Virusi vya corona: Wafanyakazi wa kipato cha chini Kenya kama Esther wahofia

Visa vya ugonjwa wa corona vimefika 25 nchini Kenya na wengi wanahofia

kuwa huenda kukawa na lockdown ilikupunguza kuenea kwa virusi hivyo. Hatahivyo, huku serikali ikiweka mikakati kupunguza visa hivyo, wengi wanaoathirika ni wafanyakazi wa kiwango cha chini. Yaya kwa jina Esther anayesema kuwa kazi hazipatikani kutokana na hofu walionayo Wakenya wengi juu ya coronavirus.