Coronavirus: 'Unyanyapaa' ulivyochochea chuki dhidi ya Wachina nchini Kenya

Abiria kutoka China wakiwasili uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wageni wakiwasili nchini Kenya kutoka katika ndege iliyotokea China, walikuwa wakikaguliwa afya yao kabla hawajaingia nchini humo mwezi Januari

Katika mfululizo wa barua za Afrika, mwandishi wa Kenya Waihiga Mwaura anaelezea ni namna gani virusi vya corona vilivyoweza kuchochea chuki dhidi ya wageni na raia wa China.

Licha ya kwamba kila kona ya dunia virusi hivi vimekuwa tishio, lakini adui mkubwa wa ugonjwa huu si virusi vyenyewe bali ni "hofu, uvumi na unyanyapaa".

Si maneno yangu ,lakini kwa wale Waethiopia ambao wanaongoza duniani kupunguza athari za ugonjwa wa Covid-19.

Mkuu wa Shirika la afya duniani, Tedros Adhanom Ghebreyesus alijibu mwezi uliopita kuhusu kesi ya unyanyapaa dhidi ya wachina.

Alirudia ujumbe wake kwenye ukurasa wa Twitter mapema wiki hii aliposimulia stori ya mwanaume kutoka Singapore alivyopigwa nchini Uingereza mjini, London, kwa sababu ya virusi vya corona.

Hali ya unyanyapaa inazidi kuenea na Kenya haina utofauti na nchi nyingine.

'Wewe ni virusi vya corona'

Filamu ya video ya kusikitisha inayosambaa mitandao ya kijamii ikionyesha mwanaume na mwanamke wenye asili ya bara la Asia wakinyanyaswa na kundi kubwa la watu wenye kipato cha chini katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Video hiyo imeanza kwa mtu ambaye hajulikani katika kundi kubwa la watu akipiga kelele:

"Wewe ni kirusi cha corona, wewe ni virusi vya corona."

Mwanaume alijibu huku akitaka kupiga picha tukio lile lakini aligundua kuwa mwenzake mwanamke anlikuwa katika hatari hivyo akakimbiliakumsaidia .

Mwanaume huyo alisimama katikati ya kundi la watu na kuanza kuwajibu kwa kelele: "Hatuna corona, hatuna corona."

Video ilisimamishwa kaba ya kuona tukio zima mpaka mwisho, lakini hali hiyo ni kutokana na athari za upande mwingine wa virusi vya corona.

Februari 27, ujumbe ulisambaa katika mtandao wa Facebook, ukidai kuwa mbunge mmoja wa Kenya ametaka wananchi wa jimbo lake kuepuka kuwa na muingiliano na raia wa China ambao wamerejea kutoka kwao baada ya sherehe za mwaka mpya wa China.

Ujumbe huo ulionya kuwa kama serikali haitawalinda raia wake, basi watalazimika kuwaweza raia wote wa China katika karantini.

Na vilevile wananchi watakuwa na ruhusa ya kumkimbiza yeyote kwa mawe katika jimbo lao.

Ubalozi wa China' uijibu madai hayo haraka kwenye kurasa ya Twitter kutaka jumuiya za watu kutoka China kulindwa na watu kuacha ubaguzi.

Si Kenya peke yake ambayo ilionyesha chuki ya aina hiyo bali kuna mataifa mengine ya angwa la sahara ambayo yanahusisha wasafiri waliotoka China.

Huku kukiwa hakuna unyanyapaa wa aina hiyo kwa wageni kutoka ulaya.

Kabla ya Kenya haijarekodiwa kwa kesi hiyo lakini chanzo cha hayo yote ni hofu na mchanganyiko wa unyanyapaa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Baadhi ya wakenya wakifanya kampeni kuzuia ndege kutoka China kuingia nchini mwao

Ubaguzi huo umeathiri uhusiano wa kiuchumi wa China na Kenya

Kenya iliazima kiasi kikubwa cha fedha kutoka China kwa ajili ya kujenga miradi yake mikubwa.

Wakati raia wa Kenya wa kawaida wakiwa haoni manufaa wanayopata, wanatafuta mtu wa kumlaumu kwa kushuka kwa uchumi wao.

Wamechoka kunyooshea kidole serikali, wengine wakiwalamu baadhi ya raia wa China waliokuja kwa wingi kutafuta fursa za kiuchumi.

Hofu ya virusi vya corona pia inafanya tabia ya ubaguzi kuongezeka.

Adrian Blomfield, ni mwandishi wa habari wa kujitegemea ambaye anasema kuwa gari binafsi zimekubaliana kukataa kubeba abiria ambao ni raia wa China.

Dereva mmoja wa taxi alisema kuwa raia wa China wamekuwa wakibadili majina yao katika programu za kuita gari za kukodi ili ombi lao lisikataliwe.

Chanzo cha picha, Reuters

Vilevile alieleza kuwa abiria wanaowatoa katika uwanja wa ndege lazima washushe vioo na kuvaa mask.

Na kuogeza kusema kuwa wanataka serikali kuwapa mask madereza wote wa taxi za uwanja wa ndege na kutoa taarifa zaidi kwa jamii.

Serikali imekosolewa kwa kutochukua hatua za haraka kuelimisha watu kuhusu virusi vya corona na kuwaonya kuhusu ubaguzi.

Uvumi ndio umefanya watu kwa na taarifa ambazo si sahihi.

Kampeni za uhamasishaji zimeanza kwa kuchelewa.

Raia wa China ambao wanaoishi Kenya kama Lin Yimenghan, ambaye ana asasi ya kusaidia wahitaji anasema kuwa aliwahi kushuhudia mtu anamuita "coronavirus" akiwa katika kituo cha basi Nairobi.

Taarifa zinasema kuwa hali hii si ya kusahaulika.

"Ni jambo la kawaida kwa watu kuwa na hofu ya kitu ambacho hawana taarifa nacho."

Kuenea kwa unyanyapaa kwa kasi zaidi ya virusi vyenyewe vya corona, watu wanahitajika kuwa na upendo na ueleo kwa wenzao.

Kama kila mtu atakuwa na tabia ya upendo basi dunia ingekuwa na amani zaidi.