Coronavirus: Kwa nini bei ya juisi ya machungwa katika soko la dunia imepanda?

Orange juice futures have shot up amid health concerns and demand for vitamin C.

Chanzo cha picha, Getty Images

Bei ya maji ya machungwa(Juisi) imepanda kwa zaidi ya asilimia 20 ndani ya mwezi huu ikiwa ni matokeo ya walaji kutafuta vyakula vyenye virutubisho vya kutosha wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

Wakati mahitaji yakizidi kuongezeka wazalishaji wanashindwa kukidhi mahitaji ya soko kutokana na vizuizi mbalimbali vya usafirishaji.

''Mlipiko huu wa Covid 19 una mahitaji na uzalishaji wa sharubati ya machungwa, virutubisho vya kuimarisha kinga ya mwili vinauhitaji mkubwa sana kwa sasa lakini tatizo hakuna nafasi ya kutosha katika makasha kukidhi mahitaji ya soko wakati huu ambao mashirika ya ndege yamesitisha safari zake

Kwenye usambazaji nako kuna changamoto mfano uhaba wa watumishi kutokana na mashamba kuweka marufuku ya mikusanyiko na kuagiza watu kujitenga.

Wazalishaji wa juisi za machungwa wamepata faida kubwa zaidi kwa mwezi tangu mwaka 2015 wakati ambapo masoko dunia yametikiswa , mjini London takwimu za FTSE 100 ziliporomoka kwa zaidi ya asilimia 13 kwa mwezi uliopita.

Wakati haya yakijiri wengi wanajiuliza iwapo kupanda huku kwa bei ya juisi za machungwa kwa sasa kutasababisha bei kuendelea kupanda kwa siku zijazo , Bwana Innes anasema : "Athari za mfumuko huu wa bei huenda zikaonekana haraka sababu wazalishaji tayari wameshaidhinisha ongezeko la bei hivyo punde katika msoko na maduka nako zitapanda"

Sasa bidhaa ya kawaida zina bei ya mbeleni ambayo inaweza tumika katika biashara kimataifa, mikataba ya mbeleni inaweza kuwasaidia wazalishaji kuweka bei elekezi inayoweza kuwakinga na kupanda kwa bei.

Mikataba ya mbeleni ni ya kawaida kwa bidhaa laini kama machungwa na ngano ambayo yako hatarini na kupanda huku kwa ghafla kutokana na mavuno mabaya na majanga asilia.

.