Sababu zinazofanya wanawake kujifanya wamefika kileleni

Orgasmo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kulingana na utafiti wa hivi karibuni, idadi kubwa ya wanawake walikiri kwamba kujifanya kuwa wamefika kileleni ni jambo la kawaida

Idadi kubwa ya wanawake waliozungumza na BBC, walisema kwamba kuna wakati walijifanya kuwa wamefika kileleni wakati wa tendo la ngono japo haikuwa ukweli.

Hatahivyo kulingana na wataalamu hili ni jambo la kawaida.

Kulingana na utafiti uliochapishwa Novemba 2019 kuhusiana na tabia za ushiriki wa tendo la ndoa, asilimia 58.8 ya watu 1008 walioshirikishwa kutoka umri wa miaka 18 hadi 94 walisema kwamba washawahi kujifanya kwamba wamefika kileleni.

Kati ya hao, asilimia 3 walisema hufanya hivyo kila wakati japo kwa sasa wameacha huku asilimia 55 wakiitambua kama tabia ya kawaida.

Lakini kwanini imekuwa jambo la kawaida?

Kiwango cha Uwongo

Kwa Blanca, kujifanya kwamba umefika kileleni imekuwa jambo la kawaida baada ya kupata mtoto wake wa kwanza.

"Baada ya kujifungua hamu yangu ya kushiriki tendo la ndoa ilikuwa imepotea. Sikuwa ninajiamini tena kwasababu ya vile mwili wangu ulivyobadilika. haukuwa sawa''.

Pia alikuwa anahisi kuchoka sana, na baada ya kurejea kazini mambo yalibadilika.

''Nilikuwa na uchovu mwingi kiasi kwamba kufanya tendo la ndoa na mume wangu ilikuwa kibarua kigumu.''

Na kwasababu nilikuwa na wakati mgumu kutuliza akili wakati wa tendo la ndoa - kila wakati nilikuwa nafikiria kile ninachotakiwa kufanya ofisini, tunachohitaji kuwa nacho kwenye jokovu, ikiwa kilio cha mtoto kilikuwa kawadia ama pengine ana shida... siku moja nikaamua kujifanya kwamba nimefika kileleni.

Sio kwasababu hakuwa ananifurahisha tena, hapana, nilikuwa ninataka kulala. "

''Pia kwasababu ya kuogopa talaka'', Luz Jaimes, aliongeza, mtaalamu wa masuala ya ngono amesema,

"Kuna idadi kidogo ya wanawake ambao wanaogopa kwamba waume zao wanawaacha kwasababu wao sio wazuri tena ama pengine wameanza kuzembea wakiwa kitandani," na kwa baadhi yao kufika kileleni huenda ikawa ishara ya weledi wao katika masuala ya ngono.

Kwa Kuiga au kukerwa

Laura Morán, mwanasaikolojia na mtaalamu wa masuala ya ndoa, anazungumzia aina mbili za kujifanya kwamba mtu amefila kileleni.

"Ama tunafanya kwa kuigiza kwasababu tuna mahusiano ya kimapenzi yenye kuhusika moja kwa moja na video za ponografia hasa zile za mapenzi ambazo zinaonesha hatua kwa hatua vile mtu anavyofika kileleni baada tu ya kama dakika mbili na hili hutokea ili mtu asionekane kwamba yeye ni wa ajabu. Ama kwasababu ya kile anachokiita kuudhika "unajifanya umefika kileleni kwasababu ya maudhi."

Hiki ndicho alichokifanya Laura baada ya kukutana na mpenzi wake walipofunga pingu za maisha: na kuamua kumpa zawadi hii, kwamba amefika kileleni ilihali ni uwongo.

"Baada ya siku nzima na sehemu ya sherehe ya usiku, nilijua kwamba haitakuwa kazi rahisi. Lakini mwanaume wake alivumilia. Tulijaribu kila aina ya mbinu na ikafika wakati sikuweza tena", anakumbuka.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ingawa wanawake wanahisi kwamba wana haki ya kufika kileleni, lazima tukubali kwamba unakuwa vigumu kufika huko, amesema Laura Morán.

"Najua kwamba tunastahili kuzungumzia kile tunachopenda na kinachotukera, na pia ni vizuri kuwa m'kweli lakini siko hapa kufindisha kila mmoja," anasema Fernanda, 33.

Wanaume pia nao hujifanya kwamba wamefika kileleni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Asilimia 21.2 ya wanaume walioshiriki utafiti wa kampuni moja ya utengenezaji bidhaa za kuamsha hashiki wamedai kwamba kuna walijifanya kuwa wamefika kileleni.

Hisia za kufika kileleni sio kitu au jambo la kikazi fulani.

Na sio kwamba hil hutokea tu kwa wanawake au kwa wanaoshiriki mapenzi ya mke na mume pekee, wanafunzi walioshirikishwa wamesema.

"Tabia ya ngono kwa wanandoa wa jinsia moja ni sawa na wale wa jinsia tofauti na kujifanya kwamba umefika kileleni ni jambo linalotokea kila wakati,"amesema Jaimes.

Kwa wanaume, utafiti unaonesha japo kwa kiasi kidogo pia nao hudanganya kwamba wamefika kileleni.

Hili lilibainika katika utafiti uliofanyiwa watu 1,400 na kampuni ya kutengeneza bidhaa za kuamsha hashiki. Kulingana na utafiti huo asilimia 21.2 ya wanaume waliwahi kujifanya kwamba wamefika kileleni ikilinganishwa na asilimia 52.1 ya wanawake.

Na asilimia 8.4 walisema kwamba huwa wanadanganya karibia kila siku ikilinganishwa na asilimia 11.8 ya wanawake

"Wanajifanya kwamba wamefika kileleni wakati wanapopoteza msisimko ama wakiwa na wakati mgumu kuudumisha kwasababu pengine wana wasiwasi fulani ama kwasababu wanatumia dawa ambazo zinachelewesha kufika kileleni," amesema Moran.

"Iwapo wametumia mpira wa kondomu, inapofika katikati ya shughuli, huivua bila ya mpenzi mwengine kuona kwasababu hilo ni kosa la uhalifu."

Baada ya yote hayo kinachojitokeza ni kwamba iwapo utashiriki mapenzi kwa kujifurahisha na ukaishia kudanganya kwamba umefika kileleni kile unachopata ni msongo wa mawazo na kupoteza hamu, kulingana na Jaimes.

Kwa hiyo iwapo hautapata kujitosheleza, hamu ya kuwa na mahusiano ya mapenzi hupungua na ikiwa mtu atapuuzwa ataishia kutokuwa na uhusiano wa kingono".