Coronavirus: Je, unawatambua watu walio hatarini kuambukizwa virusi vya corona?

Watu wenye umri mkubwa wapo hatarini zaidi kuambulkizwa virusi vya corona Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu wenye umri mkubwa wapo hatarini zaidi kuambulkizwa virusi vya corona

Virusi vya corona vinaweza kumuathiri mtu yeyote, lakini watu wenye maradhi fulani pamoja na wazee wapo hatarini zaidi kuambukizwa ugonjwa huo.

Iwapo umekuwa ukiugua kwa muda mrefu unaweza kutishiwa na habari hii. Lakini je ni nani aliye katika hatari ya kuambukizwa?

Wengi wa wale walio katika hatari ya maambukizi ni watu wenye umri wa miaka 70 kwenda mbele, wale wenye maradhi ya ubongo na watu walio chini ya umri wa miaka 70 iwapo wanakabiliwa na dalili zifuatazo.

  • Magonjwa ya mapafu kama vile pumu, uchungu mkali kifuani , kushindwa kupumua na kuwa na homa kali.
  • Magonjwa ya moyo, ikiwemo mshtuko wa moyo
  • Maradhi ya figo
  • Maradhi ya ini
  • Shinikizo la akili
  • Kisukari
  • Maradhi ya utumbo kwa mfano anapofanyiwa
  • Magonjwa yanayoathiri kinga kama vile virusi vya ukimwi na saratani
  • Waraibu wa dawa za kulevya
  • Wanawake wajawazito

Watu wameshauriwa kujilinda dhidi ya coronavirus ili kukabiliana na hatari ya maambukizi yake na kuenea kwake.

Ninaugua Pumu nifanyeje?

Mamlaka ya afya nchini Uingereza imewashauri watu wenye pumu kutumia inhaler mara kwa mara, kama kawaida.

Hii itasaidia kuzuia uwezekano wa mtu kukutwa na tatizo la kupumua linalosababishwa na virusi kama vile vya corona.

Mtu anapaswa kuhakikisha kuwa inhaler yake ipo karibu naye kila siku hata iwapo hana dalili za pumu.

Iwapo Pumu imekuja na makali na umegundua kwamba umeathirika na maambukizi ya virusi vya corona wasiliana na maafisa wa afya.

Haki miliki ya picha Getty Images

Mimi ni mzee je niko hatarini kuangamia?

Ushauri unaotoka kwa daktari hadi kwa umma bila kutilia maanani umri - ni kuwa mbali na watu wengine ili kuzuia maambukizi.

Hii ina maana kwamba mtu hafai kwenda katika maeneo yenye watu wengi ili kujumuika nao.

Hii hususan ni muhimu kwa wale wenye umri wa miaka 70 kwenda juu pamoja na watu wenye maradhi kwa kuwa wako hatarini kuambukiuzwa.

Je nifanye nini iwapo ninaugua ugonjwa hatari?

Mtu yeyote ambaye yuko Katika hatari ya kuambukizwa maambukizi kama yale ya homa ya kawaida inayosababisha joto mwilini wanapaswa kuchukua tahadhari dhidi ya mambukizi.

Watu wanaoonyesha dalili za maambukizi - kama wale wanaokohoa au wenye Flu , wanapaswa kusalia majumbani.

Iwapo dalili zimekwisha na mtu hajapona anapaswa kumuona daktari.

Nina ugonjwa wa kisukari nifanyeje?

Watu wenye aina ya kwanza na ya pili ya kisukari wako katika hatari kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Dan Howarth , mkuu wa kituo cha ugonjwa wa kisukari nchini Uingereza alisema kwamba Covid-19 inaweza kupunguza kasi ya kisukari.

Iwapo unaugua kisukari na unaona dalili kama vile kukohoa na joto jingi mwilini pamoja na kushindwa kupumua unafaa kupima hali yako mara kwa mara.

Iwapo una dalili kama hizo unapaswa kusalia nyumbani kwa siku saba, na kuendelea kutumia dawa . Usiende hospitali.

Unapokosa kuona dalili za virusi vya corona na unataka kumuona daktari unapaswa kumpigia simu ama kuwasiliana naye kwa kutumia mtandao badala ya kwenda kumuona ana kwa ana.

Je wanawake wajawazito wanapaswa kuwa na wasiwasi?

Hakuna ushahidi kwamba wanawake wajawazito na wanawao wapo katika hatari ya maambukizi ya virusi vya corona lakini serikali zimewaomba kuchukua tahadhari ya afya yao.

Kama watu wengine wajawazito wanapaswa kuchukua tahadhari ili kuzuia maambukizi.

Wameorodheshwa katika orodha ya watu walio katika hatari ya kupata maambukizi, kulingana na maafisa wa afya.

Maafisa wa afya ya wanawake wanatoa ushari ufuatao:

1. Iwapo wewe ni mjamzito kwa chini ya wiki 28 na hauugui ugonjwa wowote unapaswa kukaa mbali na umma lakini unaweza kuendelea kufanya kazi huku ukichukua tahadhari dhidi ya watu wenye maambukizi kwa kutumia vifaa vinavyokulinda.

2. Iwapo una ujauzito wa zaidi ya wiki 28 ama una ugonjwa kama vile figo , au ugonjwa wa mapafu unapaswa kutokaribiana na watu walioambukizwa virusi vya corona.