Kenya yashuka kwa idadi ya mamilionea huku Tanzania ikipanda.

Afrika Kusini iliongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya matajiri binafsi
Maelezo ya picha,

Afrika Kusini iliongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya matajiri binafsi

Inakadiriwa kuwa Mamilionea 499 kwa kiwango cha dola wamepungua nchini Kenya kutoka mwaka jana.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 shirika linalofuatilia kiwango cha utajiri binafsi wa watu (HNWI) , Wakenya sita pia walishuka kutoka kwenye kikundi cha watu matajiri sana wanaofahamika kama Ultra High Net- Super (YHBW1) wakiwa na zaidi ya shilingi bilioni 3, na hivyo kupunguza idadi yao na kufikia 42.

Ripoti hiyo imeeeleza kuwa jinsi uchumi wa Kenya ulivyo waumiza watu binafsi matajiri ambao kila mmoja wao alikua na zaidi ya shilingi milioni 100.

Mabadiliko haya yametokea katika mwaka ambao Kenya imepitia kipindi kigumu cha uchumi, ambacho kilisababisha kushuka kwa faida katika kampuni na hivyo watu maelfu ya watu walipoteza ajira.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2017 ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha kushuka kwa idadi ya mamilionea binafsi nchini Kenya

Mwaka jana wakenya 2,900 waliorothseshwa na HNWI kama watu binafsi wenye kipato cha juu zaidi mwaka jana ambacho kilipungua kwa asilimia 14.6 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Zaidi ya miaka mitatu, Kenya ilikabiliwa na sintofahamu ya kisiasa kufuatia uchaguzi wa mwaka 2017, jambo ambalo liliwafanya wawekezaji kuwekeza nchini humo.

Hali mbaya ya hewa pia ambayo iliathiri kilimo- ambacho huchangia ukuaji wa pato la ndani la taifa.

Kushuka kwa idadi ya mamilionea yalikua ni matokeo ya kudorora kwa uchumi, kwa mujibu wa Bw Andrew, mmoja wa watafiti wa ripoti ya utajiri binafsi.

Afrika Kusini iliongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya matajiri binafsi ikiwa na idadi ya watu wenye utajiri wa kupindukia 1,033, ikifuatiwa na Misri ( 764), Nigeria (724) Morocco na Tanzania (114).

Maelezo ya picha,

Ripoti za awali ziliitaja familia ya rais Uhuru Kenyatta kuwa ni miongoni mwa watu wenye utajiri mkubwa sana

Ripoti ya Knight Frank haiwataji watu binafsi, lakini ripoti nyingine za awali ziliwataja matajiri nchini Kenya miongoni mwaowakiwa ni Familia ya rais Uhuru Kenyatta, rais wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi na familia ya waziri wa zamani hayati Nicholas Biwott miongoni mwa matajiri zaidi nchini Kenya.

Wafanyabiashara matajiri waliotajwa awali ni pamoja na Vimal Shah, Chris Kirubi na Manu Chandaria.

Uchunguzi wa kiwango cha utajiri binafsi hujumuisha mali alizonazo mtu, pesa tasilimu, marupurupu ya kibiashara na makazi yake.

Bwana Shirley anasema wakati wa uchunguzi wao waligundua kuwa kuna ongezeko la kizazi walichokiita Z, cha watu waliozaliwa baada ya 1995, ambao ni miongoni mwa watu tajiri zaidi na ambao huwafikia kutafuta uhauri wa utajiri nchini Kenya.

Idadi ya watu wenye utajiri wa shilingi milioni 100 imeongezeka kwa zaidi ya mara nne kuanzia 800 mwaka 2014 hadi watu 2900 mwaka jana, kwa mujibu wa ripoti ya Knight Frank.