Tuzo ya Kumla Dumor 2020: Inamtafuta mwandishi chipukizi kutoka Afrika

Maelezo ya video,

BBC World News Komla Dumor Award 2019: Seeking a rising star of African journalism

BBC inamsaka mwandishi bora wa Afrika kwa tuzo ya BBC ya Komla Dumor, ambayo mwaka huu ni ya sita. Waandishi kutoka maeneo yote ya Afrika wamealikwa kuwasilisha maombi yao kujishindia tuzo hiyo, ambayo inalenga kugundua kukuza vipaji kutoka barani Afrika.

Mshindi atapata fursa ya kufanya kazi kwa miezi mitatu katika makao makuu ya BBC mjini London, akijipatia mafunzo na uzoefu. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 16 mwezi Machi 2020 mwendo wa saa tano usiku saa za mjini London.

Tuzo hiyo ilianzishwa kwa heshima ya Komla Dumor , raia wa Ghana aliyekuwa mtangazaji wa BBC World News ambaye alifariki ghafla mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 41. Tuzo ya mwaka huu inazinduliwa kutoka jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Tuzo hiyo itazawadiwa kwa mwandishi anayefanya kazi barani Afrika ambaye ni mwandishi stadi mwenye uwezo wa kutangaza na kusimulia habari mbali na kuwa na malengo ya kuwa nyota wa siku za baadae.

Mbali na kufanya kazi na BBC mjini London, mshindi huyo pia atapata fursa ya kusafiri barani Afrika ili kukusanya habari ambayo itasambazwa kote barani na duniani kwa jumla.

Washindi waliopita:

  • 2015: Nancy Kacungira wa Uganda
  • 2016: Didi Akinyelure wa Nigeria
  • 2017: Amina Yuguda wa Nigeria
  • 2018: Waihiga Mwaura wa Kenya
  • 2019: Solomon Serwanjja wa Uganda

Mshindi wa mwaka uliopita Solomon Serwanjja, aliripoti kutoka mji mkuu wa Nairobi kuhusu watu wanaopambana kuimarisha mazingira ya hewa mjini humo.

Nimehisi vizuri sana kushinda tuzo hii kwangu binafsi na kikazi, alisema.

Ili kuweza kufanya kazi na watu wa tabaka la Komla, ili kuweza kubadili jinsi wageni wanavyoiona katika chombo kikubwa cha habari duniani kwa kuripoti hadithi za Afrika kwa njia tofauti, ni heshima kubwa.

Serwanjja atahusika wakati wa sherehe ya uzinduzi wa tuzo hiyo ya 2020 mjini Johannesburg na ataandaa kipindi cha mjadala cha Focus on Africa katika redio ya idhaa ya BBC.

Mjadala huo utaangazia hatma ya uwezo wa Afrika na iwapo inaweza kushinikiza ukuaji wake wa kiuchumi bila kuharakisha mabadiliko ya hali ya hewa.

Mbali na uzinduzi huo, BBC News pia itatembelea vyuo vikuu vya Afrika Kusini , ikiwemo chuo kikuu cha North West kilichopo Mafikeng, Chuo kikuu cha Cape Town katika mkoa wa magharibi mwa Cape pamoja na vyuo vikuu vya Pretoria na Johannesburg huko Gauteng.

Ziara hizo zinalenga kuwatafuta waandishi chipukizi kuwapatia motisha ya kujitolea ili kushinda tuzo hii muhimu.

Maelezo ya video,

Komla Dumor's former colleagues reflect on the late broadcaster's talent

Mkurugenzi wa idhaa ya BBC , Jamie Angus, alisema: Najivunia waandishi wote ambao wamekuja BBC kupitia tuzo ya Komla Dumor, huku kila mmoja wao akiendeleza kazi ya uanahabari ya kuhadithia habari za Afrika kwa ulimwengu mzima kwa jumla.

Kila mwaka najiandaa kumtuza mshindi mpya ili kusikia habari mpya kutoka barani Afrika na kuwafunza maadili muhimu ya uaminifu na kutopendelea upande wowote ambavyo ni vigezo muhimu vya sera za BBC - ambazo ni muhimu kwa demokrasia ulimwenguni.

UPDATE LINK

  • Tazama iwapo unafuzu halafu tuma ombi, click here
  • Pia unaweza kusambaza ujumbe huu kupitia mtandao wa kijamii kwa kutumia alama ya reli#BBCKomlaAward.