Mkataba wa amani Afghanistan: “Huenda wanawake wasiruhusiwe tena kufanya kazi”

Mkataba wa amani Afghanistan: “Huenda wanawake wasiruhusiwe tena kufanya kazi”

Mazungumzo ya Amani kati ya Marekani na Taliban yanakaribia, Tahera Rezai daktari wa mifugo mwenye umri wa miaka 30, anahofia hatma ya maisha yake.

Taliban walipiga marufuku wanawake kufanyakazi na kusoma wakati walipokuwa madarakani 1996-2001.

Sasa wanajeshi wa Marekani huenda wakaondoka Afghanistan baada ya kufikiwa kwa makubaliano lakini Tahera ana wasiwasi kuhusu siku za usoni kwamba huenda wanawake wa Afghanistan wakarejeshwa katika siku za nyuma.