Virusi vya Corona: Kwanini watu wanaamini ni dhana tu?

Woman and man wearing tinfoil hats

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Taarifa ghushi kuhusu janga hili la kiafya

Ni jambo la kusikitisha kwamba kila janga la kiafya linapotokea lazima kutakuwa na usambaaji wa taarifa za uongo.

Miaka ya 80, 90 na 2000 kulikuwa na taarifa nyingi za uwongo kuhusu Ukimwi - kwa dhana ya kwamba virusi hivyo viliundwa na maabara ya serikali na kwamba kupimiwa kama umepata virusi vya ukimwi ni jambo ambalo halikuwa na uhakika.

Pia kulikuwa na nadharia ya kupotosha kwamba maziwa ya mbuzi ni dawa.

Madai hayo yalifanya watu kutojali zaidi kuhusu tabia zao na kuongeza masaibu ya janga hilo.

Mawazo potofu

Sasa kinachoshuhudia ni usambaaji wa taarifa ghushi za janga la corona.

Kuanzia kwenye mitandao ya Facebook hadi WhatsApp, mara nyingi huwa kuna taarifa za uwongo kama vile mlipuko wa janga hilo na hata namna unavyoweza kujikinga usiuguie.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Miongo ya nyumba, taarifa za uwongo kuhusu ukimwi kulifanya jana hilo kuwa baya zaidi

Kibaya zaidi nikwamba, taarifa hizo zinazosambazwa zina madhara yake - mfano, taarifa ya hivi karibuni kutoka kwa moja ya mikoa nchini Iran, ilibaini kwamba watu zaidi waliaga dunia kwasababu ya kunywa pombe ya kienyeji kwa misingi ya taarifa za uwongo zilizosamba eti pombe hiyo ilikuwa na uwezo wa kuwalinda dhidi ya Covid-19 kabla kirusi hakijaingia. .

Lakini pia mawazo kama hayo yanaweza kukushawishi wewe na wengine kujihisi kwamba muko salama, na kupuuza sheria zilizowekwa na serikali na kupoteza imani na maafisa wa serikali na mashirika husika.

Kuna ushahidi unaoonesha kwamba dhana kama hizo zinasambaa

Madai ya mwanadamu ya uwongo

Kulingana na kura ya maoni iliyoendeshwa na shirika la YouGov, Machi 2020, ilibainika kwamba asilimia 13 ya raia wa Marekani wanaamini kuwa janga la Covid-19 ni uvumi tu na kwamba kuna uwezekano mkubwa janga hili limetokana na mwanadamu.

Wakati ukitarajia kwamba akili au elimu vinaweza kuwa na mchango mkubwa kubaini lipi ni kweli na lipi ni uwongo, ni rahisi sana kupata mifano ya watu walioelimika ambao pia nao wananaswa katika taarifa hizi za uwongo zinazosambaa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kelly Brogan ana shahada ya udaktari kutoka chuo kikuu cha Cornell, lakini pia naye amehiji nadharia ya kirusi cha Covid-19 na uwepo wake

Tafakari hili, mwandishi Kelly Brogan, ana shahada kutoka taasisi ya teknolojia ya Massachusetts na pia alisomea magonjwa ya akili chuo kikuu cha Cornell .

Ameonesha wazi kuwa anahoji hatari ya virusi hivyo kwa nchi kama China na Italia. Brogan aliendelea na kuhoji chanzo cha nadharia ya virusi vyenyewe huku akizungumzia nadharia bandia.

Hata kwa baadhi ya viongozi duniani - ambao ungetegemea wangekuwa na ufahamu mzuri zaidi linapokuja suala la uvumi usio na misingi - pia nao wamekuwa wakisambaza taarifa za uwongo kuhusu hatari ya mlipuko huo na kuendeleza tiba ambayo bado haijaihinishwa ambazo huenda zikawa na mdhara.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais wa Brazil Bolsonaro alijipata katika ukiukaji wa sheria za Facebook baada ya kuhamasisha watu juu ya dawa aliodai inaponya

Hilo lilisababisha mitandao ya Twitter na Facebook kuchukua hatua ambayo haijawahi kutolewa hapo kabla za kuondoa ujumbe uliotumwa na Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na wa Brazil Jair Bolsonaro mtawalia.

