Virusi vya corona: Serikali yatangaza visa 7 zaidi vya maambukizi Kenya

Mercy Mwangangi

Chanzo cha picha, Ministry of health Kenya/Twitter

Maelezo ya picha,

Katibu wa kudumu katika wizara ya Afya Mercy Mwangangi amezitaka saloni kuhakikisha kuwa wahudumu na wateja kuzingatia maagizo ya kuepuka maambukizi ya virusi vya corona

Kenya imetangaza visa 7 zaidi vya maambukizi ya corona, idadi hiyo ikifanya idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini humo kuwa 179.

Akitoa taarifa kuhusu visa hivyo na maendeleo ya ugonjwa wa corona nchini humo, Katibu wa kudumu katika wizara ya Afya Mercy Mwangangi amezitaka saloni kuhakikisha kuwa wahudumu na wateja wanavaa barakoa na kuheshimu maagizo ya kukaa umbali wa mita moja kutoka kwa mtu mwingine.

Wiki hii wizara ya afya ilieleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.

Aidha, ndege kutoka nchi za kigeni zimeendelea kipigwa marufuku kuingia Kenya kwa siku 30 zaidi.

Hatahivyo, marufuku hii imeondolewa kwa ndege za kigeni zinazokuja kuhamisha raia wa nchi za nje waliokwama ingawa zinatakiwa kutoa taarifa kwa serikali angalau saa 72 kabla.

Ndege zingine ambazo hazitaathirika na marufuku hii ni zile za kubeba mizogo hasa ikizingatiwa kwamba kwa sasa serikali inaagiza vifaa vya wahudumu wa afya kutoka nje.

Sekta ya uchukuzi pia imeagizwa kutekeleza sheria zilizotolewa.

Na kutokana na ongezeko hilo, kuanzia Jumatatu, matatu au daladala pamoja na bodaboda ambazo zitakiuka sheria zilizowekwa zitapokonywa leseni na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kusambaza virusi kimaksudi.

Hatua zilizotangazwa na serikali ya Kenya kudhibiti coronavirus hivi karibuni

Wiki hii rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitangaza hatua kadhaa ambazo zitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanziasa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

Maelezo ya picha,

Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020

''Orodha kamili ya watu wanaotoa huduma muhimu ambao hawatathiriwa na amri hio itatolewa na wizara ya ya usalamma wa ndani'' alisema rais Kenyatta.

Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020.

Rais ametangaza hatua ya kupunguza mshahara wake kwa asilimia 80 huku mawaziri wake wakipunguza mshahara wao kwa asilimia 30.

Rais na naibu wa rais wamekubali kupunguza asilimia 80 ya mishahara yao kwa hiari huku mawaziri na makatibu wa kudumu wakikubali kupunguziwa asilimia 30 ya mshahara wao kwa asilimia 30.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Wakenya watashuhudia kupungua kwa ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020.

Uhuru alitoa wito kwa asasi nyingine za serikali kufuata nyayo kwa kupunguza kwa hiari mishahara yao wakati huu taifa linapokabiliana na janga la coronavirus.

Wafanyakazi wote wa serikali walio na umri wa miaka 50 na zaidi wataruhusiwa kuchukua likizo au kufanya kazi kutoka nyumbani.

Pia alitangaza kutolewa kwa dola milioni mia moja kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiojiweza, mkiwemo wazee na yatima.

Amesema ameamrisha watu wawanaolipwa mshahara wa dola 240 kwa mwezi wasitozwe ushuru.

Huku wale wanaolipwa shahara zaidi ya mshahara huo wakipunguziwa ushuru kwa asilimi tano.

Mabadiliko hayo ya kiuchumi yataanza kutekelezwa Aprili tarehe moja baada ya kuidhinishwa na bunge.

Bwana Kenyatta amesema hatua hizo zimechukuliwa kutokana na mienendo ambayo haizingatii hatua zilizochukuliwa za kukabiliana na coronavirus na akaonya kuwa hatua nyingine zaidi zitachukuliwa kulingana na mienendo yao.

Hatua zilizochukuliwa hivi karibuni kudhibiti coronavirus

Tangu Siku ya Jumapili hatua za dharura zilizochukuliwa ni pamoja na kufungwa kwa baa zote na wenye hoteli kuruhusiwa tu kuuza chakula cha kwenda kula nyumbani.

Ibada za Kanisa na Swala za pamoja Misikitini zimesitishwa huku mazishi ya kiruhusiwa kuhudhuriwa na familia ya marehemu pekee.

Sherehe za harusi pia zimepigwa marufuku.

Masharti mengine ya kuzuia maambukizi Kenya

  • Ndege za kimataifa zitasitishwa kuanzia Jumatano Machi 25 ispokuwa ile ya kubeba mizigo
  • Wageni wote wanaongia nchini kutoka mataifa yaliyoathiriwa watalazimika kujitenga binaffsi kwa gharama zao.
  • Wakenya katika mataifa ya kigeni wametakiwa kufuata muongozo wa nchi husika
  • Atakayekiuka maagizo ya karantini atakamatwa kama iafisa wa ngazi ya juu wa serikali aliyetiwa mbaroni pwani ya Kenya.

Huku hayo yakijiri serikali imetangaza kuwa itamfikisha mahakamani naibu wa gavana wa jimbo la Kilifi pwani ya Kenya kwa kukaidi maagizo ya kujiweka karantini binafsi baada ya kuwasili nchini wiki iliyopita. Kwa sasa anazuiliwa katika kituo cha serikali cha kuwatenga watu walio na ugonjwa wa corona.

Unaweza pia kutazama: