Virusi vya corona: Magenge ya uhalifu yaamua kuweka silaha kando Afrika Kusini

Virusi vya corona: Magenge ya uhalifu yaamua kuweka silaha kando Afrika Kusini

Usitishwaji wa vita usio wa kawaida umeafikiwa katika mji uliojaa magenge ya wahalifu wa Cape Town huku viongozi wa magenge husika wakiamua kusitisha vita na badala yake kuwapelekea chakula wakaazi wasiojiweza.

Huku Afrika kusini ikiwa katikati ya sheria ya kutotoka nje saa 24 ili kujaribu kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona , raia wengi katika jamii masikini wanatatizika kununua bidhaa wanazohitaji.