Coronavirus: Mikakati mitano ambayo imethibitisha kudhibiti maambukizi ya Covid-19

A person in a mask wipes down a window Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu zaidi ya 350,000 wameambukizwa Coronavirus kote duniani na wengine zaidi ya 15,000 wamekufa kutokana na maambukizi hayo

Coronavirus imesambaa duniani, na hivyo kusababisha wasiwasi mkubwa katika maeneo yote ya sayari: maelfu ya visa vipya na maelfu ya vifo vinatangazwa kila siku.

Miji mingi na nchi zote - zinawaambia watu wakae nyumbani, na kusababisha kufutwa kwa safari za ndege , matukio ya kimataifa na matamasha ya mwaka.

Ulaya imekua ni kitovu kipya cha ugonjwa, huku - Marekani, Amerika Kusini, na mashariki ya kati -viwango vya maambukizi vikiendelea kuongezeka kila uchao.

Lakini baadhi ya nchi zinaonekana kudhibiti kasi ya usambaaji wa virusi, ambavyo hadi kufikia tarehe 23 Machi viliripotiwa kuwaua watu 15,000 na zaidi ya 340,000 walikua wameambukizwa kote duniani.

Nchi kadhaa za Asia , licha ya kuwa karibu zaidi na Uchina Kijiografia(ambako maambukizi yalianzia) zinaongoza katika kushusha chini kiwango cha maambukizi ya Covid-19.

"Kuna nchi ambazo zimeweza kuchuakua hatua kudhibiti mlipuko, ninadhani tunapaswa kujifunza kutoka kwao ," anasema Tolbert Nyenswah, Profesa na mtaalamu wa magonjwa ya milipuko katika Chuo Kikuu cha t Johns Hopkins University nchini Marekani, ameiambia BBC.

"Sizungumzii Uchina tu, ambako idadi ya visa vya maambukizi vilipungua baada ya uchukua hatua kubwa ambazo nchi nyingine za kidemokrasia zinaweza kuona sio rahisi kuzitekeleza ," alisema.

"Nchi nyingine zimefanikiwa kuchagua njia tofauti-lakini bado zenye ufanisi - kwa njia ya hatua ."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Japan imeweza kupunguza maambukizi ya coronavirus

Jirani na Uchina Taiwan, kwa mfano, yenye idadi ya watumilioni 23.6 imeripoti visa 195 tu vya coronavirus na vifo hadi kufikia tarehe 23 Machi.

Idadi ya wakazi wa Hong Kong ni milioni 7.5 na inapakana na Uchina lakini imethibitisha visa 155 ya maambukizi na vifo vinee katika kipindi cha zaidi ya miezi mwili ( ingawa visa viliongezeka tena wiki iliyopita, hatua nyingine zimechukuliwa)

Nchi jirani ya Japan, (ina wakazi miliani 120 ) imerekodi visa 1,100 vya maambukizi, huku Korea Kusini ikiripoti takriban wagonjwa 9,000, lakini viwango vya maambukizi vna vifo vimepungua katika miaka ya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Nyenswah, nchi hizi zimefanikiwa katika kudhibiti usambaaji wa virusi kwasababu walichukua hatua kwa haraka na kutumia sera mpya walizozibuni

Zifuatazo ni hatua zenye ufanisi zaidi:

1. Pima , pima na kupima tena

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption KUpima ni hatua ya kwanza ya kudhibiti janga la ugonjwa

Wataalamu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) na wataalamu walioulizwa na BBC wanaafiki kuwa utambuzi wa mapema ni suala la kimsingi katika kudhibiti kuenea kwa mlipuko.

"Huwezi kujua athari halisi za virusi au kuchukua hatua inayofaa kama hujui ni watu wangapi wameathiriwa," anasema Nyenswah.

Krys Johnson, Profesa wa magonjwa yanayoambukiza katika Chuo Kikuu cha Temple nchini Marekani anaafiki pia hilo.

Anasema hili ndilo kusemakweli lilileta utafauti katika kukabiliana na virusi: Mataifa ambayo yanategemea matokeo ya vipimo yameshuhudia visa vya maambukizi vikishu, huku kule ambako utekelezwaji wa vipimo haukuzingatiwa wameshuhudia idadi ya visa vya maambukizi ya coronavirus vikiongezeka kwa kasi kubwa.

" Korea Kusini imekua ikiwafanyia vipimo vya coronavirus watu 10,000 kwa siku, hii ikimaanisha wamekwishawapima watu zaidi katika kipindi cha siku mbili kuliko idadi nzima ya Wamarekani katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja " aliiambia BBC.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema kwamba kumpima kila mtu mwenye dalili ni "muhimu katika kuzuwia maambukizi"ya mlipuko wa ugonjwa.

