Coronavirus: Ni kwanini watu katika baadhi ya mataifa wanatumia barakoa huku mengine hawatumii?

A man in China wearing a mask

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Watu kuvalia barakoa ni jambo ambalo limekua la kawaida katika nchi nyingi za Asia, ikiwemo Uchina

Ukitoka nje ya nyumba Hongokong au Tokyo, au Seoul ziku hizi bila kuvaa barakoa watu watakuangalia vibaya.

Tangu kuanza kwa mlipuko wa coronavirus baadhi yamaeneo yamekuwa yakitilia mkazo uvaaji wa barakoa, na yeyote anayeptikana hajavaa anaweza kujipata katika hatari ya kutengwa na jamii.

Lakini katika maeneo mengine ya dunia, kuanzia Uingereza na Marekani hadi Sydney na Singapore, inakubalika kabisa kutembea bila barakoa

Kwanini baadhi ya nchi zina utamaduni ya kuvaa barakoa huku hata sio kwasababu ya maagizo kutoka kwa serikali au hata ya kimatibabu ni kwasababu inatokana na utamaduni na historia. Lakini wakati janga hili linapokua baya zaidi, je hii itabadilika ?

Maelezo rasmi juu ya uvaaji wa barakoa

Tangu mwanzo wa mlipuko wa coronavirus, ushauri rasmi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) umekua wazi. Ni watu wa aina mbili tu wanaopaswa kuvaa barakoa: wale wanaoumwa na kuonyesha dalili, na wale wanaowahudumia watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Hakuna mtu mwingine anayehitaji kuvaa barakoa na kuna sababu kadhaa za kufanya hivyo.

Moja ya sababu hizo ni kwamba barakoa haijaonekana kuwa njia ya kuaminika ya kujikinga na maambukizi, ikizingatiwa kuwa utahiti wa hivi karibuni inaonyesha kuwa virusi husambazwa kwa matone ya mafua na sio kwa njia ya hewa. Hii ndio maana wataalamu wanasema kunawa mikono mara kwa marakwa sabuni na maji ni njia yenye ufanisi zaidi katika kujilinda na maambukizi ya coronavirus.

Kuondoa barakoa zote kunahitaji kufanywa kwa uangalifu zaidi ili kuepuka mikono iliyoa na virusi kugusa sehemu ya uso.

Katika maeneo ya bara ya Uchina, Hong Kong, Japan, Thailand na Taiwan, mtatazmo wa jumla ni kwamba kila mtu anaweza kuwa ana maambukizi ya virusi, hata watu wenye afya . Kwa hiyo katika moyo wa ushirikikiano, unahitaji kuwakinga wengine na ugonjwa wako.

Baadhi ya serikali hizi zinamtaka kila mtu kuvaa barakoa, na katika baadhi ya sehemu za Uchina, unaweza hata kukamatwa na kuadhibiwa usipoivaa.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Katika miji ya Wuhan na Guangzhou, maafisa wa Uchina wamesema kuwa wale ambao hawavai barakoa wanaweza

Kwa nchi hizi nyingi, uvaaji wa barakoa ulikua ni utamaduni hata kabla ya mlipuko wa coronavirus. Hata zimekua ni kama sehemu ya fasheni - Wakati mmoja barakoa za kampuni ya Hello Kitty zilikua zinauzwa katika masoko ya mitani ya Hong Kong.

Katika Asia Mashariki, watu wengi wamezowea kuvaa barakoa wakati wanapokua wagonjwa au wakati wa msimu wa mafua, kwasababu kukohoa au kupiga chafya mbele ya watu bila barakoa ni jambo la kutokua na heshima. Mwaka 2003 mlipuko wa virusi vya Sars, ambao uliziathiri nchi kadhaa katika kanda hiyo, pia ulisaidia kufikisha ujumbe juu ya umuhimu wa kuvaa barakoa, hususan katika Hong Kong, ambako wengi walikufa kutokna na virusi hivyo.

Kwahivyo moja ya tofauti kuu ya jamii hizi na zile la Magharibi ni kwamba walikabiliwa na janga aina hiyo kabla- na bado wanakumbukumbu ya yaliyowatolea na inawasikitisha.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Katika mji wa Hong Kong, unaweza kununua mitindo tofauti ya barakoa

Wakati huohuo yakijiri,Kusini mashariki mwa Asia ,hususan katika miji iliyo na msongangamano, watu wengi huvalia barakoa kwasababu ya kijikinga kutokana na mazingira chafu.

Baadhi yao wanasema kuvalia barakoa kunawakumbusha watu kuhusu hatari ya virusi na hata kuachangia watu kubadili tabia kwa kuzingatia usafi kwa jumla.

Taarifa zaidi kuhusu ya coronavirus:

"Kuvalia barakoa kila siku kabla ya kutoka ndani ya nyumba imekuwa desturi kama vile kuvalia sare hali ambayo inakufanya uhisi umuhimu wa kufikia viwango vinavyohitajika vya usafi,kama vile kutogusa uso wako au kuenda sehemu uliyo na mkusanyiko wa watu." Anasema Donald Low, mtaalamu wa sosholojia ya watu na profesa wa Chuo Kikuu Hong Kong cha Sayansi na Teknolojia.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Je kuvaa barkoa inaweza kuwa kitu cha kukukumbusha binafsi na wengine kuzingatia usafi zaidi?

Halafu kuna dhana kwamba juhudi madhubuti hazijachukuliwa kukabiliana na virusi vya corona.

"Hatuwezi kusema barakoa hazisaidii na kwamba tunahoji utumizi wakati tunawapatia wahudumu wa afya kama sehemu ya kinga dhidi ya maambukizi," anasema Benjamin Cowling, mwanaepidemolojia katika (epidemiologist) katika Chuo Kikuu cha Hong Kong.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waziri mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha alionekana hivi karibuni akiwa amevaa barakoa inayofanana na koti lake

"Ikiwa barakoa inatumiwa na watu wengi katika maeneo yalio na msongamano wa watu ,nadhani itadhibiti viwango vya maambukizi, wakati huu tunajizatiti kufanya kila juhudi kupunguza maambukizi - inasaidia."Lakini hatua hiyo inakabiliwa na changamoto zake bila shaka. Mataifa kama vile Japan, Indonesia na Thailand ayanakabiliwa na uhaba wa bidhaa hiyo mu himu huku Kurea Kusini ikilazimika kuitoa kwa mgao.

Kuna hofu kwamba watu huenda wakarudia kutumia barakoa zaidi ya mara moja - hali ambayo sio salama. Kilichobakia ni kutumia barakoa zinazouzwa mtaani kimagendo , amakuvalia ile ya kujitengenezea nyumbani ambayo huenda isiifikie viwango vilivyowekwa.Watu wasiovalia barakoa katika maeneo haya pia wanakabiliwa na unyanyapaa na kuzuiliwa kuingia madukani au hata majengo.Mjini Hong Kong, magazeti yamechapisha picha za watu ambao hawajavalia barakoa waliokusanyika kwa makundi katika maeneo ya burudani huku yakiwalaumu wahamiaji na watalii kwa kutochukua tahadhari ya kijikinga na maambukizi ya virusi.