwa ya watu waliokufa na mamilioni walioikimbia nchi yao, wengi wamelazimika kukumbwa na njaa na wanakabiliwa na magumu ambayo hayajaelezwa.

Kama mkataba utadumu, utasaidia mwanzo mpya katika taifa hilo jipya zaidi duniani.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Salva Kiir na Riek Machar walikubaliana kuunda serikali ya mpito kama sehemu ya mkataba wa amani uliosainiwa mwaka 2018.

Je mapigano yalikuwa ni juuya nini

Sudan Kusini ilipata uhuru wake tangu mwaka 2011, ambao ulimaliza vita vya muda mrefu. Lakini haikuchukua muda kwa ahadi ya amani kuvunjwa

Miaka miwili tu baada ya uhuru, nchi ilirejea katika mzozo mwezi wa Disemaba 2013 baada ya rais kiir kumfuta kazi aliyekua makamu wake Riek Machar.

Rais Kiir alikua amemshutumu Bwana machar kupanga njama ya kumpindua , shutuma ambazo Machar alizikana.

Huku vita vikiwa na msiingi wa kisiasa, ilikua pia na misingi ya kikabila na pia juu ya mahusiano.

Unaweza pia kusoma:

Makabila ya Dinka na Nuer, ambayo ndio makubwa zaidi nchini humo, wanakotoka viongozi hao wawili, yamekua yakushutumiana kila kabila kulilenga jingine katika vita, na maasi yaliyotekelezwa na pande zote.

Ni kwanini imekua vigumu sana kufikia mkataba wa amani?

Pande husika hazikuweza au hazikuwa na utashi wa kukubaliana juu ya masharti ya uundwaji wa serikali ya mpito, kulingana na makubaliano ya mwaka 2018.

Mkataba ulipaswa kukamilika mwezi Mei 2019, lakiniuliahirishwa mara mbili- maklataa ya mwisho yakiwa ni tarehe 22 Februari.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Bwana Machar hajaishi mjini Juba kwa muda tangu mwaka 2016

Mzozo katika nchi ya Sudan umelisukuma taifa hilo katika hali mbaya ya kibinadamu.

Licha ya hali hiyo, imekuwa ni vigumu kwa pande husika kudikia na kuimarisha mkataba wa amani ambao unaweza kuleta amani na uthabiti wa taifa.

Maisha yako vipi Sudan Kusini?

Ni nchi yenye ukame. Shirika lfedha duniani (IMF) liliiitaja kama nchi maskini zaidi duniani, kwa pato la ndani ya nchi kwa mtu . Sehemu kubwa ya nchi haijaendelea kwa miundombinu. Kwa mfano ina takriban kilomita 300 njia badala ya barabara, katika nchi yenye kilomita 600,000 za mraba.

Sehemu kubwa ya nchi nje ya miji haina maji wala umeme.

Getty Images
South Sudan

World's youngest country

  • 12mPopulation

  • 2011Year of independence

  • 2013Conflict started

  • 4.3mCitizens displaced from their homes

  • 82%of people live on less than $1 a day

  • 65%of the population can't read or write

UN Agencies

Sudana Kusini pia ni moja ya nchi yenye viwango vya chini zaidi vya watu wanaojua kusoma na kuanzika elimu duniani cha 34.5%, kwa mujibu wa Unesco (2018).

Shirika la Umoja wa mataifa la watoto, Unicef, linakadiria kuwa 70%( takriban milioni 2.2) ya watoto hawaendi shule-jambo ambalo linahatarisha hali yao ya baadae na ya nchi yao .Hii ina maanisha kuwa ni moja ya nchi eenye viwango vya juu zaidi vya watoto wasio shuleni duniani.

Kufikia mwaka 2019, zaidi ya nusu ya watu wake walihitaji msaada wa kibinadamu, wakiwa na viwango vya juu sana vya ukosefu wa usalama wa chakula kote nchini, kulingana na Benki ya dunia.

Nchi inategemea mapato ya mafuta karibu pekee na kuna uwekezaji mdogo katika sekta nyingine kama vile kilimo na miundo mbinu.

Maelezo ya picha,

Yar Ajak na John Mayen, ni vijana wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanaoishi na kusoma nchini Kenya, ambao wanasema wangependa sana kurejea kulijenga taifa iwapo amani itarejea

Je makataba ni hakikisho la amani ya kudumu ?

Hakuna hakikisho.

Mikataba ya awali ilikubalika na kuvunjwa muda mfupi baadae.

Kumekua na mikataba zaidi ya 10 na makubaliano ya usitishaji wa mapigano yaliyofikiwa na viongozi waliokosana mwaka 2013 na kutokuwa na kutokuwa kwao na uwezo wa kuimarisha mkataba wowote, mkiwemo juu ya mgawanyo wa madaraka.

Peter Adwok Nyaba, mwanahakati na waziri wa zamani nchini Sudan, anasema mkataba haumalizi kikamilifu masuala yanayoibua mzozo ukabila, kupoigania mamlaka na taasisi dhaifu za utawala, ambayo anasema bado yapo licha ya mkataba.

"Huu ni mzunguko usioisha: umaskini-mzozo-amani-ukosefu wa maendeleo-halafu mzozo," anasema.