Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 23.02.2020: Bellingham, Aubameyang, Martial, Werner, Ruiz

Anthony Martial

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 24, ambaye analengwa na Inter ili kuchukua nafasi ya mashambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez

Mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 24, ambaye analengwa na Inter ili kuchukua nafasi ya mashambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, ambaye pia anawindwa na Barcelona. (Tuttosport, via Sunday Mirror)

Liverpool imeingia katika kinyanganyiro cha kutafuta kumsajili mshambuliaji, Jude Bellingham, 16, ambaye huenda akawagharimu £30 na pia amehusishwa na kuhamia Manchester United. (Star on Sunday)

Manchester City itapata ushindani kutoka kwa Real Madrid kwa mchezaji wa Fabian Ruiz, 23, ambaye inasemekana thamani yake ni £80m. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aubameyang katika mecho zote alizoshiriki kwenye ligi ya Premier Septemba, 2019

Inter Milan inajitayarisha katika kipindi cha usajili wa wachezaji huku ikimlenga mshambuliaji wa Arsenal raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang. (Sunday Express)

Leicester City itajaribu tena kumsajili kiungo wa kati wa Celtic £25m, Callum McGregor, 26, msimu ujao. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Werner, katikati, akifunga bao baadaya kupata penalti didi ya Tottenham

Mshambuliaji wa RB Leipzig, wa Ujerumani Timo Werner, 23, - ambaye amehusishwa na kuhamia Liverpool amemtaja kocha Jurgen Klopp "kama kocha mzuri duniani". (Mail on Sunday)

Mashambuliaji wa Aston Villa, Jack Grealish, 24, anachukulia maneno ya kwamba huenda akahamia Manchester United au Liverpool "kama uvumi". (Express and Star)

Mchezaji wa Manchester City, Under-21, Phil Foden, 19, anasema kwamba anafurahia kusalia katika klabu hiyo badala ya kuhamia kwengine kwa mkopo ili aweze kupata nafasi ya kujumuishwa katika orodha ya wachezaji wa kila mara wa timu. (Manchester Evening News)

Chelsea wameonyesha nia ya kumsajili mchezaji wa Inter Mauro Icardi, ambaye yuko Paris St-Germain kwa mkopo na huenda wakamtafuta wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa. (Sport Witness)

Sheffield United itaweka £20m katika hatua ya kutaka kumsajili mlinzi wa timu ya Leeds United nchini Uingereza, 23. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nemanja Matic has anayechezea Serbia

Kiungo wa kati wa Manchester United na Serbia Nemanja Matic, 31, anakata kusalia Old Trafford baada ya mkataba wake wa sasa kukamilika msimu huu. (Sunday Mirror)

West Ham United wako katika nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji Amiens, Serhou Guirassy kwa £23m ingawa Brighton naTottenham pia nao wameonesha nia ya kumsajili. (Sun on Sunday)

Chanzo cha picha, Perez Meca/MB Media

Maelezo ya picha,

Gareth Bale ameshinda ligi ya Champions mara nne akiwa na Real Madrid

Makubaliano ya mchezaji wa Real Madrid na Wales Gareth Bale, 30, kuhamia China kwa usajili wa bila malipo ulifanywa msimu uliopita kwa asilimia 90 lakini kila kitu kiliharibika baada ya klabu ya Uhispani kutaka kulipwa, amesema Jiangsu Suning coach Cosmin Olaroiu. (Goal.com)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 35, alifikia makubaliano na Real Madrid, 2008 kabla ya kwenda kuichezea Manchester United kwa mwaka mwengine. (Manchester Evening News)

Uingereza inapanga kuongeza uwanja wa Amex uwe ni wenye kuhudumia angalau watu 32,000 kutoka 30,750. (Argus)

Kiungo wa kati wa Lille and Ureno Renato Sanches, 22, anasema kwamba alilazimishwa kuhamia Swansea kwa mkopo. (Wales Online)