Utafiti: Uchafuzi wa hewa ni hatari kuliko uvutaji sigara?

Utafiti mpya unakadiriwa kuwa uchafuzi wa hali ya hewa inapunguza miaka mtatu ya umri wa kuishi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Utafiti mpya unakadiriwa kuwa uchafuzi wa hali ya hewa inapunguza miaka mtatu ya umri wa kuishi

Ugonjwa wa mapafu, saratani, matatizo ya moyo na kiharusi vimehusishwa na uchafuzi wa hewa - kiasi kwamba imeitwa "uvutaji mpya wa sigara".

Lakini hali hii inayafupisha vipi maisha yetu?

Jopo la wanasayansi inaonyesha kwamba uchafuzi wa hewa ya nje unatushushia urefu wa kuishi kwa takriban miaka mitatu (2.9) kwa wastani - mara mbili zaidi ya makadirio ya hapo awali na zaidi ya sigara za tumbaku.

Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la Utafiti wa masuala ya moyo na mishipa, wanadai kwamba hii ni karibu mara 10 kuliko vifo ambavyo husababishwa na aina zote za vurugu kwa ujumla ikiwemo vita.

Na watafiti waligundua kuwa idadi ya vifo kutokana na uchafuzi wa hewa inaweza kuzidi ile inayosababishwa na sigara.

Walitumia mfano wa hivi karibuni wa takwimu kuhesabu vifo mnamo 2015, na waligundua kuwa uchafuzi wa hewa ulihusishwa na vifo vya watu milioni 8.8.

Matumizi ya tumbaku husababisha vifo vya zaidi ya milioni 8.2 ulimwenguni kila mwaka, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni.

Zaidi ya milioni 7 ya vifo hivyo ni matokeo ya matumizi ya moja kwa moja ya sigara.

'Ugonjwa'

Tunaamini matokeo yetu yanaonesha kuna " ugonjwa wa uchafuzi wa hali ya hewa ",Thomas Münzel, profesa katika Kituo cha tiba cha Chuo Kikuu cha Mainz na mwandishi mwenza wa utafiti huo, walisema katika taarifa.

"Watengenezaji wa sera na jamii ya kitabibu wanapaswa kulipa hili kipaumbele zaidi."

"Kwa miongo kadhaa iliyopita umakini mdogo umekuwepo kwa uchafuzi wa hewa kuliko sigara," Münzel ameongeza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanamke akivuta sigara

Münzel na wenzake wanasema kwamba matarajio ya maisha yanaweza kuboreshwa sana na kupungua uchafuzi wa hewa - wanakadiria kuwa ingekua angalau mwaka ikiwa uzalishaji ungekatwa hadi sifuri.

Upotezaji wa kikanda na kitaifa

Timu ya wataalam pia imekadiria athari za muda mrefu za uchafuzi wa hewa kwa umri wa kuishi katika ngazi za kikanda na kitaifa.

Katika Asia ya Mashariki, maisha hupunguzwa kwa wastani na karibu miaka minne, wakati athari ya chini iko katika Oceania (miaka 0.8).

Athari pia hutofautiana sana kati ya nchi na nchi.

Huko Chad, zaidi ya miaka saba ya maisha hupotea kwa uchafuzi wa hewa, wakati huko Colombia ni zaidi ya miezi minne (miaka 0.37).

Uchafuzi unaosababishwa na binaadamu

Utafiti ulichambua uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na binadamu na asili - hivi ni vyanzo vya uchafuzi ambao hauwezi kuepukwa, kama vile vumbi la jangwa na kuzuka kwa moto wa porini.

Ilihitimisha kuwa karibu theluthi mbili ya vifo vya mapema ulimwenguni vinavyosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa vinaweza kuhusishwa na hatua za wanadamu.

"Hii inakwenda hadi 80% katika nchi zenye kipato cha juu," makadirio ya Thomas Münzel.

"Vifo milioni tano na nusu ulimwenguni kwa mwaka vinaweza kuepukika."

Watafiti pia walichambua mahusiano ya uchafuzi wa hewa na aina sita za magonjwa, kuanzia shinikizo la damu hadi saratani ya mapafu.

Waligundua kuwa ugonjwa wa moyo ndio uliochangia kufupisha maisha, ikifuatiwa na magonjwa yatokanayo na mfumo wa upumuaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mzee akitumia dawa ya kivutia hewa

''Tukitazama kwa namna gani uchafuzi wa hali ya hewa imechangia katika magonjwa kadhaa, madhara yake kwa magonjwa ya mapafu kwa kiasi kikubwa yanakaribiana kuwa sawa na madhara ya uvutaji sigara, anaeleza mwandishi mwenza mwingine, Josa Lelieveld.

Wazee huathirika zaidi

Watafiti waligundua kuwa uchafuzi wa mazingira una uwezekano wa kuathiri wazee: walikadiria kuwa 75% ya vifo vya ulimwenguni kwa sababu ya uchafuzi wa hewa hutokea kwa watu wenye zaidi ya miaka 60.

Akizungumzia matokeo ya utafiti huo, Samuel Cai, mtaalam wa tiba ya magonjwa katika Chuo Kikuu cha Oxford ambaye hakuhusika na utafiti huo, alisema kuwa "inaonesha kuwa uchafuzi wa hewa ni chanzo kinachoongoza katika kuleta athari za kiafya duniani".

"Sio siri kwamba uchafuzi wa hewa ndio 'tumbaku mpya', kwa hivyo athari ya afya ya Umma iko wazi," Cai aliongezea.

"Mamlaka zinahitaji kuchukua hatua haraka na kikamilifu ili kulinda raia wao kupitia sera za kisayansi."