Coronavirus: Tahadhari ya daktari aliyeamua kujitenga binafsi kuzuia maambukizi

Dkt. Ahmed Kalebi anasisitiza kuwa ni muhimu kwa yeyote ambaye anadalili zozote ambazo zinaambatana na dalili za corona virus zinazofanana sana na za mafua ajitenge Haki miliki ya picha Dkt. Ahmed Kalebi /Twitter
Image caption Dkt. Ahmed Kalebi anasisitiza kuwa ni muhimu kwa yeyote ambaye anadalili zozote ambazo zinaambatana na dalili za corona virus zinazofanana sana na za mafua ajitenge

Dkt. Ahmed Kalebi anasisitiza kuwa ni muhimu kwa yeyote ambaye anadalili zozote ambazo zinaambatana na dalili za corona virus zinazofanana sana na za mafua ajitenge

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya matibabu ya Lancet Afrika Mashariki Dkt. Ahmed Kalebi amejitenga na familia yake pamoja na umma wote kwa ujumla baada ya kubaini kuwa ana dalili za corona virus, ameiambia BBC Jumatano asubuhi.

Licha ya kwamba bado hajapimwa na kubaini kuwa ana maambukizi ya coronavirus, anasema amekua akisafiri na kupitia viwanja vya ndege, na hivyo badi ana uwezekano wa kuwa na virus vyacorona.

''Sijapata majibu ya vipimo vya hospitali lakini kwasababu nina dalili imebidi nijitenge binafsi nikingoja majibu'', anasema Dkt. Kalebi ambaye alikuwa akikohoa mara kwa mara wakati wa mahojiano.

Hata hivyo anasema kuwa watoto wake walikua na mafua tangu Ijumaa na mwanzo alihisi kuwa huenda walimuambukiza, na akadhani ni homa ya kawaida. Hata hivyo ilibidi achukue tahadhari kwasababu alikua amesafiri sana ndani ya nchi na katika nchi kama vile Rwanda ambako pia kuna visa vya coronavirus.

''Inabidi niwe na tahadhari, kwasababu virusi vya corona ina dalili kama za mafua ya kawaida inabidi nijitenge nyumbani, si kwamba nimepata lakini ni kuwa tu muangalifu'', amesema Dkt. Kalebi.

Haki miliki ya picha Dkr. Ahmed Kalebi/Twitter
Image caption Dkt. Ahmed Kalebi amefanyiwa kipimo cha Coronavirus anasema haijaingia akilini mwa watu wengi kuwa wanaweza kuwa na maambukizi ya coronavirus na kuwaambukiza watu wengine

Ushauri wa Dkt.Ahmed Kalebi.

  • Ni muhimu kwa yeyote ambaye anadalili zozote ambazo zinaambatana na dalili za corona virus ajitenge.
  • Dalili zinazoweza kuwa ni za corona ni kama vile mafua, kupanda kwa joto la mwili (homa), maumivu ya mwili, viungo, kuhara, na nyinginezo zinazotajwa na WHO
  • Ni vema mtu kama huyo ajitenge binafsi na familia na umma kwa ujumla kwa muda wa wiki mbili na uhakikishe umepimwa na kubainika kuwa umepona kabisa,na anawe mikono yake mara kwa mara.
  • Iwapo unalazimika kunatoka nje kwa shughuli kama vile biashara za kila siku....Unapaswa kuwa mita mbili au tatu kutoka kwa mtu mwingine yoyote yule na kuvalia barakoa wakati wote
  • Unapaswa pia kupimwa ili kufahamu ikiwa una virusi vya corona au la.
  • Dkt anasisitiza kuwa baada ya kupata virusi vya corona jambo la muhimu ni kusubiri mwili wako upone kwa njia ya kawaida yaani kwa kutumia kinga yako ya mwili yenyewe kwani ndio njia pekee ya tiba kwa sasa na kutowaambukiza wengine.

Dkt. Ahmed ambaye amekua akishughulikia mlipuko wa coronavirus, anasema suala zima la maambukizi ya coronavirus bado halijawaingia watu akilini nchini Kenya na kwingineko barani Afrika:

''Kwavile tumekua tukiskia corona kwa muda mrefu kwingine mfano Uchina, Iran, Italia, Ufaransa, lakini mpaka Juma lililopita watu walikua wakikejeli kuwa wakisema haiwapati Waafrika na mengine''

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Serikali ya Tanzania yafunga shule zote nchini kuzuia maambukizi ya virusi vya corona

Lakini tufahamu kuwa ugonjwa kama huo ukiingia inachukua muda kujidhihirisha vizuri, na huu ndio wakati wa kuuzuwia na hatua zilizochukuliwa na serikali kukabiliana na virusi zinapaswa kufuatwa'', anasema Dkt. Ahmed Kalebi.

Dkt. Kalebi anasema alichokigundua katika uzoefu wake wa hivi karibuni baada ya mlipuko wa coronavirus ni kwamba: ''Watu hawaoni ile tahadhari ya maambukizi, wanaona kuwa ni kitu kigeni kwa...juzi Ijumaa nilikua msikitini na watu wanakuja wanakohoa, wakaambiwa na wenzao rudi nyumbani...wanafahamu ipo, lakini haijawaingia akilini kwamba ni kitu ambacho wanacho na wanaweza kuwambukiza watu wengine'', anasema.

Anasema elimu juu ya virusi vya corona haijatolewa vya kutosha hasa nchini Kenya: ''Lazima tuwaelimishe watu juu ya maambukizi haya kama vile Rwanda ambako watu wameelimishwa kila mahali, na

kutoa tahadhari na kila jengo , kila ofisi, sokoni na kwenye vituo vya mabasi ya umma....watu wananawa mikono kila mahali'', anasema Dkt. Kalebi.

Unaweza pia kusoma: