Niger: 'Maisha yangu ya kutokuwa na mtoto'

Niger: 'Maisha yangu ya kutokuwa na mtoto'

Inakadiriwa kuwa karibu wenza milioni 50 duniani wana matatizo ya uzazi.Katika tamaduni nyingi wanawake hubeba lawama mara baada ya wenza kushindwa kupata watoto.

Msukumo huu katika jamii husababisha wanawake kutengwa, waume zao kuoa wake wengine na hata ndoa kuvunjika. Wanawake wasio na watoto huonekana kama mzigo.

Nchini Niger mtengeneza filamu Aicha Macky, ambaye amekuwa akitafuta mtoto, anaeleza safari yake ya kuishi bila kupata mtoto katika jamii yake.