Virusi vya corona: Je unasherehekea vipi, Pasaka au Ramadhan bila ya kukaribiana?

Togo Ibada ya jumapili ya kanisa katoliki mjini Lome Togo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Togo Ibada ya jumapili ya kanisa katoliki mjini Lome Togo

Kwa wakristo wengi na wayahudi, huu ni wakati muhimu sana, katika mwaka.

Ni wakati ambao wanajiandaa kusheherekea sikukuu ya Pasaka na ufufuko wa Yesu na Waislamu nao wakiwa wanajiandaa kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Imani zote tatu, kwa kawaida wakati huwa unawajumuisha watu katika mlo wa pamoja na sala.

Lakini hali ni tofauti kwa sasa, mataifa mengi yanataka watu wasikaribiane na hivyo sherehe ambazo zimezoeleka kuwa ngumu kufanyika.

Maadhimisho ya juma kuu la kukumbuka ukombozi wao unaanza jioni ya Aprili 08, Sherehe hizo ni muhimu sana kwa kalenda ya Wayahudi.

Wanakumbuka simulizi ya kitabu cha kutoka na kipindi ambacho Wayahudi wanakumbuka jinsi Musa alivyowatoa mababu zao kwenye utumwa Misri.

Jioni ya kwanza ya Pasaka , chakula maalum na ibada maalum inayofanyika katika nyumba za watu.

Baadhi ya wayahudi ambao wanaishi nje ya Israel huwa wanaadhimisha jioni ya siku inayofuata.

Huwa wanasheherekea 'Seder' ambayo watu huwa wanasoma, wanasimuliana simulizi mbalimbali, wanakula chakula maalumu na kuimba.

Haya yote huwa yanafanyika wakati ambao familia na marafiki wamejumuika kwa pamoja wakiwa wameizunguka meza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

familia ya kiyahudi ikisherehekea pasaka

Tafrija hii huwa ni tamasha linalojumuisha watu kusheherekea uhuru na maisha. Sherehe hizi za Seder huwa zinahitaji watu wengi kusheherekea na sio familia peke yake.

Lakini kutokana na makatazo ya virusi vya corona, mwaka huu sherehe hizi za Seder zitakuwa tofauti sana.

Rabbi Rick Jacobs anaishi mjini New York, ambako sasa maambukizi ni mengi zaidi nchini Marekani.

Yeye ni rais wa Umoja wa wayahudi Marekani

Rabbi Jacobs anawashauri jinsi wanavyoweza kuungana kwa pamoja kusheherekea Pasaka ya mwaka huu.

Suluhisho moja alilosema ni kutumia simu ya video.

Ujumbe wa dini utawekwa mtandaoni ili kila mmoja atajumuika kusoma.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chakula maalum huliwa wakati wa seder

Tafrija za kale kufanyika

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Maelfu ya mahujaji wa kiyahudi wakielekea jerusalem

Rabbi Jacobs anawaelekeza watu dondoo za jinsi ya kutumia simu ya video kwa uwakilishi mzuri zaidi.

"Kimila kuna wakati ambao unahitajika kufungua mlango kwa ajili ya Eliya. Mara nyingi ni vijana wadogo zaidi ndio wanafanya shughuli hiyo wakati wa maadhimisho hayo.

"Anaweza kuwa kijana mdogo zaidi huypo katika nyumba yako sasa lakini wapo maeneo mengine ya nchi.

Wanaweza kutumia simu au tablet zao na kufungua milango ya nyumba zao na kufungua.

"Lakini ukweli ni kwamba ibada hiyo itakuwa ya hisia zaidi , mtu ahisi kuwa mlango wake umefunguliwa na kupokea ukombozi.

"Tunashauri watu watumie Zoom chat na kuuliza, 'Vitu gani wanavitarajia katika maombi yao? Vitu gani wanaridhia zaidi kuvifanya ili kuweza kuponya zaidi ulimwengu?'

"Ukombozi katika janga hili kama ilivyokuwa miaka ya mababu zetu, ndio hicho tunahitaji sasa. Historia ya wayahudi walivyopitia changamoto nyingi inawakumbusha kuwa kuna matumaini ya kukabiliana na changamoto zote."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ijumaa kuu ni kumbukumbu ya siku ya kusulubiwa kwa Yesu Kristo

Baadhi ya watu, mlipuko wa ugonjwa huu umewapa fursa ya kuimarisha imani zao zaidi.

