Zaidi ya wasichana milioni 130 hawaendi shule

Learning in Niger

Chanzo cha picha, GPE/Kelley Lynch

Maelezo ya picha,

Mradi huu unawaweka wasichana wengi shule huko Niger - wakati mataifa mengi wasichana wanaacha shule

Chukua muda wako kusoma simulizi hii inayohusu mabinti 15 ambao wangeweza kuwa wamezaa- katika mataifa masikini zaidi duniani na inawezekana wasingeweza kurejea shule .

Julia Gillard, ni waziri mkuu wa zamani wa Australia ambaye anafanya kampeni ya kupambania haki za wasichana kubaki kupata elimu, na kulieleza suala hilo kuwa ni la haraka.

Kuna wasichana zaidi ya milioni 130 ambao wameacha shule.

Wengi wako pembezoni na si rahisi kuwafikia, alisema bi. Gillard.

Yeye ni mwenyekiti wa mahusiano ya elimu duniani yaani- Global Partnership for Education (GPE), ambapo wanatafuta ufadhili kutoka mataifa yaliyoendelea kwa ajili ya kuwasaidia wasichana walio nchi 70 masikini.

Chanzo cha picha, GPE/Kelley Lynch

Maelezo ya picha,

Huko Mauritania ,ufadhili huo unasaidia wasichana wengi kupata elimu zaidi ya shule ya msingi

Serikali ya Uingereza imekuwa ikiunga mkono jitahada hizo kwa miaka zaidi ya 15 iliyopita na imeweza kutoa karibu yuro bilioni moja.

Mradi huo wa GPE umeweza kusaidia ongezeko la wanafunzi shuleni - kutokana na kipato kuwa cha chini kwa mataifa ya ukanda wa jangwa la sahara, wasichana wengi wanajikuta wanakosa kwenda shule.

Ripoti kutoka Umoja wa mataifa imezionya mataifa masikini mapema mwaka huu kwa kuwa mabinti kati ya miaka 10 na 18 ambao hawajaenda shule.

Chanzo cha picha, GPE/Kelley Lynch

Maelezo ya picha,

Nchini Ethiopia kuna mradi ambao unalinda mabinti wa kike na unyanyasaji wa kijinsia wakati wanapokwenda shuleni au chuo

Kuna hatari kuwa watoto hao wameolewa katika umri mdogo au wameenda kufanya kazi , ambazo zitaweza kusaidia familia kupata kipato cha kununua chakula.

Pamoja na haki ya mtoto kupata elimu, Bi Gillard anasema kuwa kuwapeleka watoto shule ni jambo muhimu ambalo linaweza kuinua uchumi.

Kupanua upatikanaji wa elimu kwa mabinti kuna faida nyingi katika jamii kwa kuwa elimu inasaidia wanawake kupata ajira kiurahisi, kuolewa katika wakati muafaka na kutunza familia vyema pamoja na kuzingatia masuala ya afya ya kizazi kijacho.

Kama lengo ni uchumi kuweza kuleta maendeleo, amani na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi-basi haya yote yanaweza kufanikiwa binti atakapopata elimu," alisema bi. Gillard.

Chanzo cha picha, GPE/Kelley Lynch

Maelezo ya picha,

Wamekuwa wakisaidia kutoa vitabu vya masomo ya lugha mama huko Niger

Dunia ikiwa inasheherekea siku ya mwanamke duniani, alisema kuwa ufadhili wa GPE umeweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wasichana wengi katika mataifa kama Kenya, Malawi na Afghanistan.

Kipaumbele cha bi. Gillard ni kufanya elimu ya msichana inapatikana.

Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amesema kuwa katika miaka 12 wasichana wote wataweza kupata elimu.

Bwana Johnson amekuwa akirudia wito wake wa kusaidia elimu duniani.

Maelezo ya picha,

Bi.Julia Gillard anaamini katika uwekezaji wa elimu ya binti

Bi Gillard anaamini kuwa ahadi alizotoa bwana Johnson ni za ukweli na ana nia dhabiti kufanikisha suala hilo kwa kwa ndio ufungua wa kukabiliana na matatizo mengi.

"Ameshuhudia matokeo yake na kusoma ushaidi."

Alipozungumza na BBC, wakati bwana Johnson alipokuwa waziri wa mambo ya nje alisema: Katika mataifa ambayo ni masikini, kuna vita vya kila mara na wingi wa watu,; elimu ndi changamoto kubwa.

Na sasa Bi. Gillard anataka waziri mkuu wa ingereza kuanzisha mjadala kwa viongozi wa mataifa mengine makubwa yanayofahamika kama G7.

Zaidi ya miaka 30 iliyopita, dunia imeweza kujaribu kufanikiwa kuhakikisha kila mtoto anajiandikisha kupata elimu ya msingi lakini sasa una lengo la wanafunzi kutokuwepo shule.

Chanzo cha picha, GPE/Kelley Lynch

Suala la elimu si la taifa moja bali ni la dunia nzima, kila mtu anazungumzia tatizo la virusi vya corona lakini ikumbukwe kuwa elimu ni tatizo ambalo halina mipaka pia, aisema bi Gillard.

Matokeo ya kutokuepo kwa usawa ,vurugu na migogoro ya mipaka na mataitzo ambayo mataifa tajiri yanaona kuwa yako mbali nayo, ni swali la kujiuliza yanaathiri vipi limwengu.

Kama elimu ikipatiana kwa wote masuala gani yatabadilika.