Ajali ya ndege ya Ethiopia: Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza asimulia alichoshuhudia

Ajali ya ndege ya Ethiopia: Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza asimulia alichoshuhudia

Familia za watu 157 waliofariki katika ajali ya ndege ya Ethiopia mwaka mmoja uliopita zitafanya hafla ya ukumbusho ya ajali hiyo katika eneo la tukio leo Jumanne. Ndege ya Ethiopia Nambari 302 ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji kuu wa Addis Ababa na abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo pamoja na wahudumu wake walifariki. Ripoti ya awali iliyotolewa na mamlaka nchini Ethiopia imeelekezea lawama waundaji wa ndege ya Boeing 737 Max.