Coronavirus: Algeria yathibitisha kupata maambukizi

A Kenyan health worker (L) screens a passenger wearing face mask after they arrived from China, at Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi, Kenya, 29 January 2020

Chanzo cha picha, EPA

Waziri wa Afya nchini Algeria amethibitisha kwamba nchi hiyo imepokea kisa cha kwanza cha coronavirus katika taarifa iliyotolewa na runinga inayomilikuwa na serikali, ENTV Jumanne jioni.

Waziri Abdel Rahman Ben Bouzid alisema kuwa mgonjwa huyo ni mwanamume raia wa Italia aliyewasili nchini humo Februari 17, kulingana na shirika la habari la Reuters.

Mgonjwa huyo ametengwa kwa sasa.

Algeria imekuwa nchi ya pili Afrika kuthibitisha kupata mgonjwa wa virusi vya Corona.

Misri ilikuwa ya kwanza kuthibitisha kupatika kwa kisa cha virusi vya Corona lakini baadae ikatangaza kwamba mgonjwa huyo hana tena maambukizi na anaendelea kupata nafuu.

Naibu Waziri wa Afya Iran athibitishwa kupata virusi vya Corona

Nchi hiyo ni moja ya zile ambazi zimezua wasiwasi mkubwa kwamba virusi vya Corona huenda vikawa janga.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Iran imeripoti visa 95 vya virusi vya Corona lakini idadi kamili inadhaniwa kuwa juu zaidi.

Naibu waziri, Iraj Harirchi, Jumatatu alikanusha madai ya kwamba nchi hiyo inajaribu kuficha ukweli kuhusu mlipuko wa virusi hivyo.

Iran imeripoti visa 95 vya virusi vya Corona lakini idadi kamili inadhaniwa kuwa juu zaidi.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Dunia (WHO) amesema kwamba kuongezeka ghafla kwa visa hivyo kwa nchi ambazo ziko nje ya China ni jambo la kutia wasiwasi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo, amesema Jumanne kwamba Washington ilikuwa na hofu kuwa Iran huenda imeficha taarifa muhimu kuhusiana na mlipuko wa ugonjwa huo na kusihi nchi zote kusema ukweli kuhusu virusi vya Corona.

Chanzo cha picha, KHAMIS BAKARI

Maelezo ya picha,

Raia wa Kigeni waliopo Uchina wakiwemo kutoka Afrika wamekua wakielezea hofu yao juu ya virusi vya Corona, mmojawao akiwa ni Mtanzania Dkt Khamis Hassan Bakari ambaye yupo jijini Wuhan ambao ni kitovu cha virusi hivyo.

.Wakati huo huo, naibu waziri wa afya na mbunge mmoja nchini Iran wamethibitishwa kupata virusi vipya vya Corona, wakati inapambana kukabiliana na virusi hivyo ambavyo vimesababisha vifo vya watu 15.

Watu wengi zaidi wamefariki nnchini Iran kwasababu ya virusi hivyo kuliko nchi nyengine yoyote mbali na China.

Nchi hizo mbili zina uhusiano mkubwa wa kibiashara.

Nchi zingine ambazo kwa sasa zimekumbwa na mlipuko wa virusi vya Corona kwa kiwango kikubwa ni Korea Kusini na Italia ambapo visa hivyo vimekuwa vikiongezeka katika siku za hivi karibuni.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Katika harusi ya pamoja nchini Ufilipino wanadoa walazimika kuvaa barakoa