Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 09.04.2020: Coutinho, Rodriguez, Grealish, Hart, Anderson, Willian

Phelippe Coutinho

Chanzo cha picha, BBC/twitter

Chelsea wapo katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kiungo wa Barcelona na Brazili Philippe Coutinho, 27. Nyota huyo wa zamani wa Liverpool kwa sasa yupo kwa mkopo Bayern Munich. (Sport)

Klabu za Manchester United na Napoli zinataka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (AS, in Spanish)

Kiungo wa Aston Villa na England Jack Grealish, 24, ni moja ya kipaumbele cha usajili wa Manchester United. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nyota wa Aston Villa Jack Grealish

Barcelona wametupilia mbali nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Brazil Willian,31, japo atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu. (Sport)

Wakati huohuo Chelsea wamefungua mazungumzo na beki wake Mjerumani Antonio Rudiger, 27, ili asaini mkataba utakaombakiza klabuni hapo hadi walau mwaka 2023. (Sky Sports)

Napoli wanataka kumsajili winga wa West Ham na Brazil Felipe Anderson, 26. (Corriere dello Sport, in Italian)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Beki wa Mjerumani Antonio Rudiger

Klabu ya Besiktas ya Uturuki inapanga kumsajili kipa wa zamani wa timu ya taifa ya England aliyepo klabu ya Burnley kwa sasa, Joe Hart, 32, kama mbadala wa kipa Mjerumani Loris Karius, ambaye anawatumikia kwa mkopo akitokea Liverpool.(Fanatik, in Turkish)

Brighton wanakaribia kumsajili kiungo wa Sydney FC na timu ya taifa ya Australia ya chini ya miaka 17 Cameron Peupion, 17. (Sydney Morning Herald)

Beki Diego Carlos, 27, anasema anafuraha kuwepo katika klabu ya Sevilla licha ya kutakiwa na Liverpool. (Estadio Deportivo, in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nyota wa Liverpool Sadio Mane

Sadio Mane, 27, anasema alifikiria kujiunga na Manchester United kabla ya kuhamia Liverpool. (Times, subscription required)

TETESI ZA SOKA JUMATANO

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

Klabu ya Real Madrid imeahirisha mipango yake ya kumsajili mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 21, kutoka Paris Saint-Germain mpaka 2021 kutokana na janga la virusi vya corona. (AS)

Klabu za Arsenal, Chelsea na Celtic wanamuwania mshambuliaji kinda wa Middlesbrough na timu ya taifa ya chini ya miaka 17 ya Jamhuri ya Ireland Calum Kavanagh, 16. (Sun)

Liverpool imejiunga na msururu wa klabu zinazovutiwa na kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Lille ya Ufaransa Boubakary Soumare, 21. Klabu za Real Madrid, Manchester United, Chelsea na Newcastle pia zinamuwania mchezaji huyo. (Sport)

Maelezo ya picha,

kiungo wa klabu ya Lille ya Ufaransa Boubakary Soumare,

Wakati huo huo, Liverpool wanataka kumsajili beki raia wa Brazili Diego Carlos, 27, kutoka klabu ya Sevilla. (Marca)

Klabu ya AC Milan imetuma maombi ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester City David Silva, 34. Kiungo huyo raia wa Uhispania anamaliza mkataba wake na City mwishoni mwa msimu. (Corriere Dello Sport - in Italian)

AC Milan pia wanaandaa pauni milioni 35 ili kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 24. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Manchester United bado wanahangaika kutafuta klabu itakayomnunua mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 31, kwa kuwa hataki kupunguza mshahara wake. Mshambuliaji huyo wa Chile ambaye yupo kwa mkopo Inter Milan, bado yungali na miaka miwili mpaka mkataba wake na United uishe. (Standard)

Winga Yannick Bolasie, 30, anatarajiwa kurejea Everton kutoka Sporting Lisbon mwishoni mwa msimu kulingana na wakala wake. lakini miamba hiyo ya Ureno haitaki kumsajili moja kwa moja. (Record - in Portuguese)

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton pia pia wanamnyemelea mshambuliaji raia wa Brazil mwenye jina kama lao Everton Soares, 24. Hata hivyo, mshambuliaji huyo mkataba wake na klabu ya Gremio unaelekeza auzwe kwa dau la si chini ya pauni milioni 104. (Mirror)

