Je Afrika inatarajia kunufaika vipi na 'kung'ang'aniwa' huko?

Rais wa China President Xi Jinping akitembea mbele ya viongozi wa Afrika

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mwaka jana kongamano la China-Afrika liliwavutia viongozi wengi kutoka Afrika

Nchi zilizo na uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani zimekuwa ziking'angania ushawishi wa kisiasa barani Afrika, lakini kufuatia kufufuliwa kwa usuhuba huu mpya na mataifa ya Kiafrika yanafanya nini kuhusu hatua hiyo?

Mwanidi wa BBC Dickens Olewe amelivalia njuga swala hilo ili kupata jibu.

Katika miaka ya hivi karibuni Waafrika wamezoea kuwaona viongozi wao wakijitahidi kuhudhuria msururu wa makongamano yaliyopewa maudhui yanayolenga bara Afrika, yanayoandaliwa duniani na ambayo yanatangazwa kama ushirikiano wa kimaendeleo utakaofaidi pande zote mbili.

Mwaka jana, Japan, Urusi na China ziliwaalika marais na wakuu wa serikali; mwezi uliopita viongozi 15 wa nchi za Afrika walihudhuria kongamano la uwekezaji wa Uingereza -Afrika mjini London, na mialiko mingine huenda imetumwa kwa ajili ya tukio lingine kama hilo linaloripotiwa kufanyika Ufaransa, Saudi Arabia na Uturuki amwaka huu wa 2020.

Lengo ni lipi?

Mchanganyiko wa utajiri wa madini katika bara hili, rasilimali ya kilimo ambayo haijatumiwa ipasavyo, ushawishi wa kura yake 54 katika Umoja wa Mataifa, ongezeko la hofu ya uvamizi kutoka kwa makundi yenye itikadi kali, uhamiaji wa kiuchumi na taharuki inayotajwa na baadhi ya watu kama ubaguzi wa rangi dhidi ya watu wake ni miongoni mwa masuala yanayotasadikiwa kuchangia kufufuliwa kwa ushirikiano huu mpya.

"Ipo haja ya ulimwengu kujadiliana na kusaidia kutatua matatizo ya Afrika, ambayo hivi karibuni au baadaye, yatageuka kuwa tatizo la kimataifa," Mwanauchumi wa Zambia Dambisa Moyo aliangazia katika ripoti yake ya mwaka 2018 iliyopewa kichwa: Tishio la Afrika.

"Hakujawahi kuwa na mashauriano ya kina ya kimataifa kuhusu bara la Afrika. Licha ya hilo uchumi wa kimataifa unaweza kunufaika pakubwa kutokana na uwekezaji utakaotokana na bara Afrika," Dkt Moyo aliandika.

Chanzo cha picha, Empics

Maelezo ya picha,

Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Marekani Donald Trump

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alikubaliana na hoja hiyo, katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Marekani akisema kuwa Afrika "Licha ya kuwa bara ambalo linachangia changamoto ya kiusalama au uhamiaji usiokuwa mpangilio ambao unaweza kudhibitiwa," Lakini inaweza kutoa nafasi nzuri ya uwekezaji duniani.

Hatahivyo, alionya kuhusu ushindani kutoka kwa China, Marekani, Urusi na mataifa mengine dhidi ya bara hilo:

"Nimeshuhudia mashauriano kati ya nchi za Magharibi na washirika wao wa Asia na Mashariki ya kati, nahisi ushindani wa kung'ang'ania Afrika, katika visa vingine… kuchukulia Afrika ni kama inaweza kumilikiwa na mtu yeyote mwenye uwezo... Lakini nataka niwaambie kwamba hilio haliwezekani," Bw. Kenyatta aliongezea.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mfanyikaziwa kiwanda nchini Ugandan akiunganisha simumjini Kampala

Lakini Afrika ina mpango gani?

Mwaka 2013, viongozi wa Afrika, chini ya Muungano wa Afrika (AU), walikubaliana kuhusu mpango utakaotoa muongozo thabiti wa kushughulikia changamoto inayokabili bara hilo.

Mpango huo ulifahamika kama ajenda ya mwaka 2063.

Ulitoa maono kadhaa, ikiwemo, kumaliza vita katika bara hilo, kuboresha miundo mbinu na kuruhusu utangamano huru wa watu.

Mradi mwingine ambao ulifahamika kama African Continental Free Trade Area (AfCTA), ambao unatajwa kuwa mkataba wa biashara huru kwa mataifa ya bara Afrika, unatarajiwa kuimarisha biashara miongoni mwa mataifa ya Afrika.

Wakosoaji, hatahivyo wanasema AfCTA, ambayo itaanza kutekelezwa mwezi Julai, sio suluhisho la changamoto zinazokabili Afrika na kuongeza itakabiliwa na kuhunzi cha sera ya kujilinda na miundombinu duni ya taifa wanachama.