Carole Kutsushi ni mkristo anayeishi jijini Nairobi nchini Kenya.

Wakati taifa limetangaza marufuku ya kutotoka na serikali imewataka watu wakae nyumbani, Shule zikiwa zimefungwa na rais amewataka watu wasikusanyike hata kwenye shughuli za ibada.

Carole ana watoto wawili ambaao sasa wako nyumbani wakati wote na hali imekuwa ngumu kwa sababu ana biashara ndogo .

Licha ya changamoto zilizopo, lakini bado Carole anajaribu kuwa na mtazamo chanya.

Kanisa lake huwa lina sala za jumuiya ambapo kundi dogo la watu wanakutana kwa sala na huwa wanaenda kusali nyumba moja kwa kila wiki.

Sasa wanafanya jumuiya hiyo kupitia mikutano ya simu na kuweza kusali kwa pamoja kwa kutumia Zoom kila Jumanne na Ijumaa.

"Nadhani ni changamoto kidogo lakini ni namna nzuri ya kuwa karibu na Mungu tukiwa nyumbani"

"Nadhani sala hizi za simu za video zimetuweka karibu na Mungu zaidi ya ilivyokuwa awali ".

Sherehe ya Pasaka

Pasaka ni sherehe muhimu sana kwa wakristo, mwaka huu sherehe hiyo itaadhimishwa Aprili 12, kama ishara ya kukumbuka kifa cha Yesu msalabani na kufufuka kwa Kristo.

Watu wengi huwa wanafanya jitihada maalumu za kuhudhuria misa takatifu katika kipindi hiki haswa siku ya Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka.

"Tutaadhimisha siku hii tafatifu ya Ijumaa kuu kwenye simu ya video ya Zoom," says Carole.

"Kwa sababu sasa hali ilivyo ni ngumu kupokea mwili wa Yesu kwa kupata sakramenti ya Komuniyo tukiwa kanisani kama ilivyokuwa kawaida lakini sasa tutatumia ishara ambayo itawasilisha tukio hilo.

"Tutachukua kipande cha mkate wa kawaida tu na juisi ya zabibu na kuziombea na kutumia hizo kama komuniyo.

Yesu anataka sisi tuonyeshe upendo kwa kujaliana", alisema Carole.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ramadan ni wakati wa waislamu kumkumbuka na kumkaribia Mungu

Msimu wa Ramadhani

Mwezi wa Ramadhani unaanza tarehe 23, Aprili.Ni wakati ambao wanakumbuka kitabu kitakatibu cha Qur'an kilipotolewa n na mtume Muhammad.

Waislamu huwa wanafunga chakula na maji wakati wa saa za mchana na kujidhatiti katika sala ili kuimarisha imani zao kuwa karibu na Mola.

Kila jioni jua linapozama, familia na marafiki wanajumuika kwa pamoja kwa ajili ya kufturu.

Wengi huwa wanaenda msikitini kusali.

Lakini jinsi hali inavyoenda, inawezekana utaratibu huo ambao wamezoea hautaweza kufanyika tena kwa mwaka huu.

Afrika Kusini imefunga nchi yake tangu Machi 26, watu wakiwa hawaruhusiwi kutoka nje labda kwa ajili ya mahitaji maalumu ya chakula na dawa.

Marufuku hiyo ilikuwa idumu kwa muda wa wiki tatu lakini hali inavyoenda , marufuku itaongezeka muda.

Sataar Parker ni msemaji wa msikiti mkuu nchini humo Masjidul-Quds uliopo Cape Town,wenye waumini wapatao 5,000.

Yeye anasema, watatumia mitandao ya kijamii kama YouTube na Facebook, ili kufanya maadhimisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Chakula cha Iftar ni fursa ya familia na marafiki kuhitimisha kumalizika kwa kufunga

Futari

Nchini Uingereza, kundi la vijana wa kiislamu wameamua njia ya teknolojia kuadhimisha futari hii.

Kwa kawaida , waislamu huwa wanaweka tent nje n kuandaa chakula ambacho yeyote anakaribishwa kujumuika kula.

Wakati huu ambao mjumuiko wa watu unakatazwa, watu watajumuika kwenye video kwa sala wakati kila mtu ameandaa futari yake akiwa peke yake au mbali na mtu mwingine .