Coronavirus: Vijana hawana uwezo wa ''kuiepuka', WHO yaonya

Vijana katika nchi nyingi wamekua wakipuuza tahadhari za kiafya zinazotolewa kuhusu coronavirus
Image caption Vijana katika nchi nyingi wamekua wakipuuza tahadhari za kiafya zinazotolewa kuhusu coronavirus

Vijana hawana kinga ya mwili dhidi ya coronavirus na wanapaswa kuepuka kuepuka mikusanyiko ya kijamii na kuwaelezea wazee na watu wengine wanaokabiliwa na hatari ya maambukizi juu ya virusi hivyo , limeonya shirika la Afya Duniani (WHO)

Chaguo lililofanywa na vijana linaweza kuwa "tofauti kati ya maisha na kifo cha mtu fulani", Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema.

Zaidi ya wagonjwa 11,000 yatari wamekwishafariki duniani kutokana na Covid-19 ambao ni ugonjwa unaoshambulia mfumo wa kupumua.

Kwa ujumla takriban wagonjwa 250,000 wamepatikana na virusi vya corona.

Image caption Mkuu wa WHO -Tedros Adhanom Ghebreyesus amewaambia vijana hawana uwezo wa kuepuka, virusi vinaweza kuwaweka hospitalini kwa wiki kadhaa au hata kuwaua

Tamko la Mkuu wa WHO linafuatia taarifa kuwa vijana katika nchi nyingi wamekua wakipuuza tahadhari za kiafya zinazotolewa kuhusu coronavirus katika nchi zao , kwasababu uapatikanaji wa virusi hivyoumekua ni miongoni mwa watu wenye umri mkubwa zaidi.

Milipuko wa coronavirus ulirekodiwa kwa mara ya kwanza nchini Uchina mwezi Disemba. Lakini kwa sasa kitovu cha janga hilo ni Ulaya.

Nchini Italia-ambako virusi vimewauwa watu zaidi ya nchi nyingine - idadi ya vifo imefikia hadi watu 627 siku ya Ijumaa, na hivyo kufikia jumla ya vifo 4,032, na kuifanya kuwa ndio siku ya vifo zaidi kuwahi kushuhudiwa katika nchi moja tangu mlipuko huo uanze

unaweza pia kusoma:

WHO imesema nini ?

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kupitia mtandao kutoka makao makuu ya WHO mjini Geneva, Bwana Tedros amesema: " Ingawa wazee ndio wanaoathiriwa vibaya na virusi, vijana sio salama."

Aliongeza kuwa: " Nina ujumbe kwa vijana : ' Hamuna uwezo wa kuepuka, virusi vinaweza kukuweka hospitalini kwa wiki kadhaa au hata kukuua. Hata kama hauugui chaguo lako la ni wapi unakotaka kwenda linaweza kuleta tofauti kati ya kifo na maisha kwa mtu mwingine'

Bwana Tedros amepongeza kupungua kwa visa vya voronavirus katika mji wa Uchina wa Wuhan-ulikoanzia mlipuko wa virusi hivyo, ambako siku ya Alhamisi hawakuwa na kisa hata kimoja cha coronavirus.

Image caption Vijana wengi duniani wanasemekana kuendelea kuponda raha katika sherehe zao bila kuchukua tahadhari ya coronavirus

Amesema hii imeleta''matumaini kwa maeneo mengine ya dunia kwamba hata hali mbaya zaidi inaweza kubadilishwa''

Tafiti zimeonyesha kuwa watu wa rika malimbali wanaweza kuathiriwa na virusi - lakini ni hatari zaidi hususan kwa wazee na wale wenye magonjwa ya kudumu.

Wastani wa watu wanaokufa kutokana na Covid-19 nchini Italia ni wate wenye umri wa miaka 78.5.

Wachache zaidi ya 1% ya wagonjwa wenye chini ya miaka 50 walikufa nchini Uchina , kwa mujibu wa gazeti la New York Times. Lakini uliwaua karibu ya 15% ya wale waliokua na umri wa zaidi ya miaka 80.

WHO sasa inapendekeza "watu wasikaribiane " badala ya "utengano wa kijamii" iki kusaidia kuzuwia maambukizi ya virus, limeripoti shirika la habari la Reuters.

"Tunataka watu waendelee kuwasiliana," amesema Dkt Maria Kerkhove, mtaalamu wa majonjwa yanatoambukizwa katika WHO.

" Kwa hiyo tafuta njia za kufanya hilo, tafuta njia kupitia intaneti na kwa njia ya mitandao ya kijamii ili kuendelea kuwasilianakwasababu afya yenu ya akili mnapopitia kipindi hiki cha janga ni muhimu tu sawa na afyya yenu ya mwili ," alisema.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii