Ronaldinho akamatwa nchini Paraguay kwa tuhuma za paspoti bandia

Ronaldinho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Ronaldinho alistaafu baada ya kucheza michezo saba katika timu Fluminese ya Brazil mnamo mwaka 2015

Mchezaji soka wa zamani wa safu ya mashambulizi ya Brazil Ronaldinh anashikiliwa na polisi wa nchini Paraguay kwa madai ya kutumia pasi ya kusafiria ya bandia kuingia nchini humo, maafisa wanasema.

Polisi walifanya msako katika hoteli Asuncion, iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Jumatano, ambako nyota huyo maarufu wa kandanda anasemekana alikua akikaa na kaka yake.

Waziri wa mambo ya ndani wa Paraguay ameliambia gazeti la Brazil -ESPN kwamba Ronaldinho na kaka yake hawajakamatwa bali wanachunguzwa.

Waziri Euclides Acevedo pia amesema kuwa wanakana kufanya kosa lolote na wanaonyesha ushirikiano na mamlaka za Paraguay.

Chanzo cha picha, Fiscalia Paraguay, on Facebook

Maelezo ya picha,

Picha ya kitambulisho cha Paraguay iliyoshirikishwa umma na mamlaka ya Paraguayan yenye jina la Ronaldo

Mwezi Julai mwaka 2019, mchezaji huyo anaripotiwa kuwa paspoti zake za Brazil na Uhispania zilichukuliwa kwa kutolipa ushuru.

"Ronaldinho atasikilizwa na ofisi ya mwendeshamashtaka," waziri Euclides Acevedo aliiambia AFP, na kuongeza kuwa maafisa wa mamlaka za forodha pia watafanya uchunguzi wao .

Maelezo ya video,

World Cup moments: Cheeky Ronaldinho

"Ninaheshimu umaarufu wake wa kimchezo lakini sheria pia lazima ziheshimiwe. Hata kama wewe ni nani, sheria lazima itekelezwe'', Bwana Acevedo aliviambia vyombo vya habari.

Ronardinho mwenye umri wa miaka 39- ambaye alikua mchezaji bora wa mwaka wa dunia mara mbili alikua amesafiri kuingia Paraguay kunadi kitabu chake na kampeni ya kuwasaidia watoto wasio na msaada.

Mwanaume mwingine ambaye aliyefiri na kaka yake mwenye umri wa miaka 45 Wilmondes Sousa Lira - pia amekamatwa.

Ronaldinho alikua mchezaji bora wa dunia mwaka 2004 na 2005 na alifurahia mchezo wake kama mchezaji mwenye haiba ya juu katika timu kubwa ya Uhispania Barcelona.

Alishinda Kombe la Dunia mwaka 2002, sambamba na mchezaji nyota wa mashambulizi Ronaldo na Rivaldo.

Utajiri wa Ronaldinho unakadiriwa kuwa kati ya pauni milioni 80 na pauni milioni 100 na aliripotiwa kuwa hutoza garama ya pauni £150,000 kwa ujumbe ambao aliunadi kwenye Instagram.

Naweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Oscar Litonde: Kwa kupepeta mpira, nataka kuwa bingwa wa dunia