Kwa bahati nzuri, wanasaikolojia yatari wanafatilia hali hii.

Na kile watakachobaini huenda ikatoa mwongozo wa njia mpya za kujilinda kuokana na taarifa za uwongo na kusaidia kuzuia kusambaa za taarifa za uwongo na taia mbovu.

Habari nyingi kupita kiasi

Sehemu ya tatizo hilo linatokana na uhalisia wa taarifa zenyewe.

Tunapokea taarifa tele, siku nzima, kila siku na hivyobasi huwa tunategemea hisia zetu kuamua kama kitu fulani ni sahihi au la.

Msambazaji wa taarifa za uwongo anaweza kufanya taarifa yake ikaonekana kuwa kweli kwa kutumia mbinu ambazo zinatuzuia kufikiria na kuhoji alichosema kama vile kuangalia chanzo cha taarifa yake.

Kama vile mwandishi wa utafiti mmoja alivyosema: "When thoughts flow smoothly, people nod along."Mawazo yako ukiyapanga vizuri, watu watafuata tu kila kitu utakachosema."

Eryn Newman katika chuo kikuu cha taifa cha Australia, kwa mfano, ameonesha kwamba picha tu ya kawaida ikiwa na maelezo inaongeza uaminifu kwa uhakika wa taarifa yenyewe - hata kama itakuwa na umuhimu kidogo kwa dai lenyewe.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hisia za kwamba unamjua tu kunaweza kufanya mtu asifikirie kutathmini taarifa aliyotumiwa kama ni ya kweli au uwongo

Kwahiyo kadiri tunapoona kitu katika taarifa zetu, uwezo wa kuamini taarifa hiyo unaongezeka hata kama awali tulikuwa na mashaka na taarifa yenyewe.

Kusambaza taarifa bila kufukiria mara mbili

Njia kama hizi zimefahamika kwa muda mrefu na wanaotoa taarifa kutaka kubadilisha fikra za wengine ama wanaosambaza taarifa za uwongo lakini mitandao ya kijamii hii leo inatuweka kuwa katika hatari ya kuwa waathirika.

Ushahidi wa hivi karibni unaonesha kwamba watu wengi wanashirikisha wengine taarifa wanazopokea bila hata kufikiria kuhusu ukweli wa ujumbe wenyewe.

Gordon Pennycook, mtafiti mkuu kuhusu taarifa za kupotosha kisaikolojia katika chuo kikuu cha Regina, Canada, alitaka washiriki watathmini mchanganyiko wa taarifa zenye ukweli na uwongo kuhusu mlipuko wa viusi vya corona.

Walipoulizwa kutathmini kuhusu ukweli wa taarifa, washiriki walisema taarifa za uwongo ni jambo la kweni kwa asilimia 25 ya muda unaotumika.

Na walipoulizwa ikiwa wanaweza kutumia wengine taarifa hio, karibia asilimia 35 walisema ndio wanaweza kusambaza taarifa za uwongo kwa watu wengine takriban asilimia 10.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Utafiti unaonesha kwamba watu wengi wanatumia wengine taarifa za uwongo kwasababu ya vichwa vya habari husika

"Utafiti huo unamaanisha kwamba watu wanashirikisha wengine taarifa ambazo wenyewe walikuwa na uwezo wa kujua ikiwa zilikuwa za uwongo iwapo wangefikiria tena kidogo tu.

Pengine walikuwa wakifikiria kwamba taarifa hiyo inaweza kupendwa zaidi na watu kwa kubofya kitufe cha 'like' ama wengine nao wangeisambaza kwa ingi badala ya kuanza kufikiria kuhusu uhalisia wake.