Miradi ya Ajenda 2063

  • Kuunganisha miji mkuu yote ya Afrika na vituo vya kibiashara kupitia mtandao wa usafiri wa treni ya mwendo kasi
  • Kuimarisha biasha baina ya mataifa ya Afrika ili kuboresha nafasi yake katika soko la kimataifa
  • Kuboresha bwawa la Inga nchini DR Congo ili kuzalisha Megawati 43,200 ya umeme
  • Kuondoa vikwazo vya usafiri kwa waafrika, wanaotaka kufanya kazi katika matifa yaliyo nadi ya bara lao
  • Kumaliza vita, mizozo ya ndani, unyanyasaji wa kijinsia, kuzui ghasia na mizozo inayochangia mauaji ya kimbari
  • Kubuni tiketi moja ya usafiri wa angani katika eneo la Afrika (Saatm)
  • Kuimarisha mashirika ya anga ya mbali barani Afrika
  • Kubuni chuo kikuu cha Afrika cha kidijitali
  • Kubuni encyclopaedia ya Kiafrika itakayotoa maelezo ya kuaminika kuhusu historia ya baraAfrika na maisha ya Waafrika

Chanzo: Agenda 2063

Hatahivyo Muungano wa AU anajivuta kutekeleza Agenda 2063 kwasababu shirika hilo halina ushawishi wa kushurutisha mataifa wanachama kuangazia mipango iliyofikiwa, W Gyude Moore, waziri wa zamani wa nguvu kazi wa Liberia, anasema.

Ameongezea kuwa mataifa ya Afrika yamezongwa na madeni na kwamba yamekuwa yakitumia rasilimali zao kulipa mikopo, hali inayofanya kutotilia maanani mipango mikubwa ya kuimarisha bara hilo.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Miondo mbinu mibovu ya barabara imekwamisha maendeleo ya kiuchumi katika nchi za Afrika

Anapendekeza bara hilo litumie fursa inayojitokeza ya kung'ang'aniwa na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani kutafuta njia ya kuimarisha miundo mbinu hususan ya barabara inayojitokeza ili kuboresha uchumi wa mataifa yake.

Japo miradi ya Ajenda 2063 itafikiwa kupitia treni ya mwendo kasi, mfumo wa usafiri wa barabara bado unachangia karibu 80% ya uchukuzi wa bidhaa na watu, kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB).

Hali mbaya ya barabara katika nchi 49 yaliyo katika eneo la kusini mwa jangwa la sahara imewafanya watu kutengwa katika upatikanaji wa elimu ya msingi, huduma ya afya, kubuniwa kwa vituo vya kibiashara, na kukosa nafasi za kiuchumi,ADB inasema.

"Ni 43% tu ya barabara barani Afrika zinazostahili kuunganisha miji mikuu lakini 30% kati ya bara za iana hiyo zinapatikana katika nchi moja: Afrika Kusini", Bw. Moore, ambaye kwa sasa ni mwanazuoni wa wa ngazi ya juu katika kituo cha kimataifa cha sera ya maendeleo nchini Marekani, anasema.

"Ni vigumu sana kuwa na jamii ya kisasa na kufikia uchumi wa kisasa bila ya kuw na barabara," Bw. Moore anasemaMwanamume anaosha piki piki yake katika barabara iliyosombwa na maji ya mafuriko katika mji mkuu wa Liberia

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mwanamume anaosha piki piki yake katika barabara iliyosombwa na maji ya mafuriko katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia wakati wa mlipuko wa Ebola wa mwaka 2014

Alitoa mfano wa mlipuko wa mwaka 2014 wa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi, ambao ulitokea wakati wa msibu wa mvua. "Kitu kilichoanza kama janga la kiafya pia kiligeuka kuwa janga la miundo mbinu ya uchukuzi wa barabrani," alisema

"Kuchukua sampuli ya damu kutoka kwa mgonjwa na kupeleka katika maabara ilikuwa vigumu kwasababu ilichukuwa muda mrefu kwa kufikisha sampuli hiyo," aliongeza.

Bw. Moore anasema utafiti na uwekezaji katika ujenzi wa barabara amabzo zitahimili mvua kubwa utabadili pakubwa bara la Afrika.

Pia unaweza kusoma:

Changamoto nyingine inayokabili mataifa kadhaa ya Afrika ni ukosefu wa mfumo maalumu unaofanya kazi katika ofisi za serikali, Dkt Ken Opalo kutoka chuo kikuu cha Georgetown aliimbia BBC. Kitu ambacho, anasema, mataifa ya Afrika yanaweza kujifunza kutoka China.

"Kile kitu ambacho kinameiwezesha China kufaulu sio utawala wa kikomunisti, bali ni uwezo wa utawala huo kufanya kazi... uwezo wa kutekeleza sera za serikali ili kuhakikisha kila kitu kinafanywa ilivyopangwa ikiwa ni pamoja na kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Kwahivyo ni jambo la kuchekesha kutarajia mambo yabadilike katika nchi kama Sudan Kusini, Jamhuri ya Afrika ya Kati au hata Malawi," Bw. Opalo anaongeza.

Muungano wa Kiafrika umekiri kumekuwa na changamoto na kwamba unapanga kuzindua mbinu muafaka wa kufuatilia utekelezaji wa Ajenda 2063, naibu mwenyekiti wa shirika hilo Quartey Thomas Kwesi, alisema hivi karibuni.

"Pia tunakaribisha wakosoaji," aliongeza.

Suala lingine la kutia hofu ni kuwa licha ya viwango vya umasikini vinashuka duniani, vinaendelea kupanda barani Afrika, kwa mujibu waWakfu wa Bill & Melinda Gates.

Shirika hilo linakadiria Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo huenda zikawa nyumbani kwa 44% ya watu masikini zaidi duniani katika kipindi cha miaka 30 iki hali ya sasa itaendelea.

Sekta ya kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa mataifa mengi ya Afrika inatoa fursa nzuri itakayo wakomboa mamilioni ya watu kutokana na umasikini bado haijaangaziwa ilivyo. Hali ambayo imechangiwa na ukosefu wa uwekezaji. Bw. Opalo anasema

Kutokana na ukosefu wa ajira na kupoteza matumaini vijana wengi wanakimbilia maeneo ya mijini.