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez,

Barcelona wanataka kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, kutoka klabu ya Inter Milan lakini wanakabiliana na ushindani mkali kutoka kwa Real Madrid na Manchester City. (Marca)

Klabu ya Wolves haitamuuza Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70 huku winga huyo akihusishwa na mipango ya kuhamia Liverpool. (Football Insider)

Arsenal wanalenga kumsajili beki wa Athletic Bilbao Unai Nunez, 23, kama kipaumbele chao kwa usajili wa majira ya kiangazi. Beki huyo wa Uhispania ana kifungu cha mkataba kinachoelekeza kuuzwa kwa euro milioni 30. (La Razon - in Spanish)

Maelezo ya sauti,

Wachezaji wa Barcelona kupunguziwa mishahara

Maelezo ya picha,

Klabu ya Wolves haitamuuza Adama Troare, 24, kwa dau lolote chini ya pauni milioni 70

Shirikisho la mpira duniani Fifa linapanga kuongeza muda wa moja kwa moja wa msimu wa 2019-20 ili kuruhusu kila nchi kuamua ni lini msimu huo utaisha. (The Athletic - subscription required)

Liverpool, Manchester City na Manchester United wote wameonesha nia ya kumsajili winga wa Uhispania na Valencia Ferran Torres, 20. (Goal)

Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 27, hana mpango wa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Kiungo huyo anahusishwa na uhamisho kuelekea Arsenal na Everton. (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa Manchester United Jesse Lingard, 27, hana mpango wa kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Liverpool wanakusudia kutuma ofa mbili za usajili kwa kiungo wa Uswizi Denis Zakaria na mshambuliaji wa Ufaransa Marcus Thuram wote kutoka klabu ya Borussia Monchengladbach. (Express)

Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, amefanya mazungumzo ya awali juu ya kuongeza mkataba katika klabu ya Chelsea. (Football.London)

Chelsea pia inajipanga kushindana na Arsenal katika mbio za kumsajili beki yaw a Ujerumani Jerome Boateng, ambaye anakaribia kuingia katika miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake na klabu ya Bayern Munich. (Mail)

TETESI ZA SOKA JUMATATU

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Borrusia Dortmund jadon Sancho

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, amekataa uhamisho wa kuelekea Manchester United mwisho wa msimu huu iwapo watashindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa (Sun)

Real Madrid inataka kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane mwenye umri wa miaka 26. (Sport)

Leicester, Newcastle, Crystal Palace na Aston Villa wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Rangers na Colombia Alfredo Morelos, 23. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Ham imekuwa ikiwasiliana na wakala wa mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez huku wakifikiria kumsaini mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal na Manchester United .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan kutoka Man United. (Sport Witness)

Kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania David Silva, 34, huenda akapatiwa mechi ya mwisho ya kumuaga katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu iwapo mlipuko wa coronavirus utamzuia kuwaaga mashabiki wa klabu hiyo baada ya kuichezea klabu hiyo kwa miaka 10 kitu ambacho kimemsaidia kushinda taji la ligi kuu mara. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Aliyekuwa mshambuiaji wa Manchester United na Tottenham Dimitar Berbatov anaamini kwamba mshambuliaji wa klabu ya RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 24, atafurahia kujiunga na Bayern Munich badala ya Liverpool mwisho wa msimu huu . (Mirror)

Leicester, Tottenham na Everton wote wana hamu ya kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 Baptiste Santamaria, ambaye anaichezea klabu ya Angers katika ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa. (Express)

Klabu za ligi ya Premia zimenunua vifaa vyao vya kupima virusi vya corona huku kukiwa na hofu kwamba mechi zitachezwa bila mashabiki. (Star)

Beki wa Uholanzi na Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 22, anakabiliwa na hali ya switofahamu katika klabu hiyo huku mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer akifikiria iwapo anaweza kumuongezea mwaka mmoja katika kandarasi yake (Mirror)

Mshambuliajhi wa Celta Vigo na Urusi Fedor Smolov, 30, alikiuka hatua ya Uhispania kuweka sheria ya kutotoka ndani , akiwa ni mchezaji wa pili wa taifa hilo kwenda kinyume na sheria hiyo kwa kurudi nchini mwake. (AS, in Spanish)