Hosni Mubarak: Je alikuwa nani Misri?

Hosni Mubarak

Chanzo cha picha, Getty Images

Hosni Mubarak alikuwa mwanajeshi, lakini aliyetaka taifa lake kuunga mkono amani duniani.

Chini ya uongozi wake , Misri ilichukua jukumu la kujairibu kuweka makubaliano kati ya Israel na Palestina.

Miongo yake mitatu mamlakani ilikamilika mwaka 2011, wakati maandamano yalipomuondoa afisini.

Alikabiliwa na ukosoaji mkubwa kwa kutumia tahadhari ya taifa kukabiliana na wapinzani na miaka ya mwisho ya maisha yake alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya ufisadi.

Rubani wa ndege za kivita

Muhammad Hosni Said Mubarak alizaliwa tarehe 4 mwezi Mei 1928 katika eneo la Kafr-El Meselha, kaskazini mwa Misri.

Licha ya kutoka katika familia ya umasikini, alifuzu katika chuo cha mafunzo ya kijeshi 1949. Alihamia katika jeshi la angani ambapo alianza kazi 1950.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hosni Mubarak akiwa afisa mchanaga wa jeshi la wanahewa 1952

Alihudumu kipindi cha miaka miwili akiendesha ndege za kivita na kupanda cheo cha kuwa mwalimu wa kuendesha ndege .

Alishuhudia mapinduzi ya kijeshi ya jenerali Gamal Abdel Nasser mwaka 1952 na mgogoro wa rasi ya suez uliofuatia.

Mwaka 1959, Mubarak alisafiri Urusi - ambalo ndio taifa lililokuwa likiuzia serikali mpya ya Misri silaha ambapo alijifunza kundesha ndege za kurusha makombora.

Alimuoa Suzanne - mtoto wa miaka 17 wa daktari , na kupanda ngazi na kuwa mkuu wa chuo cha mafunzi ya marubani wa jeshi kabla ya kupanda ngazi juu zaidi na kuwa mkuu wa jeshi la wanahewa 1972.

Shujaa wa taifa

Ilikuwa katika wadhfa wake wa kuwa kamanda wa jeshi la wanahewa la Misri na naibu waziri wa ulinzi ambapo alipata umaarufu.

Mubarak alikuwa miongoni mwa watu waliohusika sana na njama ya uvamizi wa ghafla dhidi ya majeshi ya Israel mwaka 1973 wakati wa vita vya Waarabu na Israel.

Uvamizi huo ulifanyika katika eneo la Yomm Kippur, ikiwa ndio siku takatifu katika kalenda ya Wayahudi.

Mubarak alikuwa shujaa wa kitaifa kwa jukumu ambalo jeshi la Misri la wanahewa lilichukua katika rasi ya Suez Canal. Urusi na Marekani zilikaribia kuzozana wakati zilipokuwa zikiwauzia silaha washirika wake .

Israel iliukabili uvamizi huo lakini ikarudisha eneo hilo kwa Misri.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Israeli soldiers wanaondoka katika ukingo wa rasi ya Suez canal nchini Misri 1973

Makamu wa rais

Mubarak alipata tuzo yake miaka miwili baadaye , wakati rais Anwar Sadat alipomfanya kuwa makamu wake wa rais.

Sadat alikuwa mtaalamu wa sera ya kigeni ya 'electrick shock'. Alifukuza washauri 16,000 wa Urusi , akatembelea mji wa jerusalem wakati akia katika vita na akakataa kukutana na viongozi wa Saudi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais Sadat alimetua Hosni Mubarak kuwa naibu wake 1975

Mubarak alianza kutatua matatizo ya nchini , lakini akaanza kujenga ushirikiano wa karibu na viongozi wengine wa Kiarbu hususan mfalme wa saudi mwanamfalme Fahd.

Hakuonekana kuunga mkono makubaliano ya amani ya Camp David ya 1979- yaliotiwa saini na rais Sadat na waziri mkuu wa Israel Menachem Begin.

Makubaliano hayo yaligawanya ulimwengu wa nchi za Kiarabu.