"Mitandao ya kijamii haitoi taariza za ukweli," Pennycock amesema.

Au pengine walifikiria wangetoa jukumu la kufikiria na kutathmini taarifa hiyo kwa wengine: Wat wengi wamekuwa wakitoa taarifa za uwongo lakini wanatoa ilani mwanzo kabisa, kama vile, "sina uhakika kama taarifa hii ni ya ukweli…".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kukabiliana na taarifa za uwongo, ni muhimu kuzingatia ukweli

Pia wanaweza kuanza kufikiria kwamba iwapo taarifa hiyo itakuwa na ukweli wowote, inaweza kuwa msaada kwa marafiki na wanaowafuatilia katika mitandao ya kijamii na iwapo basi itakuwa ya uwongo, haitakuwa na madhara yoyote kao, kwahiyo kitu cha msingi hapo ni kutumia wengine taarifa hiyo bila kujua kwamba hatua hiyo inaweza kusababisha madhara pia.

Wacha kusambaza

Katika kuhakikisha ukweli -hali ambayo mtu hutingisha kichwa tu anapoamini jambo, mashirika yanayojaribu kuthibitisha dhana hiyo yaepuke kuwa na vigezo vingi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kukabiliana na taarifa za uwongo, ni muhimu kuzingatia ukweli

Badala yake yanastahili kubainisha ukweli pengine kwa usaidizi wa picha, jedwali au grafu yanayofanya mawazo kueleka kwa urahisi zaidi.

Siyo sahihi kutoa tu azo zuri na kutarajia kwamba kila mmoja alitilia maanani.

Acha kujirejelelea

Kampeni za kubainisha uwongo na ukweli zinastahili kuepuka kujirudia.

Kujirejelelea kunafanya mtu ahisi kwamba hilo wazo analifahamu zaidi, na kuongeza uwezekano wa dhana ya ukweli.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kujirejelelea kunafanya taarifa ya uwongo ionekane kama inafahamika

Sio kwamba hilo hutokea kwa asilimia 100, lakini kampeni kama hizo pia zinaweza kujaribu ukweli ufahamike zaidi na kukumbukwa badala ya ile dhana, na hivyobasi itakuwa rahisi jambo kama hilo kusalia akilini mwa mtu.

Tujitathmini wenyewe

Linapokuja suala la tabia yetu mtandaoni, tunaweza kuepuka kuzingatia hisia zetu na kufikiria zaidi kuhusu ukweli wa taarifa husika kabla ya kusambaza kwa mwengine.

Je taarifa hiyo inazingatia alichosema mtu binafsi au ushahidi wa kisayansi, je unawezaje kufahamu chanzo cha taarifa hiyo? Na je mwandishi anatumia uwongo kuthibitisha taarifa yake?

Hayo ndio baadhi ya maswali tunastahili kujiuliza badala ya je ujumbe huo utapendwa na wengi, ama kama itakuwa na manufaa yoyote kwa wengine.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kitu kimoja ambacho tunaweza kufikiria ni kuhusu ukweli wa taarifa yenyewe kabla ya kuisambaza

Pia kuna ushahidi kwamba kila mmoja anaweza kuwa na mazoea ya maswali kama hayo.

Gordon Pennycook anapendekeza kwamba mitandao ya kijamii inaweza kusihi watumiaji wawe waangalifu zaidi.

Kiuhalisia, inaweza kuwa jambo rahisi tu, kujenga mazoea ya kuhakiki na kutathmni taarifa kabla ya kuutuma kwa mwengine, ingawa pia kampuni hizo zinaweza kupata nia nyengine za kuamika za kuhakiki taarifa, amesema.

Lakini hakuna suluhisho la moja kwa moja.

Kama ilivyo kwa jaribio letu la kukabilina na virusi vya corona, ikiwa kutahitajika njia zingine kukabiliana na usambazaji wa taarifa za uwongo

Na wakati janga hilo linaongezeka, ni jukumu la kila mmoja kukabilipambana na usambaaji huo wa taarifa ghushi.