Suleiman Yusuf Koore: Bawabu aliyefanikiwa kuwa waziri katika ofisi aliyolinda Somalia

Suleiman Yusufu Koore

Chanzo cha picha, SULAYMAN YUSUF KOORE

Maelezo ya picha,

Waziri wa habari na mawasiliano nchini Somaliland Suleiman Yusufu Koore

Katika mfumo wa kisiasa nchini Somalia , ni vigumu kwa mtu wa tabaka la chini kupata mafanikio makubwa na kupanda ngazi kisiasa.

Lakini sio vigumu kwa mtu kufanikisha malengo yake

Ama kwa kweli katika taifa hilo lililokumbwa na msukosuko wa vita vya wenyewe kwa wenyewe haikuwa rahisi kwa bawabu kupanda ngazi hadi kuwa waziri wa serikali , lakini Suleiman Yusuf Koore alipitia njia hiyo na kufanikiwa.

Cha kushangaza ni kwamba Jinsi alivyopanda ngazi na kufikia alipo hivi sasa ni tofauti na jinsi wanasiasa wengi hupata mafanikio.

Mwaka 1984 akiwa na umri mdogo wa miaka 18 , waziri Suleiman alishiriki katika mpango wa huduma za serikali , ambapo wanafunzi walipitia kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuanza kazi.

''Nilisajiliwa kwa huduma ya kitaifa baada ya shule ya upili ambapo katika kipindi cha miezi saba nilikuwa bawabu katika kituo cha habari cha Hargeisa ambapo hivi sasa nimekuwa waziri , aliambia BBC Somali.

''Hatahivyo mazingira ya kuishi wakati huo yalikuwa magumu , hususan katika sekta ya chakula, na nilikuwa nikipewa 'sandwich'moja kila asubuhi kama kiamsha kinywa , lakini nilishukuru kutokana na hali ilivyokuwa wakati huo''.

Chanzo cha picha, SULAYMAN YUSUF KOORE

Maelezo ya picha,

Suleiman Yussuf Koore

Pia anasema kwamba alilazimika kuhamishwa na kurudishwa katika kituo hicho cha redio miezi mitatu baadaye smbapo anasema usiku ulikuwa mrefu sana kwake.

''Nilikuwa mlinzi usiku na asubuhi nilikuwa nikifanya kazi kama vile mwalimu ama kazi nyingine yoyote niliopewa'', aliendelea

Waziri Suleiman pia aliambia BBC kwamba familia yake ilikuwa ikiishi nchini humo na kwamba alipoajiriwa , alilipwa dola 12 za Marekani kwa mwezi , ambazo alisema kwamba hazikutosha kununua nguo, kulipa kodi na kununua vitu vingine.

Tofauti ni kwamba , mawaziri Somaliland sasa wanapokea $ 2000 kila mwezi na hadi marupurupu ya $705.

Alisema kwamba huduma hiyo ya kitaifa ilikuwa ya kila mmoja aliyemaliza shule ya upili na akaongezea: Sikuweza kuingia katika ofisi ambayo kwa sasa ninaisimamia wakati huo , kwa kuwa nilikuwa mlinzi.

Suleiman anasema kwamba amefanya kazi nyingi nchini Somaliland 1991 na kushikilia baadhi ya wizara , lakini uteuzi wake katika wizara ya habari ulikuwa muhimu kwa kuwa ndio ofisi yenye mlango aliokuwa akiulinda.

Bwana Koore anasema kwamba amekuwa katika siasa kwa takriban miaka 25 na ameshikilia nyadhfa kadhaa za waziri- lakini mwezi Disemba alianza kazi katika wizara ya habari na mawasiliano, ambayo anaichukulia kama nyumbani kwake.

Chanzo cha picha, SULAYMAN YUSUF KOORE

Maelezo ya picha,

Aliyewkuwa wakati mmoja bawabu apanda ngazi hadi kuwa waziri katika afisi aliokuwa akiilinda

Anasema kwamba ana kumbukumbu maalum kuhusu ofisi hiyo na kwamba alipotoa habari hiyo kwa umma wengi walimkosoa na kusema kwamba lilikuwa jambo la aibu kulitaja .

Na sasa kama waziri wa habari na mawasiliano , bwana Koone ndio afisa wa ngazi ya juu zaidi katika afisi hiyo.

"Inaingia maanani kwangu mimi kwamba nimekuwa waziri katika wizara niliyofanya kazi wakati wa ujana wangu kwani ina maana kubwa maishani mwangu," aliiambia BBC.

Aliongezea: Ni muhimu kwamba watu hawasalimu amri kwa haraka na kwamba wanang'ang'ana hadi mwisho