Madada wa Cambodia wenye miaka 98 na 101, wakutana tena baada ya miaka 47

Bun Sen and Bun Chea

Chanzo cha picha, CCF

Maelezo ya picha,

Bun Sen, (kushoto) na Bun Chea walionana kwa mara ya mwisho mwaka 1973

Madada wawili wa Cambodia wenye umri wa miaka 98 na 101 -wamekutana tena baada ya miaka 47, huku kila mmoja wao akifikiria kuwa mwenzake alikufa wakati wa utawala wa kikatili wa Khmer Rouge miaka ya 1970.

Bun Sen, 98, pia walikutana na kaka yake mwenye umri wa miaka 92, ambaye alifikiri alikufa, limesema shirika moja lisilo la kiserikali.

Takriban watu milioni mbili wanadhaniwa kuwa walikufa chini ya utawala wa Khmer Rouge.

Familia nyingi zilitengana wakati wa kipindi hiki, huku watoto wakitengwa na wazazi wao wakati utawala ulipokua ukijaribu kuchukua udhibiti kamili wa nchi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mtawala wa wakati huo -Pol Pot (mbele) alionyesha dunia kwamba raia wa Cambodia wanamuunga mkono

Chanzo cha picha, CCF

Maelezo ya picha,

Bun Sen pia alikutana na kaka yake mwenye umri wa miaka 92, kushoto

Bun Sen alimpoteza mume wake chini ya utawala wa Pol Pot ambao ulipinduliwa mwaka 1979 na hatimae akaishi katika eneo lilililopo karibu na mahala pa kutupa taka Stung Meanchey katika mji mkuu, Phnom Penh.

Kwa muda mrefu aliishi katika eneo hilo la taka akijaribu kutafuta bidhaa anazoweza kusafisha na kuziuza, ili kuwatunza watoto wake katika makazi duni.

Alikuwa mara kwa mara akizungumzia kutembelea kijiji cha kwao kilichopo katika Kampong Cham, umbali wa maili 90 tu mashariki mwa mji mkuu Phnom Penh.

Lakini sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na umri wake na kutokuwa na uwezo wa kutembela, viliifanya ndoto ya kukitembelea kijiji chake kuwa ngumu kutimizwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Utawala wa Khmer Rouge ulikua madarakani kuanzia mwaka 1975-1979, na kuwaua watu milioni mbili

Khmer Rouge walikua ni akina nani?

  • Makatili wa Khmer Rouge, walikua madarakani kuanzia mwaka 1975-1979, waliwauwa watu milioni mbili
  • Utawala ulioongozwa na Pol Pot-ulijaribu kuirejesha Cambodia katika miaka ya zamani, na kuwalazimisha mamilioni ya watu kutoka maeneo ya mijini kufanya kazi katika mashamba ya ushirika vijijini
  • Umoja wa Mataifa ulijaribu kuanzisha mahakama ya kuendesha kesi za viongozi wanaoishi wa Khmer Rouge, iliyoanza shughuli zake 2009
  • Ni viongozi watatu tu wa zamani wa Khmer Rouge waliokwisha hukumiwa- Kaing Guek Eav, aliyeendesha jela la ukatili la Tuol Sleng jail, mkuu wa utawala Khieu Samphan na kamanda wa pili wa Pol Pot , Nuon Chea

Shirika lisilo la kiserikali la Cambodia linalosimamia watoto -ambalo limekua likimsaidia Bun Sen tangu mwaka 2004 - lilianza kupanga safari yake ya kumpeleka kijijini kwao.

Ni wakati huo waligundua kuwa dada yake na Bun Sen na kaka yake bado walikua hai na wanaishi katika kijiji chao.

Chanzo cha picha, Satoshi Takahashi/Getty Images

Maelezo ya picha,

Bun Sen aliishi karibu na dangulo la takataka la Stung Meanchey

Baada ya takriban karne, Bun Sen aliungana na dada yake mkubwa Bun Chea na kaka yake mdogo.

"Niliondoka kijijini kwangu siku nyingi sana zilizopita na sikurudi. Nilikuwa kila wakati nawafikiria dada zangu na kaka zangu nikidhani walikufa.

"Kumkumbatia dada yangu mkubwa tena ina maana kubwa sana kwangu. Na mara ya kwanza kaka yangu aliponisalimia nilianza kulia ."

Chanzo cha picha, CCF

Maelezo ya picha,

Baada ya kukutana madada walisafiri kutembea katika mji mkuu Phnom Penh pamoja

Chanzo cha picha, CCF

Maelezo ya picha,

Bun Chea, kushoto na Bun Sen wakibarizi katika mto Tonle Sap mjini Phnom Penh

Bun Chea, ambaye mume wake aliuawa na Khmer Rouge, na kumuacha na watoto 12, alisema kuwa pia aliamini dada yake mdogo aliuawa.

"Tulikua na ndugu wa damu 13 waliouawa na Pol Pot na tulidhani pia huyu dada yetu alikufa. Umekua ni muda mrefu sana," alisema.

Sasa madada hawa wana mengi ya kuzungumza baada ya muda mrefu sana. Wiki hii walikwenda katika matembezi katika mji mkuu pamoja.

"Tulimzungumzia," Bun Chea alisema. "Lakini sikufikiria tungemuona tena ."

Unaweza pia kusikiliza:

Maelezo ya sauti,

Habari za Global Newsbeat 1500 03/08/2017