Virusi vya corona: Je mataifa ya Afrika yanakabiliana vipi na athari za kiuchumi za Corona?

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ametangaza kuwa serikali yake italipia bili ya maji ya raia kwa kipindi cha miezi mitatu

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ametangaza kuwa serikali yake italipia garama ya maji ya raia kwa kipindi cha miezi mitatu

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo ametangaza kuwa serikali yake italipia garama ya maji kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ikiwa ni jitihada za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Wafanyakazi wote wa afya hawata katwa kodi katika kipindi cha miezi hiyo mitatu.

Kuosha mikono kwa sabuni na maji, Maji yanatajwa kuwa namna nzuri ya kukabiliana na maambukizi.

Wagonjwa 214 wamethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Corona na watu watano tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

Wiki iliyopita, Ghana iliweka amri ya kutotoka nje kwa muda wa wiki mbili katika miji ya Accra, Tema na Kumasi - ikifungwa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Kupitia matangazo ya televisheni rais Akufo-Addo alisema serikali kuwa kampuni zote zinazosambaza maji na umeme kwa uhakika na yeyote asikatiwe huduma hizo.

Matenki ya maji pia yatakuepo kutoa huduma ya maji kwa wananchi wasio na uwezo.

Kwa sasa wafanyakazi wa afya wanao wahudumidia wagonjwa wa Covid-19 wataongezewa mshahara kwa asilimia hamsini.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC)

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) watatoa huduma bure ya umeme na maji nchi nzima kwa kipindi cha miezi miwili ijayo.

"Hatua hizo zimechukuliwa ili kuhakikisha kuwa gharama za maisha za watu zimepungua katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ," Naibu waziri wa maji bwana Papy Pungu alieleza.

Maelezo ya picha,

Serikali ya rais Felix Tchiseketi imetoa agizo la kutoa maji na umeme bure kwa raia kwa kipindi cha miezi 3 ili kusaidia kukabiliana na athari za kiuchumi za virusi vya corona

Shirika la maji na shirika la umeme yamethibitisha kufuata agizo la serikali kwa kutoa huduma ya maji bure pamoja na umeme kwa kipindi cha miezi miwili.

"Tutafanya kila tuwezalo ili kiuhakikisha kuwa umeme na maji unatolewa bure kwa sababu serikali imehaidi kugharamia huduma," alisema mkurugenzi Shirika la maji bwana Clement Mubiayi.

Naye mkurugenzi wa shirika la umeme bwana Jean-Bosco Kayombo, alisema kuwa watakaofaidika na huduma hiyo ya umeme na maji bure, ni nyumba za watu na wafanyabiashara wadogo na wenye viwanda vya wastani ili kupunguza uwezekano wa maambukizi kuenea zaidi.

Serikali ya Kongo imesema kuwa imeamua kuchukua hatua hiyo kwa sababu watu hawaendi kazini kwa sasa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Kenya

Wakati nchini Kenya, benki za kibiashara zimetakiwa kutoa punguzo kwa wateja wao wa mikopo binafsi na kuwaongezea muda wa mwaka mmoja.

Chanzo cha picha, Patric Njoroge/Twitter

Maelezo ya picha,

Gavana wa benki kuu ya Kenya Patric Njoroge ametaka mikopo ya ujenzi kutolewa kwa wastani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya corona

Gavana wa benki kuu Kenya, bwana Patrick Njoroge anasema kuwa wataweka mikakati ya kuimarisha uchumi katika kipindi hiki cha athari za kiuchumi ambazo zinawakumba wateja wao kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Katika harakati za kuokoa uchumi binafsi, bwana Njoroge ametaka mikopo ya ujenzi kutolewa kwa wastani.

"Watu waliochukua mikopo binafsi, baadhi ya watu watapoteza ajira zao kutokana na mlipuko wa ugonjwa huu hivyo wanaweza wakawa hawana fedha za kurudisha marejesho ya mikopo yao hivyo inabidi waongezewe muda.

Vilevile rais pamoja na makamu wake, wametaka mishahara yao kwa mwezi huu ikatwe kwa asilimia ishirini.

Uganda na Rwanda wanatoa huduma ya chakula kwa raia wenye uwezo wa chini.

Maelezo ya video,

Ni lini Chanjo ya corona itapatikana?

Unaweza pia kutazama: