Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok anusurika kuuawa

Abdalla Hamdok

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Abdalla Hamdok aliapishwa kuwa waziri mkuu mwezi Agosti mwaka jana.

Waziri mkuu wa Sudan amenusurika kuuawa katika jaribio la shambulizi lililotokea katika mji mkuu wa Khartoum.

"Ninataka kuwahakikishia watu wa Sudan kuwa niko salama na niko katika hali nzuri," Abdalla Hamdok ameandika katika kurasa yake ya tweeter.

Bwana Hamdok alichaguliwa kuwa kiongozi wa serikali ya mpito ya Sudan mwezi Agosti, miezi michache baada ya kuondolewa madarakani aliyekuwa rais wa muda mrefu nchini humo bwana Omar al-Bashir.

Alisema kuwa shambulio hilo limekuja wakati ambao kulikuwa na uchochezi wa mabadiliko nchini Sudan.

Haijawa wazi bado ni nani alihusika katika shambulio hilo lakini hali ya kisiasa nchini Sudan bado haijatengamaa kutokana serikali ya mpito kuongoza na watu ambao walikuwa katika ngazi za juu haswa kwenye jeshi.

Nini kilitokea?

Picha zilizoonyeshwa katika televisheni ya taifa, zinaonyesha namna gari hilo lilivyoharibika katika eneo ambalo mlipuko ulitokea, AFP imeripoti.

Chanzo cha picha, AFP

"Bomu lilipiga gari la waziri mkuu Abdalla Hamdok ambalo gari hilo likiwa linaendeshwa lakini kwa neema za Mungu, hakuna aliyejeruhiwa", Ali Bakhit alikiambia chombo cha habari cha AFP.

Waziri wa habari Faisal Salih alisema kuwa wameanza kufanya uchunguzi ili kubaini ni nani anahusika na shambulizi hilo la kigaidi.

Imeripotiwa kuwa alihamishiwa katika eneo salama.

Kwa mujibu wa Reuters , walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa shambulio hilo lilitokea karibu na kaskazini mashariki mwa mwanzo wa daraja la Kober, ambalo linaunganisha kaskazini ya Khartoum na mjini, eneo ambalo waziri mkuu anaishi.

Jaribio la shambulizi hilo linaonekana kuwa lilitoka juu, shaidi alisema.

Niliona kama mlipuko ulitoka katika gorofa, mmoja wa mashaidi alisema.

Bwana Hamdock ni nani?

Bwana Hamdok ni kiongozi wa adhi ya juu wa zamani wa uchumi wa Umoja wa mataifa na kipaumbele chake ni kutatua janga la kiuchumi la Sudan.

Yeye alichaguliwa kuongoza katika serikali ya muungano wa raia sita na wanajeshi watano.

Baraza la uongozi lilitokea baada ya mvutano wa miezi kadhaa kati ya wanajeshi na raia ambao walikuwa wanaandamana wakitaka wanajeshi warudi kambini baada ya kumuondoa bwana Bashir mwezi Aprili 2019.

Wanajeshi walilenga kuwa kuongoza uraiani kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa mujibu wa Reuters, tangu kuchaguliwa kwa bwana Hamdok, serikali yake imekuwa ikipingwa wakati wakati ikijaribu kufanya mabadiliko ya kiuchumi.

Aidha waziri mkuu alisema kuwa kushambuliwa kwake hakutazia mabadiliko hayo kufanyika.

"Tumefanya jitihada nyingi kupata mabadiliko haya kwa ajili ya kesho iliyo bora na kuwa na amani.Mapinduzi yetu mara zote yaongozwe kwa amani," aliandika kwenye kurasa za tweeter.