Kukamatwa kwa wanamfalme wa ngazi ya juu watatu wa Saudia kuna maana gani?

Mohammed Bin Salman(left), Mohammed Bin Nayef (centre), and King Salman (file photo)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mohammed Bin Nayef (katikati) - mwanamfalme wa zamani aliyekua mamlakani - ni miongoni mwa wale wanaoshikiliwa

Kukamatwa kwa wanamfamlme wa ngazi ya juu na kiongozi wa kiimla , Mwanamfalme aliyeko mamlakani Mohammed bin Salman, kumeibua wimbi la uvumi juu ya ni kwanini waliondolewa ghafla mamlakani.

Si ajabu kwamba utata huu umeibuka , Mwanamfalme Mohammed bin Salman (al maarufu MBS) ameonyesha kutumia mbinu chafu kushinikiza kupata mamlaka ya juu zaidi ya ufalme huo na upinzani dhidi yake kutoka kila nyanja umeongezeka kuanzia mwaka 2015.

Suala la kuibuka kwa tamaa ya MBS wakati huu liliibuka kutoka kwa wajumbe wa familia ya Saudi - hususan ni mmoja wa wajomba zake, Mwanamfalme Ahmed bin Abdul Aziz, wazairi wa zamani wa mambo ya ndani na binamu yake , Mwanamfalme Mohammed bin Nayef (anayefahamika kama MBN), ambaye alikua mwanamfalme wa zamani aliyekua mamlakani na waziri wa mamnbio ya ndani - ambao walifungwa kwa kuhojiwa na kuchunguzwa kwa tuhuma za uhaini, licha ya kwamba hakuna mashitaka yaliyotolewa.

Unaweza pia kusoma:

Hakuna yeyote kati yao ambaye ana mamlaka tena. MBN aliondolewa ofisini bila utaratibu wowote mwaka 2017 wakati Mfalme Salman alipotoa fursa kwa MBS - mwanae kukalia kiti cha ufalme, na Mwanamfalme Ahmad alipendelea kutumia muda wake na pesa zake katika jiji la London kabla ya kurejea katika ufalme wake mwishoni mwa mwaka jana.

Swali ambalo wengi wanajiuliza ni je ni kwanini MBS aliamua kwa mara nyingine tena kuwawinda mahasimu wake, hususan ikizingatiwa kwamba tayari walikua dhaifu na hawakua na uwezo wa kupinga kiu yake ya mamlaka?.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Mohammed Bin Nayef (katikati) - mwanamfalme wa zamani aliyekua mamlakani - ni miongoni mwa wale wanaoshikiliwa

Ni yeye pekee anayejua jibu halisi , na katika nchi isiyo na uwazi kama Saudi Arabia haitawezekana kupata ukweli kamili kutoka kwa vyanzo vya maafisa wa Saudia.

Lakini jambo moja ni ambalo ni dhahiri ni kwamba - Mwanamfalme kijana aliye mamlakani alifahamu fika kwamba hakutakua wa athari kubwa iwe ya kitaifa au kimataifa.

Tetesi na shauku

Kutokana na kwamba aliweza kunusurika na wimbi la ukosoaji mkubwa lililofuatia mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudia Jamal Khashoggi katika ubalozi wa Saudia mjini Instanbul mwaka 2018, MBS hana la kumtia hofu.

Ikulu ya White House ya Trump ilimuunga mkono MBS; Uingereza na Ufaransa walimkosoa kidogo, lakini bado waliendelea kufanya biashara na Riyadh; na Urusi na Uchina hawakujali lolote.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Donald Trump amekua mshirika wa karibu wa MBS

Na kwahivyo MBS ameweza kufanya kufanya kila awezalo kupata mamlaka kwa kutumia mbinu katili , kupata mamlaka kwa kuzitenga sekta zote za umma wa Wasaudia-wawe viongozi wa kidini, wafanyabiashara wala makundi ya haki za binadamu- na kuwamaliza mmoja baada ya mwingine kwa nguvu za dola.

Ni siasa za Dikteta 101, lakini katika mtindo wa karne ya 21. Mwanamfalme amewekwa katika mazingira mazuri, kama vile Mwanamfalme wa Riyadh Ritz-Carlton mwaka 2017, na MBS amekua makini kuonekana myenyekevu, kama alivyofanya wakati wa MBN mwaka huo huo, alipopiga magoti na kumbusu binamu yake akinyenyekea na kumuomba kwa unyenyekevu.

Lakini kama mtu aliyekua na uwezo kama MBN alikua katika utawala wa taasisi za usalama wa kitaofa wa Ufalme, hakuwa ametayarishwa, na hakuweza kukithi haja na tamaa ya MBS na ujasusi.

Wenye mamlaka ndani ya familia ya ufalme wa Saudia kila mara hubadili maneneo na uvumi uliopo unasema kwamba Mfalme Salman alikua karibu kufa, au kwamba MBS alihisi kuwa kulikua na mpango wa mapinduzi ya ufalme na akaingilia kati haraka kuyazima.

Hapakua na ukweli juu ya madai haya, ambayo yalipuuza majibu ya kawaida: Kulikua na ujumbe kutoka Salman na MBS kwa wanafamilia wengine kufuata sheria, kitendo cha nidhamu ambacho kitaunusuru ufalmne na kumkumbusha kila mmoja ni nani bosi.

Na usifanye kosa lolote, bila shaka MBS ndie bosi wa Saudi Arabia.