Mubarak alijuta kufeli kwa Sadat kuzuia kuporomoka kwa uhusiano na washirika wenye msimamo wa kadri na makundi yenye itikadi kali.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mubarak alijeruhiwa wakati wa mauaji ya rais Sadat 1981

Mwezi Oktoba 1981, wanajeshi waliowatiifu kwa kundi moja kama hilo walimuua Sadat wakati wa gwaride la kijeshi ambalo li;likuwa linaadhimisha ushindi wake katika mgogoro wa vita kati ya Waatabu na Israel 1973. Waliomuua walijificha katika gari ambalo lilisimama mbele ya rais.

Akidhania walikuwa miongoni mwa gwaride alienda kuwasalimia. Walirusha guruneti na kufyatua risasi katika umma wakiwa wamejihami na bunduki aina ya AK -47, Sadat alifariki hospitalini saa mbili baadaye. Hosni Mubarak alikuwa miongoni mwa wale waliijeruhiwa.

'Amani baridi'

Mubarak alifanikiwa kuwa rais akipata asilimia 98 ya kura katika kura ya maoni ya kitaifa ambapo alikuwa mgombea wa pekee.

Aliahidi kutekeleza makubaliano ya Camp David , lakini uhusiano wake na Israel ulikuwa mbaya zaidi ya ulivyokuwa na Sadat. Wachanganuzi waliitaja kuwa 'amani baridi'.

Misri na saudia pia -ambazo ndio nchi zemnye idadi kubwa ya watu na tajiri zaidi katika mataifa ya Kiarabu - pia waliungana kupinga uwezo wa Ayatollah Khomeini nchini Iran.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hosni Mubarak na mwenyekiti bwa PLO Yasser Arafat

Misri iliondolewa katika ligi ya mataifa ya Arabuni 1979 - ilirudishwa tena katika muungano huo kabla ya makao rasmi ya muungano huo kurudi katika ukingo wa mto Nile.

Vita vya Ghuba

Uvamizi wa Iraq nchini Kuwait 1991 ulikuwa pigo kwa Mubarak ambaye alidai kwamba alikuwa amepokea ahadi kutoka kwa Saddam Hussein kwamba hakuna njama kama hiyo.#

Huku akiunga mkono vikwazo vya kimataifa , Mubaraka aliahidi kusaidia katika kuunda muungano wa majeshi dhidi ya kiongozi huyo wa Iraq.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hosni Mubarak na rais George Bush

Saddam alitaka kupinduliwa kwa serikali ya Misri.

Maandamano ya Arab Spring

Mwezi Januari 2011, Misri ililipuka. Kulikuwa na wiki ya maandamano yaliofanywa na waandamanaji waliokasirishwa na ufukara, ufisadi, ukosefu wa ajira na uongozi wa kiimla.

Ahadi yake ya kutogombea urais haikutosha. Baada ya siku 18 ya maandamano alitangaza kwamba anajiuzulu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raia wa Misri waliandamana dhidi ya Mubarak 2011 na akalazimishwa kujiiuzulu

Miezi minne baadaye , Mubarak aliyekuwa mgonjwa alifunguliwa mashtaka akiwa katika kitanda cha hospitali ambapo alishtakiwa na mashtaka ya ufisadi na ukosefu wa ajira na utawala wa kiimla.

Kundi lake la mawakili awali lilikuwa limesema kwamba bado alikuwa rais wa Misri hivyobasi alikuwa na kinga ya kushtakiwa.

Mwezi Juni 2012, Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kushindwa kuzuia mauaji ya waandamanaji lakini akaondolewa mashtaka mengine.

Uamuzi huo ulisababisha maandamano katika barabara kuu za Cairo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hosni Mubarak aliposimamishwa kizimbani 2014

Hatahivyo baadaye Mubarak aliondolewa mashtaka ya ufisadi na kushtakiwa kwa ubadhirifu wa fedha.

Mwaka 2017, mahakama kuu ya Misri ilimuondolea mashtaka ya mauaji ya waandamanaji na akaachiliwa huru.