Simu bilioni moja za Android zimo hatarini kudukuliwa.

Nyingi kati ya simu za Android hazina uwezo wa kupokea mfumo wa kuboresha usalama wake, na hivyo kuziacha katika hatari ya kudukuliwa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nyingi kati ya simu za Android hazina uwezo wa kupokea mfumo wa kuboresha usalama wake, na hivyo kuziacha katika hatari ya kudukuliwa.

Zaidi ya vifaa bilioni moja vya Androiod vimo katika hatari ya kudukuliwa kwasababu havilindwi na app za usalama au waangalizi wa usalama wake ambao wamesema hayo.

Uwezekano wa kudukuliwa unawafanya watumiaji kote duniani kuwa katika kuweza kuiobiwa data au taarifa zao kwa kudaiwa kufanya jambo au mashambulio mengine ya kimtandao kwa kutumia vifaa vinavyoweza kuiba data za mtumiaji.

Mtu yeyote anayetumia simu ya Android iliyotolewa mwaka 2012 au mapema anapaswa kuwa na wasiwasi, ilisema kampuni ya uangalizi wa usalama wa data ambayo inasema haikuridhishwa na jibu ililopewa na Google.

Na kampuni hiyo kubwa ya Android haijajibu ombi la BBC iliyoitaka ijibu juu ya taarifa madai yaliyotolewa kuhusu usalama wa bidhaa zame.

Data za Google zinasema kwamba ni 42.1% ya watumiaji wa Android kote duniani wanaotumia 6.0 ya mfumo wake au chini yake.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu usalama ya Android, hakuna mfumo wa kuimarisha usalama uliotolewa kwa mfumo wa Android mwaka 2019 kwa aina zilizo chini 7.0.

Kuendeleza matumizi ya simu zenye data hizo, ni jambo linaloashiria kuwa simu za Android mbili kati ya tano hazina mfumo wa kulinda usalama wa data kama inavyohitajika.

Halafu ikafanya majaribio ya simu tano:

  • Motorola X
  • Samsung Galaxy A5
  • Sony Xperia Z2
  • LG/Google Nexus 5
  • Samsung Galaxy S6

Simu hizo zilipofanyiwa majaribio ya kiusalama ziliuliza mtumiaji app ya anti-virus AV na hazikutoa chaguo na hivyo kutumia mfumo wa kuiba taarifa na jaribio hilo lilifanikiwa kwa kila simu, na kusababisha athari kwa baadhi ya simu.

Ilisema kuwa iliishirikisha matokeo ya uchunguzi wake kampuni ya Google lakini kampuni hiyo kubwa kiteknolojia "ilishindwa kutoa hakikisho kwamba ina mipango iliyopo ya kumsaidia mtumiaji yeyote wa simu ambaye simu yake haiwezi kusaisiwa kutunza taarifa zake.

Kampuni ya uangalizi wa usalama wa data za simu imesema kuwa Google na watoaji wa huduma za usalama wa mawasiliano wanapaswa kutoa hakikisho la uwazi juu ya ni muda gani simu haiwezi kuwa na usaidizi wa kuboreshwa kwa na ni kwa muda gani uboreshaji wa simu za utafanyika.

Na ilisema kuwa sekta ya simu za mkononi inahitaji kufanya kazi nzuri kwa kuwapa usaidizi wateja juu ya ni nini wafanye baada ya uboreshaji wa simu zao kutowezekana.

Kate Bevan,ambaye ni mhariri wa kpmpyuta, alisema kuwa : " Inatia hofu sana kwamba vifaa ghali vya Android havina muda mrefu wa kuishi kabla ya kupoteza uwezo wa usaidizi wa usalama , na hivyo kuwaacha mamilioni ya watumiaji katika hatari ya athari mbaya ikiwa vitaangukia mikononi mwa wadukuzi tim to

Google ana watengenezaji wa simu za mkononi wanahitaji kuwa mbele katika uboreshaji wa app za usalama-kwa kuwa na taarifa zinazoeleweka juu ya ni muda gani zinaweza na wateja wanapaswa kufanya nini zinaposhindwa kuboreshwa.

"Serikali lazima pia ziweke sharia kuhakikisha watengenezaji wanakuwa na uwazi juu ya usalama wa uboreshaji wa vifaa vya smart- na athari zake kwa watumiaji."

Chanzo cha picha, SAMSUNG

Maelezo ya picha,

Samsung Galaxy S6 ilitolewa sokoni mwaka 2015

Jinsia ya kuangalia ikiwa simu yako inaweza kudukuliwa na la kufanya

  • Kama aina yako ya kifaa cha Android kimedumu kwa zaidi ya miaka miwili , angalia kama kinaweza kuboreshwa na kuwa cha kisasa (update) na kuwa katika mfumo mpya. Kama unatumia aina ya zamani kuliko Android 7.0 Nougat, jaribu kukiboresha kwa mfumo mpjya (update) kupitia mpangilio ama Settings> System>Advanced System update.
  • Kama hauwezi ku update, simu yako inaweza kuwa katika hatari ya kudukuliwa, hususan kama unaytumia mfumo wa Android 4 au wa chini zaidi. Kama hivi ndivyo ilivyouwe makini katika kupakua app nje ya Google Play store.
  • Pia uwe makini na jumbe unazozipokea.
  • Tunza data zako walau katika maeneo mawili ya ziada (hard drive na cloud service)
  • Weka mfumo wa kupambana na virusi au anti-virus kupitia app, lakini ufahamu kuwa unaweza kutumia huduma hiyo kwa kiwango kidogo unapokua na simu za zamani.