Coronavirus: Wafungwa zaidi ya 54,000 waachiwa huru Iran kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona

Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Iran umewaua karibu watu 77 pkatika kipindi cha wiki mbili

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 nchini Iran umewaua karibu watu 77 pkatika kipindi cha wiki mbili

Iran imewaachia huru kwa muda wafungwa zaidi ya 54,000 ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa corona katika magereza yaliyo na msongamano wa watu.

Msemaji wa mahakama Gholamhossein Esmaili amewaambia waandishi wa habari kuwa wafungwa waliruhusiwa kutoka gerezani baada ya kupimwa na kukutwa hawana ugonjwa wa Covid-19(virusi vya corona).

Wafungwa wa usalama waliofungwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitano hawataachiwa.

Mfanyakazi wa wahitaji nchini Iran ambaye ni raia wa Uingereza, Nazanin Zaghari-Ratcliffe anaweza kutolewa hivi karibuni kwa mujibu wa mbunge wa Uingereza .

Balozi wa Uingereza nchini Iran,Tulip Siddiq alisema kuwa bi Zaghari-Ratcliffe ataachiwa huru leo au kesho.

Mume wake alisema siku ya jumamosi kuwa aliamini mke wake alipata maambukizi ya Covid-19 akiwa gereza la Evin laTehran na mamlaka yalikuwa yanakataa kumpima.

Lakini bwana Esmaili alisisitiza siku ya jumatatu kuwa Zaghari-Ratcliffe alikuwa akiwasiliana na familia yake na kuwaambia kuwa afya yake iko salama.

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Nazanin Zaghari-Ratcliffe ameshikiliwa katika gereza la Evin Tehran's Evin

Bi.Zaghari-Ratcliffe alifungwa kwa kipindi cha miaka mitano mwaka 2016 baada ya kukamatwa alikanusha kuhusika na madai yanayomkabili.Huku Uingereza ikisisitiza kuwa bi Zaghari hana hatia.

Msemaji wa ofisi ya mambo ya nje alisema kuwa serikali ya Iran itawaruhusu haraka wataalamu wa afya kuingia katika gereza la Evin kuangalia hali za raia wenye uraia wa Uingereza na Iran zikoje.

Mpaka sasa zaidi ya kesi 90,000 za ugonjwa wa Covid-19 duniani kote zimeripotiwa na vifo3,110 tangu ugonjwa huu uanze mwishoni mwa mwaka jana, huku wengi waliokufa ni wachina .

Mlipuko wa virusi vya corona umeuwa watu wapatao 77 nchini Iran kwa muda usiozidi wiki mbili.

Siku ya Jumanne, wizara ya afya imesema kuwa idadi ya visa vya corona vilivyothibitishwa ni zaidi ya asilimia hamsini.

Kwa sasa ni watu 2,336, ingawa inaaminika kuwa takwimu i kubwa zaidi ya inayotajwa.

Kesi zinazohusisha Iran zimeripotiwa Afghanistan, Canada, Lebanon, Pakistan, Kuwait, Bahrain, Iraq, Oman, Qatar na Nchi za falme za kiarabu.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kuna visa vipya 835 vya ugonjwa mpya wa Covid-19 siku ya Jumanne

Maafisa wa juu wa Iran pia wamepata maambukizi ya virusi hivyo vya corona. Miongoni mwao ni wahudumu wa afya katika kitengo cha dharura, Pirhossein Kolivand.

Kati ya wabunge 290, wabunge 23 wana maambukizi ya virusi vya corona tayari.

Siku ya Jumatatu, kiongozi mmoja wa nchi hiyo aliyefariki kutokana na Covid-19 huko Tehran, chombo cha habari cha taifa kilisema kuwa Mohammad Mirmohammadi, mwenye miaka 71, alikuwa ana uhusiano wa karibu na Ayatollah Khamenei.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ayatollah Ali Khamenei ni kiongozi wa Iran akitoa angalizo la virusi vya corona

Katika maadhimisho ya upandaji wa miti ambayo iliadhimishwa siku ya Jumanne duniani kote, Kiongozi huyo aliyefariki aliwataka umma kuzingatia usafi na kufuata muongozo ambao wizara ya afya umetoa na maagizo ambayo serikali imetoa.

Ayatollah Khamenei alisisitiza kuwa mamlaka ya Iran haifichi taarifa ya ukubwa wa tatizo;"Maafisa wetu wamekuwa wairipoti kwa uwazi na ukweli taarifa zote za ugonjwa tangu siku ya kwanza.

Ingawa kuna baadhi ya mataifa ambayo wanajaribu kuficha tatizo la mlipuko huu."

Aliongeza kuwa mlipuko wa corona Iran hautakaa sana.

Kwa sasa wazriri wa afya Saeed Namaki alisema kuwa wanaanzisha kampeni ya upimaji wa virusi hivyo ambayo itaanza siku ya Jumatano.

Wahudumu wa afya watawatembelea wagonjwa ambao wanadhaniwa kuwa na maambukizi ya Covid-19 na hawana huduma ya afya.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Timu ya shirika la afya duniani iliwasili Tehran siku ya jumatatu

Kundi ya wataalamu wa afya kutoka shirika la afya duniani(WHO) iliwasili Iran siku ya Jumatatu ili kuisaidia mamlaka ya Iran.

WHO imesema kuwa ikiwa na wahudumu wa afya zaidi ya 15,000 na vifaa vya maabara zaidi ya 100,000.