Coronavirus: Jinsi Covid-19 inavyozuia familia kuaga wapendwa wao Italia

"Tunaweka nguo ambazo familia ilitupatia juu ya maiti, kama wamevalishwa " Haki miliki ya picha JILLA DASTMALCHI
Image caption "Tunaweka nguo ambazo familia ilitupatia juu ya maiti, kama wamevalishwa "

Italia imepiga marufuku mazishi ya watu wanaofariki kutokana na janga la corona.

Kwa wengi virusi vya corona vimewanyima fursa ya kuwaaga wapendwa wao

"Janga hili linaua mara mbili," anasema Andrea Cerato, ambaye anafanya kazi katika hifadhi ya maiti mjini Milan. "Kwanza inakutenganisha na wapendwa wako kabla hujafariki. Kisha, inamzuia mtu yeyote kuuaga mwili wako baada ya kifo chako."

"Familia zimefadhaika na zinapata wakati mgumu kukubali."

'Hawana budi kutuamini'

Inchini Italia waathiriwa wa Covid-19 wanafarika katika hospitali ya kuwatenga wagonjwa bila kuwa na jamaa wala marafiki zao.

Hakuna ruhusa ya kuwatembelea kwa sababu hofu ya maambukizi iki juu sana.

Huku mamlaka za afya zikisema virusi hivyo haviweza kuambukizwa baada y a mgonjwa kufariki , bad vimelea vyake vinaweza kusalia kwa nguo kwa saa kadhaa.

Hii inamaanisha maiti inafungiwa moja kwa moja teary kuzikwa.

"Jamaa za marehemu wanauliza ikiwa wanaweza kuruhusiwa kumuona mpendwa wao kwa mara ya mwisho. Lakini ombi hilo limezuiliwa," anasema Massimo Mancastroppa, anayefanya kaziya kuzika watu mjini Cremona.

Taarifa zaidi kuhusu coronavirus:

Waliofariki hawawezikuzikwa kwa kuvishwa nguo nzuri. Badala yake wanavishwa nguo za hospitali ambazo hazivutii kabisa.

Lakini Massimo ianafanya kila awezalo kuvisha maiti nguo nadhifu.

"Tunatumia nguo tunazopewa na familia kufunika miili kana kwamba maiti imevishwa," anasema. "Shati juu na sketi kwa chini."

Haki miliki ya picha JILLA DASTMALCHI
Image caption "Hatuwezi kuwafanya wapendeze na wenye kuwa na amani. Inasikitisha sana."

Katikamazingira hayo magumu wazikaji ghafla wamejipata wakichukua nafasi ya familia, marafiki na wachungaii.

Watu wa karibu wa waathirika wanaofariki kutokana na virusi nao huwa wamejiweka karantini

"Tunawatekeleze majukumu yao," anasema Andrea. "Tunawatumia wapendwawao picha ya jeneza litakalotumiwa, tunachukua mwili kutoka hospitali na kuuzika au kuuchoma. Hawana budi kutuamini.

Changamoto kubwa kwa Andrea sio kushindwa kuwasaidia waliofiliwa bali ni kuzifahamisha familia kwa kuorodhesha vitu vyote ambavyo hasahili kufanya.

Analazimika kuandika orodha hiyo kila wakati mtu anapokufa.

"Hatuwezi kumvisha ngu, hatuwezi kumchana nywele ,hatuwezi kumpaka vipodozi. Hatuwezi kupendezesha maiti kabla ya safari yake ya mwisho duniani. Inasisikitisha sana."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ibada za mazishi zimepigwa marufuku nchini Italia kama sehemu ya hatua za dharura za kupambana na coronavirus

Andrea amekuwa akifanya kazi ya kuzika wafu kwa miak 30, sawa na baba yake alivyokuwa akifanya kabla yake.

Ni mambo madogo lakini ni muhimu kwa familia zilizofiliwa.

"Kumgusa mashavu kwa upole mara ya mwisho, kumshika mikono na kumwaga mpendwa wao kwa heshima ni jambo la maana sana. Kushindwa kufanya vyote hivi kunaumiza sana."

Wakati huu ambao kuna mlipuka wa virusi wazikaji wanalazimika kukutana na jamaa za marehemu upande wa pili au kupitia mlango uliofungwa .

Jamaa za marehemu wanajaribu kupitisha vijikaratasi vilivyoandikwa kwa mkono, vilivyo na ujumbe kwa marehemu ima iwe ni shairi ama au ujumbe wakusema watazikwa karibu na baba, ndugu, dada au binti sikuwakifariki.

Lakini vijikaratasi hivyo havitawekwa ndani ya jeneza.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Idadi ya vifo imekua nyingi kuliko uwezo wa sekta ya mazishi nchini Italia

Kubaki na vitu vya kibinafsi vya aliyefariki sasa ni hatia ni hatia. Hatua hiyo nikali lakini itasaidia kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huu hatari.

Ikiwa mtu atafariki nyumbani wazikaji bado wanaruhusiwa kuingilia shuguli ya mazishi wakiwa wamevalia mavazi rasmi: kama vile miwani, barakoa, glavu,koti na kadhalika ili mradi wamejikinga dhidi ya maambukizi.

Hali hiyo inawahuzunisha sana jamaa ambao wameashuhudia mpendwa wao akifariki muda mfupi uliopita.

Laki baadhi ya wazikaji pia wamejiweka karantini . Baadhi yao wamelazimika kufunga biashara zao.

Swali kuu sasa ni nani atakayefanya kazi ya kuzika waliofariki huku waliosalia wakiwa hawana vifaa vya kushughulikia maiti.

Huwezi kusikiliza tena
Coronavirus: Utajuaje kuwa umeathirika na virusi?

Unaweza pia kutazama:

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii