Mwanzilishi wa shirika la maarufu za misaada L'Arche, Jean Vanier alinyanyasa wanawake.

Jean Vanier founded L'Arche in 1964

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiongozi wa kidini mwanzilishi wa shirika la wenye matatizo ya kusoma alinyanyasa wanawake sita nchini Ufaransa, kwa mujibu wa ripoti ya ndani.

Padri Jean Vanier raia wa Canada ni mwanzilishi wa shirika kubwa la kimataifa duniani la L'Arche nchini Ufaransa mwaka 1964, ambaye alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 90.

Miongoni mwa aliowanyanyasa hakuna hata mmoja ambaye ni mlemavu, ripoti hiyo inasema.

Uchunguzi dhidi ya Vanier ulipendekezwa mwaka jana na shirika aliloanzisha mwenyewe baada ya kuzuka kwa tuhuma hizo.

Ripoti kamili inatarajiwa kuchapishwa siku chache zijazo.

"Tumeshutuka kwa taaifa hizi na tuna laani vitendo hivyo, ambavyo vinakinzana na maadili ambayo Jean Vanier alidai kuwa nayo, na hayaendani kabisa na heshima na maadili ya mtu, tofauti kabisa na misingi ya shirika la L'Arche," hayo yameandikwa katika tovuti ya shirika la kimataifa la L'Arche.

Shirika hilo linaendesha makazi na vituo ambapo watu ama walio au wasio na ulemavu huishi kwa pamoja na linaendesha shughuli zake katika nchi 38 kote duniani lenye wanachama karibia 10,000.

Ripoti hiyo inasema nini?

Vanier, muumini mkatoliki mwenye msimamo mkali, aliwanyanyasa kimapenzi wanawake sita eneo la Trosly-Breuil, Ufaransa kati ya mwaka 1970 and 2005, kulingana na taarifa ya sharika aliloanzisha la kimataifa la L'Arche.

Mahusiano ya kimapenzi yalikuwa yanaanzishwa na Vanier kwa misingi ya kutoa mwongozo wa kiroho.

"Wanawake hawa walitoa madai ya kufanana yenye kuhusishwa na tabia fiche tofauti na mwongozo wa kiroho," taarifa hiyo imesema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jean Vanier alishirikiana na mfanyabiashara Philippe Pozzo di Borgo kuandika kitabu kuhusu wenye ulemavu

"Uhusiano huo [...] ulikuwa na athari mbaya katika maisha ya wahusika na mahusiano mengine yaliyofuata.

"Vitendo hivyo ni ishara ya uhusiano wa kipekee wa kisaikolojia na kiroho aliokuwa nao Jean Vanier kwa wanawake hawa," taarifa hiyo imesema.

Pia taarifa hiyo imesema kwamba Vanier aliomba wanawake hao kuwa wasiri katika mahusiano yao.

Wanawake hao ni pamoja na wasaidizi na watawa, kulingana na gazeti la Canada la the Globe and Mail,

Vanier pia alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na matendo yasiyo ya kawaida ya kimapenzi na askofu aliyefedheheshwa Thomas Philippe, kulinga na gazeti hilo.

Askofu Philippe, aliaga dunia 1993 na alikuwa baba wa kiroho wa padri Vanier.

Hata hivyo Vanier alikanusha hadharani kutekeleza vitendo kama hivyo, lakini ripoti hiyo imebaini kwamba alikuwa anatumia njia zile zile kwa aliokuwa nao mahusiano.

Vitendo vya padri Vanier "vimeonyesha kwamba aliiga na kuendeleza tabia na vitendo vya askofu Thomas Philippe kwa kipindi kirefu tu", kulingana na tarifa ya shirika la L'Arche.

Uchunguzi huo ulifanywa na shirika lisilopendelea upande wowote nchini Uingereza.

Padri Jean Vanier ni nani?

Kijana wa mwanadiplomasia wa Canada, aliacha unabaharia mwaka 1950 ili kusomea theoljia, akisema kwamba anataka kumfuata Yesu.

Akiwa amehudhuria kikao cha makasisi mjini Paris ambao walishirikiana na wanaume wenye matatizo ya kusoma, aliaanza kufadhaishwa na hali mbaya alizoshudia ambazo wanaume hao walikuwa wanazipitia.

Alianzisha shirika la L'Arche kwa watu wenye matatizo ya kusoma ili kuweza kuishi na watu wasio na ulemavu bila ubaguzi.

Kwa sasa kuna vituo 154 vya shirika la L'Arche kote duniani.

Vanier alichaguliwa katika shindano la Amani la Nobel paoja na kupewa tuzo lenye kuzingatia ubinadamu la 'Companion of the Order of Canada'.

2015, alipata tuzo nyengine ya 'Templeton Prize', huku Askofu Mkuu wa Kantabari, Justin Welby akiashiria kwamba hakuna anayestahili kushinda tuzo hio zaidi yake.