Vita vya Syria: Mashambulio dhidi ya Idlib yalenga shule na hospitali'

People inspecting bomb damage - shelled-out cars and rubble - in the town Maarat Misrin in Idlib province

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa zilikua ni shule na Hospitali ya jiji la Idlib na miji inayozingira jiji hilo, yamesema makundi ya kutete haki za binadamu

Takrina raia 20, mkiwemo watototisa wameawa katika mashambulio ya anga ya jeshi la Syria katika jimbo la Idlib Jumanne, Shirika la waangalizi wa mzozo la Syria limesema.

Shrika hilo ambaloi linachunguza haki za binadamu limesema kuwa shule na hoispitali zilikua miomngoni mwa maeneo yaliyolengwa.

Vikosi vya serikali ya Syria vimekuwa vikiendeleza mapambano makali kwa ajili ya kulichukua jimbo la Idlib, likiwa ni eneo muhimu nchini Syria ambalo bado liko chini ya udhibiti wa waasi na wapiganaji wa jihadi

Takriban watu milioni tatu wanaishi katika maisha ya shida katika jimbo hilo.

Rami Abdel Rahman, mkuu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria , amesema kuwa mashambulio yalilenga jiji kuu ambalo pia linaitwa -Idlib - na maeneo mengine yanayozingira jiji hilo

Mtoto mmoja wa shule na waalimu watatu pamoja na watu wengine wawili, waliuawa katika jiji la Idlib, alisema, huku takriban watoto sita wakiwa miongoni mwa raia 10 waliouawa katika mji wa Maarat Misrin, uliopo kaskazinimwa jiji la Idlib.

Aliongeza kuwa watu wengine wanne , mkiwemo mama na watoto wake wawili , walikufa katika mji wa Binnish, uliopo kaskazini -mashariki mwa jiji hilo.

Chanzo cha picha, AFP

Muungano wa huduma za tiba-The Union of Medical Care na mashirika ya misaada (UOSSM) yamesema kuwa jumla ya shule 10- zikiwemo mbili za chekexhea- pamoja na hospitali kuu yaIdlib vimepigwa na mashambulio ya anga na ardhini.

Muungano huo umeyataja mahambulio hayo kama "ukatili".

Mkurugenzi wa Amnesty International wa kanda ya Mashariki ya kati na Afrika Kaskazini Heba Morayef, amelaani mashambulio hayo akisema : "Shule zinapaswa kuwa mahala salama kwa watoto kusoma na kucheza, hata katika maeneo ya mizozo.

" Kushambulia shule na vituo vya chekechea vinavyotumiwa na raia ni uhalifu wa kivita ."

Unaweza pia kusoma:

Mzozo wa hivi karibuni katika jimbo la Idlib umeelezewa kama mbaya kuwahi kushuhudiwa tangu kuanza kwa mzozo wa Syria mwaka 2011.

Awali Umoja wa mataifa ulionya kwamba kiwango cha mapambano kwa ajili ya udhibiti wa Idlib kinaweza kufikia " umwagaji damu mkubwa ". Juma lililopita, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja.

Ni kwanini kuna mzozo wa Ilib?

Idlib ni ngome ya mwisho ya waaasi na wapiganaji wa Jihad ambao wamekua wakijaribu kumpindua rais wa Syria Bashar al-Assad tangu mwaka 2011.

Wakati mmoja upinzani ulidhibiti maeneo makubwa ya nchi, lakini jeshi la Syria limeyachukua tena mengi ya maeneo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa usaidini wa nguvu za mashambulio ya anga ya Urusi na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran. Sasa jeshi linataka ''kuikomboa'' Idlib .

Katika miaka ya hivi karibuni idadi ya watu waliosambaratishwa na mapigano imeongezeka mara dufu ya idadi ya watu wapatao milioni tatu, mkiwemo watoto milioni moja.

Uturuki, ambayo unaunga mkono wapinzani wa Assa na yenye hofu ya kuongezeka kwa wakimbizi wengi wanaokimbilia nchini humo kutoka Syria, imewapeleka wanajeshi wake katika vituo vya uangalizi katika maeneo ya mpaka katika jimbo la Idlib chini ya makubaliano na Urusi ambayo iliweka eneo lisilo la mapigano - katika mkataba Sochi 2018.

Hata hivyo, imeshindwa kuzuwia jeshi la Syria kuchukua tena maeneo makubwaya jimbo hilo kwa usaidizi wa mashambulio ya anga ya Urusi na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.