Coronavirus : Hofu yawafanya kununua maburungutu mengi ya karatasi za chooni

Karatasi zikielekea kuisha

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Karatasi zikielekea kuisha

Labda hali mbaya ya siku ya mwisho ni hii: Kukwama kwenye choo na kubaini kuwa karatasi za chooni ndio zimekwisha.

Hali hiyo inaonekana kuwa ya kutisha na kuwashangaza Waaustralia wengi hivi sasa, ambao wamekuwa kundi la mwisho kuchukua hatua kutokana na hofu ya virusi vya corona kwa kununua karatasi nyingi za chooni.

Hii ni licha ya mamlaka kusisitiza hakuna uhaba wa karatasi hizo - kutokana na karatasi nyingi za choonikutengenezwa nchini humo.

Hata hivyo huko Sydney, jiji kubwa zaidi ,rafu za maduka makubwa zilizokuwa na karatasi hizo zimekuwa tupu kwa dakika chache, na kulazimisha ununuzi kwa idadi ya mwisho ya karatasi nne tu zilizofungwa pamoja.

Polisi waliitwa kwenye mzozo Jumatano, na ripoti zikisema kisu kilitolewa kwenye mzozo kuhusu karatasi za chooni, mzozo uliosababishwa na wateja wa bidhaa hiyo.

Kwenye mitandao ya kijamii kampeni ya hashtag ya #toiletpapergate na #toiletpapercrisis zilitamba mitandaoni Jumatano. Karatasi hizo zilikuwa zikiuzwa kwa mamia ya dola mtandaoni, huku wasikilizaji wakipiga simu kwenye vituo vya redio ili kushinda vifurushi vya karatasi za chooni.

Chanzo cha picha, KATHERINE QUIRKE/TWITTER

Maelezo ya picha,

Raia wa Australia wamekuwa wakiigombe bidhaa ya karatasi za chooni madukani wiki hii

Hali katika saa 48 zilizopita imeonesha kuwa kulikuwa na ripoti ya watu kuiba karatasi za chooni kwenye vyoo vya Umma.

Nini kinaendelea na kwa nini watu wanafanya hivi?

Tatizo la karatasi za chooni si jambo la kushangaza- hali kama hiyo pia imejitokeza kwenye maeneo mengine yaliyoathiriwa na virusi vya corona kama vile Singapore, Japan na Hong Kong.

Mwezi uliopita, wanyang'anyi waliiba maburungutu ya karatasi za chooni huko Hong Kong kutokana na hali ya upungufu wa karatasi hizo. Pia kuna ripoti kuhusu manunuzi ya juu ya karatasi hizo.

Nchini Australia, hali hii ilianza mwishoni mwa juma baada ya kuwepo kwa kesi ya maambukizi ya Covid-19 na kuripotiwa kwa kifo cha mtu mmoja.

Ripoti ya mwishoni mwa juma lililopita lilisababisha hali ya tahadhari kubwa

Mpaka siku ya Jumatano, Australia imerekodi visa 41 vya maambukizi na kifo cha mtu mmoja. Hii ni idadi ndogo ukilinganisha na mataifa mengine.

Muongozo nchini humo unawataka watu kuzingatia usafi na kunawa mikono.

Picha za mitandaoni zimeonesha wateja wakisukuma toroli zilizojaa maburungutu ya karatasi za chooni

Kutokana na ripoti hizi, mamlaka zimetaka Umma kuacha kugombea bidhaa hiyo, na kuwa kununua karatasi hizo na kuacha rafu zikiwa tupu madukani si suala la maana kufanya wakati huu.

Maduka makubwa kama Coles na Woolworths zimeanza kuagiza bidhaa hiyo kwa wingi, huku wazalishaji Kleenex toilet paper nchini humo wanafanya kazi ya utengenezaji wa karatasi za chooni kwa saa 24 ili kukidhi mahitaji.

Serikali imesema imejiandaa vyema, na kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi kuenea.

Hata hivyo bado hali ya kugombea bidhaa hiyo inaendelea nchini humo.

F