Siku ya wanawake Duniani 2020: Mambo matano unayofaa kujua

Wanawake waandamana

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Huenda umeshuhudia siku ya Wanawake Duniani ikitajwa kwenye Vyombo vya Habari au kusikia kwa marafiki .

Lakini kwa nini? Lini? Je ni sherehe au maandamano? na Je kuna siku kama hiyo ya kimataifa kwa Wanaume?

Kwa zaidi ya karne sasa, watu duniani wamekuwa wakisherehekea siku hii.

1. Ilianzaje?

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.Kilikuwa chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadae.

Chanzo cha picha, ILYAS AKENGIN

Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina Clara Zetkin.

Alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Kulikuwa na wanawake 100 hapo kutoka nchi 17 na wakakubaliana kwa pamoja.

Kwa mara ya kwanza ilisheherekewa mwaka 1911, Austria, Denmark,Ujerumani na Switzerland.

Sherehe ya 100 ilifanyika mwaka 2011, hivyo mwaka huu ni sherehe ya 107 ya wanawake duniani.

Chanzo cha picha, Topical Press Agency

Maelezo ya picha,

Clara Zetkin alianzisha siku hii mwaka 1910

2.Ilikuwalini?

Tarehe 8 mwezi Machi. Wazo la Clara Zetkin la Siku ya kimataifa ya wanawake duniani halikuwa na tarehe maalum na haikuwa rasmi mpaka kipindi cha vita ya mwaka 1917 wakati wanawake wa kirusi walipodai Amani na kufanyia kazi tatizo la upungufu wa chakula (Waliimba Amani na Mkate).

Siku nne za mgomo, zilifanya watawala wa Urusi kuwapa wanawake haki ya kupiga kura.Tarehe ambayo mgomo ulianza ulikuwa kwenye kalenda ya Julian, ambayo ilikuwa ikitumika Urusi wakati huo, ilikuwa siku ya Jumapili tarehe 23 Mwezi Februari.

Siku hii katika kalenda ya Gregoria ilikuwa tarehe 8 mwezi Machi.

Na ndio hii inayosherehekewa leo.

3.Je kuna siku ya wanaume?

Ndio ipo, tarehe 19 Novemba. Lakini iliadhimishwa tangu miaka ya 90 na haitambuliwi na Umoja wa Mataifa.Watu huiadhimisha katika nchi zaidi ya 60. Lengo la siku hii ni kutazama afya za wanaume na wavulana, kuimarisha mahusiano ya jinsia,usawa wa jinsia na kutathimini jinsia ya kiume kama watu wa mfano wa kuigwa.Kauli mbiu ya mwaka 2017 ilikuwa 'kuwaadhimisha wanaume na wavulana'

4.Siku ya wanawake duniani inaadhimishwaje duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mwanamke akiwa amebeba maua mjini Roma, siku ya Wanawake duniani mwaka 2012

Siku ya kimataifa ya wanawake ni siku ya mapumziko katika nchi nyingi ikiwemo Urusi, ambapo mauzo ya maua huwa mara mbili zaidi wakati wa siku tatu au nne kabla ya siku yenyewe, ambapo wanaume na wanawake huwapa maua wapendwa wao wa kike na wafanyakazi wenzao.

Nchini China, wanawake wengi hufanya kazi nusu siku tarehe 8 Machi, kama ilivyoshauriwa na Baraza la nchi hiyo ingawa waajiri si mara zote wanatekeleza utamaduni huo.

Nchini Italia, siku ya kimataifa ya wanawake au La Fiesta della Donna inasheherekewa kwa kupeana maua chanzo cha utamaduni huu hakifahamiki lakini inaaminika ilianzia Roma baada ya vita ya pili ya dunia.

Nchini Marekani, Mwezi Machi ni mwezi wa historia kwa wanawake. Rais hutambua kila mwaka na kuthamini mafanikio ya wanawake wa Marekani.

Nchini China, wanawake wengi hufanya kazi nusu siku tarehe 8 Machi, kama ilivyoshauriwa na Baraza la nchi hiyo ingawa waajiri si mara zote wanatekeleza utamaduni huo.

Nchini Italia, siku ya kimataifa ya wanawake au La Fiesta della Donna inasheherekewa kwa kupeana maua chanzo cha utamaduni huu hakifahamiki lakini inaaminika ilianzia Roma baada ya vita ya pili ya dunia.

Nchini Marekani, Mwezi Machi ni mwezi wa historia kwa wanawake. Rais hutambua kila mwaka na kuthamini mafanikio ya wanawake wa Marekani.

5. Mwaka huu kinafanyika nini?

Kauli mbiu inayoendesha kampeini ya siku ya kimataifa ya wanawake duniani mwaka huu ni usawa kwa sawa #EachForEqual, ambayo inaangazia usawa wa papoja.

"Sote ni sehemu ya dunia moja," kampeini hiyo inasema. "Mchango wetu wa kibinafsi, mtazamo, tabia na fikira zetu zinaweza kubadili jamii kwa ujumla.

"Kwa pomoja, tunaweza kuleta mabadiliko. Kwa pamoja, kila mmoja wetu anaweza kuchangia upatikanaji wa usawa wa kijinsia duniani."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alexandria Ocasio-Cortez alikuwa mwanamke mwenye umri mdogo kuchaguliwa katika bunge la Congress Novemba 2018.

Katika miaka miaka michache iliyopita wanaharakati wa kutetea haki za wanawake walipiga hatua kubwa. Mwezi Oktoba 2017, mamilioni ya wanawake walianza kapeini ya #MeToo katika mitandao ya kijamii ili kupinga unyanyasaji na dhulma za kingono.

Mwaka In 2018, kampeini ya #MeToo ilipata umaarufu duniani, huku mataifa kama vile India, Ufaransa, China, na Korea Kusini yakijiunga na kampeini hiyo kushinikiza mabadiliko.

Nchini Marekani, wanawake walivunja rekodi katika uchafuzi wa katikati ya mhula.

Mwaka jana utoaji mimba ulihalalisha Ireland Kaskazini huku sheria inayodhibiti mavazi ya wanawake nchini Sudan ikifanyiwa mabadiliko.