Coronavirus: Je, ni nani anayefaidika kifedha na mlipuko wa virusi vya corona?

kampuni za Netflix, ununuzi wa bidhaa mitandaoni, uuzaji wa chakula ni miongoni mwa kampuni zinazolengwa sana na wawekezaji

Chanzo cha picha, Getty Images

Sio kampuni zote zimepata hasara kufuatia kusambaa kwa ugonja wa virusi vya corona kote duniani pamoja na kushuka kwa hisa katika masoko mengi duniani siku za hivi karibuni.

Kuna kampuni ambazo kutokana na hali ya biashara zao - zimeongeza mapato kwa muda mfupi.

Na makadirio ni kwamba iwapo visa hivyo vya virusi vitaendelea kuongezeka, kampuni hizo zinaweza kuimarisha mauzo yao pamoja na thamani ya hisa zao katika masoko ya hisa.

Miongoni mwao, ni kampuni zinazotengeneza chanjo. sabuni za kuuwa viini na barakoi.

Na ndani ya makundi hayo biashara za kampuni za dawa na zile za biotech ambazo zinafanya majaribio kutengeneza chanjo dhidi ya virusi hivyo zimeongezeka maradufu.

Biashara ya kampuni za dawa kama vile Inovio iliongezeka baada ya kutangaza kwamba itaanza majaribio ya chanjo yake miongoni mwa binadamu mwezi ujao nchini Marekani. Thamani yake imeongezeka maradufu.

Washindani wengine ni kampuni za Moderna, Novavax, Gilead, AIM ImmunoTech na Vir Biotechnology.

Lakini kuna kampuni nyingine ambazo zimefaidika kutokana na mlipuko wa virusi hivyo japo sio moja kwa moja, kama zile ambazo zimehusika katika kutoa kumbi za mikutano, elimu ya mitandaoni na burudani, tangu baadhi ya mataifa kama vile Japan na Itali kufunga shule huku baadhi ya kampuni kama vile Google na Twitter, zikitoa wito kwa wafanyakazi wao kufanya kazi kutoka nyumbani.

Katika maeneo mengine tofauti duniani, watu wameamua kutotembelea maeneo yenye watu wengi kwa kuwa visa vya maambukizi vimefikia 90,000 duniani huku vifo vikifikia 3,000.

Hata kampuni zinazofaidika na mzozo huo wa kiafya zinakabiliwa na changamoto huku ugonjwa huo ukiendelea kuathiri binadamu.

Benki ya Marekani haikusazwa katika changamoto hizo huku ikilazimika kupunguza hadi nusu viwango vya riba siku ya Jumanne.

Kufutia mzozo huo wa Kiafya zifuatazo ni baadhi ya kampuni ambazo zimefaidika pakubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano ya video mtandaoni , afya na huduma za elimu zimefaidika

Inovio: Thamani yake ya biashara imepanda maradufu tangu mlipuko huo kuanza. Chanjo yake ya aina ya INO-4800 , ilitengenezwa kwa kutumia jeni za virusi badala ya mbinu za kawaida ambazo hufanya kazi kulingana na majaribio na virusi ambavyo havifanyi kazi.

Modern: Hisa zake zilipanda kwa asilimia 42 wakati kampuni hiyo ilipotangaza kwamba imetuma chanjo ya majaribio dhidi ya virusi vya corona katika taasisi ya kitaifa kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi nchini Marekani ili kufanyiwa majaribio katika wanadamu.

Novavax: Wakati alipotangaza kuhusu hatua zilizopigwa katika utafiti wake wa chanjo wiki chache zilizopita hisa za kampuni hiyo zilipanda kwa asilimia 20.

Regeneron Pharmaceuticals: Ikiwa kampuni iliojitolea kutafuta tiba ya ugonjwa wa virusi vya corona , ni mojawapo ya kampuni za Wall Street S&P 500 Index ambazo bei za hisa zake zilipanda kwa asilimia 10 wiki iliopita.

Top Glove: Kampuni kubwa inayotengeneza glavu duniani.

K12: Ni wataalam katika elimu ya mitandaoni kwa watoto. Wiki iliopita thamani ya hisa zake zilipanda kwa asilimia 19.

Zoom Video: Inatoa huduma za mikutano ya video miongoni mwa makampuni.

Teladoc: Huduma yake kuu ni kuwakutanisha wagonjwa na madaktari kupitia mtandaoni. Hisa zake zilipanda kwa asilimia 10 wiki iliopita na asilimia 50 mwaka huu.

Netflix: Ijapokuwa hisa za kampuni hiyo zimepanda kiasi katika siku za hivi karibuni, mwaka huu zimepanda kwa asilimia 15.

Amazon: Ijapokuwa hisa zake zilishuka thamani katika siku za hivi karibuni, kushuka kwake ni kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na soko lote kwa jumla.

Youtube: Haijakuwa na biashara nzuri kufutia mlipuko wa virusi vya corona, lakini kampuni ya Alphabet inaendelea vyema.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Wawekezaji wanacheza kamare katika kampuni ambazo zinatenegenza chanjo na huduma kwa wale wasiotoka kuondoka katika makaazi yao

Kwa wale wanaotaka kusalia majumbani kampuni kama vile Facebook, kampuni ya utengenezaji wa michezo ya video Activision Blizzard, Peloton kampuni ya kutengeza vifaa vya mazoezi na kampuni ya kuuza chakula pamoja na Netflix na Amazon .

Katika ripoti , kampuni hiyo ya uwekezaji inasema kwamba inafuatilia bidhaa ama kampuni ambazo zinaweza kufaidika iwapo wanadamu watatengwa.

USB Global Wealth Management analysts walisema kwamba kampuni zilizojitolea kuuza chakula zinaweza kupata ongezeko la wateja huku wakati ambapo watu watakuwa hawataki kutoka kwenda mbali

Mauzo ya sabuni za kuosha mikono yameongezeka

Mahitaji ya sabuni za kuosha mikono yameongezeka katika maeneo tofauti duniani.

Kulingana na data zilizochapishwa siku ya Jumanne na kampuni ya utafiti wa masoko Kantar, mauzo ya sabuni za kuosha mikono nchini Uingereza yalisajili ongezeko la kibiashara la asilimia 255 mnamo mwezi Februari ikilinganishwa na mwezi kama huo mwaka jana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nchini Marekani mauzo ya sabuni za kuosha mikono yaliongezek kwa asilimia 70.

Hata baadhi ya kampuni za kuuza dawa katika taifa hilo zimeidhinisha mauzo ya sabuni mbili za kuosha mikono kwa kila ununuzi.

Na nchini Marekani , mahitaji ya bidhaa hizo yalipanda hadi asilimia 70 mwezi Februari , kulingana na ripoti iliochapishwa na Nielsen.

Wateja wa bara Asia pia wamekuwa wakiweka bidhaa za usafi wa kibinafsi kufuatia mlipuko huo na nchini Itali ambapo kuna zaidi ya visa 2,000 uuzaji wa sabuni hizo umeongezeka maradufu.

Biashara ya kampuni ya 3M ambayo hutengeneza barakoi miongoni mwa bidhaa nyinginezo imekuwa na tabia tofauti , licha ya kwamba serikali ya Marekani imetangaza kandarasi mpya na kampuni hiyo.