"Tuna ujumbe rahisi kwa nchi zote - pima, pima, pima," alisema katika mkutano wa hivi karibu wa waandishi wa habari , "Nchi zote zinapaswa kuwa na uwezo wa kuwapima watu wote wanaoshukuiwa kuwa na virusi -hawawizi kupambana na janga hili bila kuelewa ni wangapi wana maambukizi ."

2. Kuwatenga waliopata virusi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kuwatenga wenye maambukizi au wanaoshukiwa kuwa na maambukizi- ni muhimu katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi (stock image)

" Korea Kusini na Uchina zimefanya kazi nzuri katika kuwatafuta, kuwapima na kuwadhibiti raia wake,"anasema Profesa Krys Johnson.

Vipimo havisaidii katika kuwatenga wagonjwa na kuzuwia kuenea kwa virusi tu bali kusaidia kubaini vinavyoweza kuwa visa vipya mapema.

Taiwan, Singapore na Hong Kong zilitumia njia tofauti: kutenga visa vinavyoshukuwa majumbani na kutangaza faini ya zaidi ya $3,000 kwa wale ambao watavunja sheria

3. Matayarisho na uingiliaji kati wa haraka

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Taiwan hadi sasa imefanikiwa katika kudhibiti maambukizi ya Covid-19

Nyenswah, ambaye awali alifanya kazi katika kuzuwia maambukizi ya Ebola Afrika Magharibi, anasema moja ya mambo ya kimsingi katika udhibiti wa virusi ni kuchukua hatua kwa haraka, kabla virusi havijaenea miongoni mwa watu.

"Nchi kama Taiwan na Singapore zimedhihirisha kwamba hatua ya haraka ya kubaini na kutenga visa vipya inaweza kuwa hatua yenye ufanisi katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona ," anasema.

"Kuwa tayari kuchukua hatua na kuzichukua haraka ni jambo muhimu katika hatua za mwanzo za mlipuko . Katika Ulaya na Marekani , tumeona kwamba si tu kwamba nchi hizo hazikua tayari, bali pia zilizorota kuchukua hatua ," anasema Nyenswah.

Hong Kong ilianza kutekeleza mpango wa kubaini vipimo vya joto vya watu na kuweka vituo vya utekelezwaji wa shughuli hiyo kwenye vituo vya kuingia kuanzia Januari 3, na kuwatenga watalii katika karantini kwa siku 14 , huku madaktari wakiagizwa kuripoti mgonjwa yeyote mwenye joto la juu la mwili au mwenye tatizo kubwa katika mfumo wake wa kupumua na mwenye historia ya kusafiri Wuhan ya karibuni.

Unaweza pia kusoma:

4. Kutokaribiana kwa watu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kutokaribiana kwa watu -ambako kunaonekana pichani katika bunge la Australia - husaidia kuzuwia maambukizi

" Pale ugonjwa unapokuwa tayari umeingia nchini mwako hatua za kuudhibiti zinakuaha hazina maana tena," anasema Nyenswah.

Kwa wakati huo, njia yenye ufanisi zaidi ya kuwalinda watu ni kutekeleza haraka hatua ya kutokaribiana kwa watu katika jamii - kama ilivyofanyika katika Hong Kong na Taiwan.

Hong Kong iliwambia watu kufanyakazi nyumbani, ikafunga shule na kufuta matukio yote ya kijamii mwishoni mwa mwezi wa Januari.

5. Kuhimiza hatua za usafi

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Katika nchi kama vile Singapore, vituo vya jeli za kuua bakteria vinaonekana kila mahali mitaani

WHO inasema kuwa kuosha mikono mara kwa mara na usafi wa kutosha ni muhimu katika kuepuka maambukizi.

"Nyingi kati ya nchi za Asia zilijifunza kutokana na uzoefu wa mlipuko wa SARS mnamo mwaka 2003. Mataifa haya yanafahamu kuwa usafi utawasaidia kuugua na kuwazuwia kuwaambukiza watu wengine ," anasema Nyenswah.

Katika nchi kama Singapore, Hong Kong, na Taiwan kuna vituo vya jeli za kuua bakteria kwenye mitaa na matumizi ya mara kwa mara ya barakoa.

Ingawa barakoa huenda zisiwe na ufanisi wakati wote katika kuzuwia mvaaji kupata ugonjwa,husaidia kupunguza hatari ya wagonjwa kusambaza virusi

kupitia kikohozi na kupiga chafya.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii