Coronavirus: Afrika kusini kufungwa wiki tatu

afrika kusini Haki miliki ya picha Getty Images

Afrika kusini imetangaza vifo viwili vilivyotokana na maambukizi ya virusi vya corona wakati taifa hilo likianza kutelekeza marufu ya kutoka nje huku nchi hiyo ikiwa na maambukizi zaidi ya 1,000.

Jeshi la ulinzi na usalama la Afrika kusini limeanza leo kuhimiza utekelezwaji wa marufuku ya kutoka nje ikiwa ni hatua ya kupambana na kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Corona.

Mapema kabla ya kuanza kutekelezwa kwa agizo hilo foleni ndefu ya watu ilionekana kwenye maduka makubwa wakifanya manunuzi muhimu ili kujiwekea akiba wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.

Afrika kusini imeripoti kuwa na wagonjwa ya 1,000 ikiwa ni idadi kubwa zaidi barani Afrika.

Jioni siku ya Alhamisi rais Cyril Ramaphosa alitembelea kambi ya jeshi kabla askari hao kuruhusiwa kuingia barabarani,

''Nina watuma kwenda kuwalinda watu wetu na virusi vya Corona,"Aliyasema hayo akiwa amevalia sare za jeshi.

Haki miliki ya picha EPA

''Ni wakati mbaya kwa demokrasia yetu, lakini pia kwa historia ya taifa letu kwamba tutaifunga nchi yetu kwa siku 21 ili kupambana na adui asiyeonekana, virusi vya corona"

Maduka ya vyakula hayatafungwa ingawa maduka ya vilevi yamepigwa marufuku wakati huu wa siku 21 Waziri wa Polisi Bheki Cel amewataka raia wa Afrika kusini kuwa timamu bila vileo wakati huu wa marufuku ya kutoka nje.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Afrika kusini kusitisha mauzo ya pombe

Siku ya alhamisi kuliripotiwa misururu mirefu ya magari kwenye barabara kuu ya kutoka Johannesburg, licha ya agizo la serikali la kuwataka watu wasiende safari ndefu.

Maelfu walifurika kwenye vituo vya mabasi wakikusudia kutoroka mjini na kwenda kukaa na familia vijijini jambo ambalo linazua hofu kwamba huenda baadhi wakaenda kuwaambukiza jamaa zao vijiji hasa wazee.

Haki miliki ya picha AFP

Serikali imesema yoyote atakaye kaidi agizo hilo atatumikia kifungo cha miezi sita kama adhabu ama faini kali.

"Kama watu hawakubaliani na maelekezo wanaweza (wanajeshi) kulazimika kuchukua hatua kali zaidi" alisema waziri wa ulinzi Nosiviwe Mapisa -Nqakula.

Afrika ya kusini tayari ilikuwa imefunga shule na kupiga marufuku mikusanyiko ya zaidi ya watu 100.

Ijapokuwa Afrika kwa ujumla haija athirika kwa kiwango kikibwa kama sehemu nyingine za dunia ijapokuwa wataalamu wanahofia mifumo dhaifu ya Afya barani humo kama itaweza kukabiliana na maambukizi kasi ikiongezeka.

Afrika kusini kuna hofu ya ziada kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi hasa watu takribani 2.5 nchini humo ambao hawatumii dawa za kufubaza virusi hivyo.

Mada zinazohusiana