Coronavirus: Marekani yaipiku Italia na China katika kesi za maambukizi ya corona duniani

First responders evacuate sick crew members with flu-like symptoms from two cruise ships in Miami Haki miliki ya picha Reuters

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

Idadi kubwa ya maambuizi imekujwa wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.

Marekani imepokeaje taarifa hizi?

Rais Trump alieleza namna alivyosikitishwa na idadi ya maambukizi.

Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona virus vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.

Bwana Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawafahamu idadi ya maambukizi yaiyopo China, "Hamfahamu takwimu ya maambukizi yaliyopo China."

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

Idadi kubwa ya maambuizi imekujwa wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.

Je, rais Trump ana matumaini ya kuendelea na mazuio aliyoweka dhidi ya mataifa mengine

Bwana Trump alikuwa amekosolewa kwa taratibu alizoweka mpaka ifikapo sikukuu ya Pasaka, April 12.

Mipango yake inaonekana kupiga mwamba baada ya siku ya Alhamisi , maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kuonekana kusambaa kwa kasi nchini mwake.

Siku ya Alhamisi alitangaza kuwa Wamarekani inabidi warejee kazini , nchi inabidi irejee katika hali yake ya kawaida mapema iwezekanavyo.

"Tunaweza kuchagua upande ambao hauna maambukizi sana na kuanza kuwajibika."

Aliongeza: "Watu wengi niliposema mrejee katika shughuli zenu, mlinieewa vibaya- naona waliachana na suala la kuwa mbali, kuosha mikono, kushikana mikono na kila kitu ambazo kilizuiwa.

Ufafanuzi zaidi alihaidi kutoa wiki ijayo.

Katika barua iliyotumwa na gavana , bwana Trump alisema timu yake imepanga kutoa muongozo wa watu kutokuwa karibu na kushauri baadhi ya miji kupunguza makazo.

Katika mapambano dhidi ya maambukizi ya corona, rais Trump aliweka katazo kwa baadhi ya nchi kuingia katika taifa lake.

Je, amri ya rais inaweza kumrudisha kila mtu kazini?

Hapana, wakati ambao rais alitoa agizo hilo maambukizi yalikuwa kidogo, ilikuwa Machi 16.

Katiba ya Marekani iko wazi kabisa kuwa inajali uslama wa mtu na vilevile maelekezo ambayo yalitolewa yanadiwa kuwayalikuwa yanampa mtu nafasi ya kuchagua au kuacha na haikuwa lazima.

Mada zinazohusiana