BBC Africa Eye: Kwa nini Gambia inauza miti China ilihali haina misitu?

BBC Africa Eye: Kwa nini Gambia inauza miti China ilihali haina misitu?

Gambia imekuwa ikisafirisha zaidi ya tani laki tatu, za mbao zinazotokana na miti ya mwaridi ama Rosewood kwenda nchini China tangu mwaka 2017, Rais wa nchi hiyo Adama Barrow alipoingia madarakani.

Uchunguzi uliofanywa BBC Africa Eye umeonesha kuwa mbao nyingi hupatikana kimagendo kutoka nchi jirani ya Senegal, ambako misitu ya nchi hiyo imekuwa ikiporwa kwa kiasi kikubwa, licha ya miti hiyo ya mwaridi inayopatikana Afrika Magharibi kulindwa.