Contagion: Je filamu iliyotolewa takriban miaka 10 iliyopita ilibashiri mlipuko wa virusi vya corona?

Contagion movie poster Haki miliki ya picha Warner Bros
Image caption Contagion ilikua ni filamu ya 61 kwa kuingiza mapato ya mwaka 2011 lakini imepata umaarufu kutokana na mlipuko wa Covid-19

Filamu ya Contagion ilitolewa mwaka 2011 na haikutambulika kuwa mojawapo ya filamu maarufu wakati huo

Licha ya kuwahusisha wachezaji maarufu mkiwemo Matt Damon, Jude Law, Gwyneth Paltrow, Kate Winslet na Michael Douglas, filamu hiyo ilikuwa ya 61 miongoni mwa filamu zuilizoingiza zaidi mapato ya mwaka huo.

Lakini Contagion imerejea ghafla kwenye orodha ya filamu zilizopakuliwa zaidi katika Apple's iTunes Store nchini Marekani, huku jina lake likisakwa zaidi Google.

Warner Bros. - studio ambayo ilitengeneza filamu ya Contagion - imesema kuwa ilikuwa ni ya 270 katika ya filamu maarufu mwezi Disemba, wakati taarifa ya kwanza ya mlipuko wa virusi vya corona au Covid-19 ilipotangazwa nchini Uchina .

Miezi mitatu baadae , Contagion iko nyuma tu ya filamu nane za Harry Potter franchise.

Yote hayo yamesababishwa na virusi vya corona , na kufananishwa kwa mlipuko wa hivi karibuni wa virusi vya corona na kilichoongelewa katika filamu muongo mmoja uliopoita

Sanaa ya maigizo ya maisha

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gwyneth Paltrow alikua akicheza kama mgonjwa zero wa mlipuko katika filamu Contagion

Katika filamu hiyo , nafasi ya mfanyabiashara mwanamke (ilichezwa na Paltrow) ambaye anaonekana akiuliwa na ugonjwa wa ajabu wa virusi alivyovipata alipokua katika safari yake ya Uchina, lakini baada ya kusababisha dharura ya afya kote duniani.

Uhusiano na Uchina ni mojawapo ya mambo mengi ya maisha halisia ambayo yameongeza umaarufu wa filamu hii katika wiki za hivi karibuni, huku watazamaji wakiitazama sana filamu ya Contagion.

Nia ya kutaka kuitazama filamu hii ilichochewa na ujumbe uliotumwa na Gwyneth Paltrow: mchezajifilamu mwanamke wa Kimarekani aliyetuma picha yake akiwa amevalia barakoa katika ndege iliyokua ikisafiri tarehe 26 Februari ikivuka maeneo ya pacifiki .

"Njia kuelekea Paris. mfadhaiko? Mkanganyiko ? mtulivu ? mlipuko ? Propaganda? Paltrow anaendelea na yote haya tu na kusinzia ndani ya ndege ,"zilisomwa ujumbe zake za Instagram

"Tayari nimeishawahi kuwa ndani ya filamu hii . Muwe salama . Msishikane mikono. Mnawe mikono mara kwa mara." mchezaji filamu huyo mwenye ufuasi wa watu milioni 6 kwenye mtandao wa kijamii , aliandika.

Mambo yanayofanana

Kuna mambo ya kushangaza yanayofanana ya hali halisi na yaliyomo katika filamu ya Contagion.

Mchezaji filamu Paltrow anapata virusi , vinavyoitwa MEV-1, kutoka kwa mpishi wa Hong Kong ambaye alimchinja nguruwe ambaye alipata maambukizi kupitia popo - kwa kusalimiana kwa mikono.

Halafu anasafiri kwa ndege kurudi nyumbani na kuugua sana, na kufa muda mfupi baadae. Baadae mwanae wa kiume anakufa pia, nafasi iliyochezwa na mume wake Matt Damon anabainika kuwa na kinga.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kama ilivyo kaytika filamu ya Contagion, maafisa wa afya wanaamini kuwa mlipuko wa Covid-19 ulianzia kwa wanyama na kuenezwa kwa binadamu.

Katika maisha halisi, wataalamu wa afya wanaamini kuwa maambukizi ya binadamu kwa binadamu katika mji wa Uchina wa Wuhan ndiko ulikoanzia mlipuko wa Covid-19 mwezi Disemba.

Hata haikufikiriwa kwamba hii coronavirus pia ilianzia kwa ndege, kama tu ilivyokua katika mlipuko wa Sars wa mwaka 2002-03. Halafu uliambukizwa kwa binadamu kupitia viumbe wangine.

Jambo la kushangaza

Yaliyochezwa kwenye filamu na ugonjwa halisi husabishamatatizo ya kupumua, lakini MEV-1 ni jina lililotokana na virusi halisi vinavyoitwa Nipah, ambavyo haviko katika familia moja na virusi vya Covid-19.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Popo wamehusishwa na virusi vya kufikirika katika filamu ya Contagion vya MEV-1 na vile halisi vya Covid-19

Kutengwa

Wakati mlipuko unaposhukiwa katika filamu, wahudumu kutoka huduma za uchunguzi wa mlipuko - Epidemic Intelligence Service - ambalo ni shirika halisi -wanasambazwa kujaribu kutambua na kuwatenga watu walioambukizwa.

Katika filamu, mji wa Marekani wa Chicago ni sehemu ya maeneo yenye taswira ya umati wa watu waliotengwa, jambo ambalo lilifabyika Uchina.

Italia pia sasa imeyatenga majimbo kadhaa ya kaskazini mwa nchi kwa lengo la kukabiliana na kusambaa kwa Covid-19.

Kurejea tena kwaumaarufu wa filamu ya Contagion kumemshangaza Scott Z Burns, ambaye aliyeandika maneno ya filamu.

Lakini katika mahojiano na jarida la Fortune alisema kuwa wazo la awali la Contagion lilikua ni kuionyesha jamii ya sasa kuwa inakabiliwa na tisho la kupata milipuko ya aina hiyo.

"Kile kilicho muhimu zaidi na cha uhakika ni jinsi jamii inavyokabiliana na kuenea kwa hofu na athari za mlipuko wenyewe ."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Scott Z Burns wrote the script for contagion

Huenda alikua akizungumzia mchezaji mmoja katika filamu ya Contagion : nadharia ya mpango wa siri ya mwanablogi aliyeitwa Alan Krumwiede.

Nafasi iliyochezwa na Jude Law, Krumwiede alisambaza taarifa za uvumi zisizo na msingi wowote juu ya virusi na kutoa taarifa gushi juu ya toba ya virusi.

.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption The Nipah virus, which has a fatality of up to 75%, served as inspiration for the disease in Contagion

Ukweli wa kuaminika wa kisayansi

Umaarufu wa filamu ya Contagion unaweza pia kuelezewa kwa jinsi Burns alivyotaka kujitolea kuhakikisha kwamba inaaminiwa kisayansi.

Aliomba ushauri kwa jopo la wanasayansi wataalamu wa virusi na wataalamu wa milipuko, mkiwemo WHO, alipokua akiandika mistari ya maneno ya filamu

Walimpa baadhi ya ushauri wa kuaminika

" Nilipozungumza na wataalamu katika sekta hii, wote waliniambia kwamba mlipuko sio suala la kama, bali ni suala la lini " Burns alimwambia mwandishi wa habari wa Hollywood.

Mada zinazohusiana