Coronavirus: Jitihada za Zanzibar kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona

Coronavirus: Jitihada za Zanzibar kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona

Hatua hii imekuja baada ya kuendelea kwa maambukizi nchini Italia.

Siku chache tu zilizopita taarifa zilisema kuna mtalii raia wa Italia alitoka visiwani Zanzibar, aliporudi nchini kwao Italia alikutwa na virusi.

Waziri wa afya visiwani Zanzibar Hamad Rashid ameiambia BBC kwamba ugonjwa huu utaathiri uchumi visiwani humo na hasa sekta ya utalii, lakini serikali imejipanga kudhibiti athari hizo.

Haya hapa ni mahojiano yake na mwenzetu Sammy Awami ambapo kwanza Wazir Rashid alianza kwa kuelezea hali ilivyo hivi sasa visiwani humo.