Coronavirus: Marufuku ya Museveni ya usafiri wa umma yaathiri uchumi Uganda

Biashara za maduka, usafiri na majumba ya kibiashara mjini Kampala vimefungwa
Image caption Biashara za maduka, usafiri na majumba ya kibiashara mjini Kampala vimefungwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza jana usiku marufuku ya usafiri wote wa umma kote nchini humo ili kuzuwia kusambaa kwa coronavirus.

Hii imeleta athari kubwa kwa mamilioni ya watu -na situ kwasababu inazuwia matembezi yao bali pia kwasababu inaathiri mapato ya baadhi ya watu wengi waliomo hatarini zaidi. Watu hawawezi kufika kazini au katika biashara zao, hii ikimaanisha kuwa hawana kipato cha cha kuwawezesha kuishi.

Wafanyakazi wa vibarua wanaopokea malipo ya kila siku kulingana na kazi wanayoifanya pia wanaumia . Masoko yameamrishwa kuuza bidhaa za chakula pekee.

Biashara za maduka, usafiri na majumba ya kibiashara mjini Kampala vimefungwa . Leo asubuhi video ilianza kusambaa ya vikosi vya usalama vikiutawanya umati wa wauzaji wa bidhaa na watu katikakati ya jiji la Kampala.

Polisi na wanajeshi wameshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi , ambapo walionekana wakiwapiga watu mitaani.

Waandishi wa habari wanasema kuwa ingawa maduka hayapaswi kufungwa kulingana na maagizo ya rais , vikosi vya usalama vimefunga biashara zote mjini Kampala isipokua maduka ya jumla na migahawa ya chakula.

Image caption Usafiri wa umma umepigwa marufuku Uganda

Polisi wamesema kuwa kufikia mchana watu 14 wamekamatwa baada ya kuiba

Mabasi madogo na yale makubwa yanayoelekea maeneo ya mashambani pamoja na magari moshi pia yamepigwa marufuku.Magari ya kibinafsi yanaweza kutumika lakini sasa yatalazimika kubeba watu watatu pekee akiwemo dereva.

Masoko nayo yatasalia wazi lakini yatakuwa yakiuza vyakula peke yake.

Huku bei ya baiskeli imepanda ghafla baada ya tangazo hilo.

Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuthibitisha visa vingine vitano vya ugonjwa wa coronavirus kikiwemo kisa cha mtoto mwenye umri wa miezi minane na hivyobasi kufanya visa hivyo katika taifa hilo kufikia idadi ya watu 14.

Wiki mbili zilizopita serikali ya Uganda ilizindua sera ya karantini ya lazima kwa wasafiri wanaowasili nchini humo kutoka mataifa 16 yaliyopo katika 'hatari zaidi' ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Uingereza, Marekani na nchi kadhaa za Ulaya ni miongoni mwa mataifa yatakayoathiriwa na sera hiyo mpya ya usafiri nchini Uganda.

Wiki iliyopita taifa hilo la Afrika Mashariki lilitangaza hatua kama hiyo dhidi ya mataifa saba.

Serikali pia ilisema kwamba wasafiri wanaowasili katika uwanja wa kimataifa wa Entebbe hivi karibuni watakuwa wakipuliziwa dawa.

Hatua ya kudhibiti wageni wanaowasili nchini Uganda kutoka mataifa yanayokabiliwa na ugonjwa huo inamaaninisha Covid-19 haitawaathiri watu wengi ikiwa mtu yeyote aliyeambukizwa atashughulikiwa ipasavyo.

Kwanini Uganda iliwafurusha raia 22 wa kigeni waliowasili kwa kongamano la kibiashara

Maafisa wa wizara ya afya nchini Uganda mnamo tarehe tisa mwezi Machi walisema kwamba takriban raia 22 wa kigeni waliriudishwa katika mataifa yao huku hofu ya maambukizi ya virusi vya corona ikiendelea.

Uganda ndio iliokuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa kuhusu biashara lililoanza nchini humo wiki tatu zilizopita.

Image caption Polisi na wanajeshi wameshutumiwa kutumia nguvu kupita kiasi , ambapo walionekana wakiwapiga watu mitaani

Image caption Kabla ya marufuku ya hivi karibuni usafiri wa bodaboda ulishamiri

Kwa mujibu wa waziri ya afya nchini humo raia hao walikataa kwenda karantini kwa siku 14 walipowasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe.

Aidha hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na dalili ama ishara za COVID19. "Tuliwaambia kuhusu hatua zetu za kujiweka katika karantini kwa siku 14 .

Hatahivyo hawakuwa tayari kufuata maagizo yetu .Hii leo watarudi nyumbani kwao'', waziri wa afya Dkt. Ruth Aceng alisema sikjuya Jumapili. ''

Hatua hiyo ya Uganda ilijiri saa chache tu baada ya mtalii kutoka Ujerumani kufariki kutokana na virusi vya corona katika eneo la kitalii la Sinai mashariki mwa Misri, ikiwa ndio kifo cha kwanza kurekodiwa Afrika.

Raia huyo wa Ujerumani aliyekuwa na mwenye umri wa miaka 60 alionyesha dalili za joto mwilini na kulazwa katika hospitali ya Hurghada tarehe 6 mwezi Machi , kabla ya kupatikana na ugonjwa huo , ilisema ripoti ya wizara ya afya.

Mtalii huyo aliyewasili kutoka Ujerumani wiki moja iliopita , alifariki baada ya kukataa kuhamishwa hadi katika eneo lililotengwa baada ya kuugua ugonjwa mbaya wa mapafu.

Siku ya Jumamosi , wizara ya afya ilitangaza kuhusu visa 45 vya raia wa Misri na wale wa mataifa ya kigeni waliodaiwa kuambukizwa virusi hivyo katika meli moja mto Nile.

Unaweza pia kutazama:

Huwezi kusikiliza tena
Namna sahihi ya kuosha mikono kuzuia Coronavirus

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii